Kifo cha Abu Ubaydan Al Banshiri katika MV Bukoba

KWA MSAADA WA MASHIRIKA MBALIMBALI..

Mungu awarehemu wote waliopoteza maisha katika ajali ya meli ya MV BUKOBA, tarehe kama ya leo, miaka 22 iliyopita.
Umbali wa maili kama 30, sawa na kilometa 56, meli hiyo ilizama mita 25 chini ya maji ya ziwa Victoria. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1979, meli ya MV Bukoba ilikuwa chini ya umiliki wa Shirika la Reli; TRC, pamoja na meli zingine za MV Serengeti ya ziwa Victoria na MV Mwongozo ya ziwa Tanganyika na zingine huko ziwa Nyasa. Shirika la Reli lilichukua jukumu la kuendesha huduma za meli baada ya jumuia ya Afrika mashariki kuvunjika mwaka 1977.
Tarehe 21 mei 1996, meli ilitoka Bukoba ikiwa na abiria wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 1000. Abiria 443 walikuwa katika daraja la kwanza na la pili huku daraja la tatu likiwa na abiria wengi kuliko uwezo wake. Meli hiyo ilikuwa uwezo wa kubeba tani 850, lakini mara kwa mara katika safari zake ilibeba mizigo mingi yenye uzito mkubwa zaidi.
Kapteni Joseph Muguthi, aliyekuwa kapteni wa chombo hicho, mkenya aliyehudumu katika jeshi la maji la Kenya na mwandishi wa gazeti la Nairobi Daily News, alilaumu mamlaka kwa kupuuza mambo muhimu katika huduma za usafiri wa majini. Upungufu wa vifaa vya uokozi, waendesha meli wasiokuwa na ujuzi, kutokuwa na ratiba maalum ya kufanya marekebisho na kutokuwepo kwa utaratibu mzuri wa ukaguzi, zilitajwa kuwa sababu zilizopelekea ajali ya MV Bukoba. Jambo moja la kushangaza ni kwamba, ilibidi waokoaji watoke Afrika ya kusini, na kweli walifika, kuokoa mabaki ya meli. Taarifa za kiserikali zinadai watu 864 walipoteza maisha, vyanzo vingine vinadai watu zaidi ya 1000 walipoteza maisha.
Baadhi ya maofisa wa TRC walifunguliwa mashitaka baada ya tukio hilo. Na mwaka 1997, kitengo cha usafirishaji wa majini kilijitenga kutoka TRC na kujitegemea.

Wanaume, Wanawake na watoto walipoteza maisha. Mnara wa kumbukumbu ulijengwa kuwaenzi marehemu hao, na Rais Benjamin Mkapa alitangaza siku tatu za maombolezo.
Mungu awarehemu.

Hata hivyo, miongoni mwa ndugu waliopoteza maisha, alikuwako pia mmoja wa watu hatari duniani wakati huo. Jina lake hasa la kuzaliwa ni Ali Al Amin 'Ali al-Rashid, Lakini katika shughuli zake alijulikana kama Abu 'Ubayda al-Banshiri. Jina hilo alijipa akiwa nchini Pakistan miaka ya 1980 hadi 1989 akiwa katika mapambano dhidi ya vikosi vya umoja wa nchi za muungano wa ki-isovieti, akishirikiana na Ahmed Shah Massoud aliyekuja kuwa kiongozi wa Takriban wakati mauti yakimfika Al- Rashidi.

Haifahamiki hasa alizaliwa tarehe gani, lakini ni mwezi wa tano mwaka 1950 huko mjini Cairo nchini Misri. Al Rashidi, pengine alijua siku moja atakufa kwa bomu au kwa risasi, au kwa mateso ya CIA huko Guantanamo Bay, lakini alikufa kwa maji wakati akiwa mtu mwenye nguvu katika Al Qaeda, nafasi ya pili tu baada ya Osama Bin Laden wakati huo.

Al Rashid alianza kuwa mtumishi katika jeshi la polisi la Misri. Lakini serikali ya Misri iliwafukuza askari wengi waliokuwa waislamu wenye misimamo mikali, Al Rashid akiwa mmoja wao.

Historia yake inaanzia mwaka 1981 wakati wa mauaji ya Rais Anwar Al Saddat wa Misri. Moja ya wahusika wa mauaji hayo ni Abd-Hamid ‘Abd al-Salam, aliyekuja kuwa shemeji wa al-Rashidi, baada ya wote kuoa ndugu wa familia moja, huko Kenya. Ni mwaka 1983 ambapo Al Rashid alifunga ndoa na Hafsah Sa'd Rwashan.

Al Rashid na mkewe walihamia Jedda Saudi Arabia katika nyumba iliyomilikiwa na Osama Bin Laden, na baadye walihamia Medina katika nyumba ya Mohammed Matawi. Hapo waliishi kwa siku kumi tu, na kisha kutimkia Pakistan. Mke wa Al Rashid, Hafsah alikuja kueleza kuwa safari hizo ziligharamiwa na mtu asiyemjua. Katika mji wa Peshawar huko Pakistan, Al Rashid alijiunga katika kambi la mafunzo la Sada, akijitambulisha kama Abu Ubayda. Ndipo alipokutana na Ayman Al Zawahiri, aliyemtambulisha kwa Osama Bin Laden.
Osama alimkubali sana Al Rashidi. Walikuwa marafiki na walianzisha makundi mengi ya jihadi huko Pakistan. Mafanikio yao makubwa yaliyowapa umaarufu ni katika kile kilichoitwa "Battle of Jaji".
Katika mapambano hayo makali ya mjini Jaji, kikosi cha akina Osama na Al Rashid kiliwashinda kikosi maridadi cha jeshi la sovieti kilichoundwa na makomandoo wa Spetsnaz, wenye ujuzi mkubwa sawa na Navy Seal ya US, au Sayeret Matkal ya Israel.
Lakini baada ya mapambano hayo, baadhi ya vikosi vya jihad vilishindwa kutoa ushirikiano kwa Osama na wenzake.
Mkutano wa siku nne wa Tarehe 17-20 Agosti 1988, Al-Rashidi akiwa na Osama bin Laden, Wael Julaidan na
Mamdouh Mahmud Salim walijadili na kuanzisha Al Qaeda. Ingawa jina hilo lilikuwapo awali, lakini kundi rasmi lilianzishwa katika mkutano huo.

Kwa maneno yake Osama bin Laden, mnamo October 21, 2001, anakumbusha, kwamba "jina la Al Qaeda ni la zamani sana. Lakini kaka Al Rashid alianzisha mafunzo ya vijana wa kupambana dhidi ya manyanyaso ya wasovieti, ndipo jina Al Qaeda, "The base" lilipokolea"

Kundi la Al Qaeda lilijikita zaidi nchini Afghanistan na kuanzisha Makambi mengi ya mafunzo. Mwaka 1990, Al Qaeda walifikiria kutanua mapambano nje ya Afghanistan, wazo lilopelekea kuanzisha shughuli zake nchini Sudan. Lakini kwanza ilibidi wapitie Yemen, na mwaka 1992 walifika Sudan. Al Rashid aliratibu shughuli za Al Qaeda huko Yemen na katika Pembe ya Afrika, Sudan, Somalia, Kenya, Tanzania na Uganda.
Mwaka 1993, mkutano wa Al Rashid na Osama bin Laden uliamua kuanza kushambulia vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyopo nchini Somalia na kwingineko Afrika. Baadae wazo hilo lilikua na kujumuisha balozi za Marekani.
Ili kuficha shughuli zao, Al Rashid na wenzake Muhammed Atef, and
Mohammed Sadiq Odeh walianzisha biashara ya uvuvi mjini Mombassa, Kenya mwaka 1994.
Pia, Al Rahid na Wadih Al Hage walianzisha makampuni ya kuuza Vito vya thamani, Dhahabu na Tanzanite kutoka Mererani, Arusha, kwa ajili ya kupata fedha za kuendesha shuguli zao.
Taarifa za shirika la kijasusi la ndani la Marekani, FBI, zinadai kwamba Al Rashid alimiliki ardhi mjini Mwanza, alikuwa na kampuni iliyoitwa Taheer Ltd aliyoianzisha mwaka 1993, ambayo kwa mujibu wa "global witness ", kampuni hiyo ilijihusisha na biashara ya Magendo ya Alimasi, kutoka Mwadui na/au Congo, pamoja na shughuli za kutakatisha fedha.
Rafiki yake Al Rashid, Wahid Al Hage alimiliki kampuni ya Tanzanite King, iliyojihusisha na biashara ya madini ya Tanzanite pamoja na Almasi zilizopatikana kimagendo kutoka kampuni ya Taheer Ltd.
Ili kuficha zaidi shuguli zao za kigaidi, Al Rashid na Al Hage walianzisha mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya kusaidia watu masikini katika pembe ya Afrika, mfano, "Mercy International Relief Agency" na
"Help Africa People".

Haitegemewi mtu wa aina ya Al Rashid asheherekee siku ya kuzaliwa, labda pengine ilikuwa ndio siku yake ya kufa. Mei 21, 1996 alimaliza kazi wakati akiandaa kazi ya kulipua ofisi za ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya. Hakuishi kuona ndoto hiyo ikitimia. Lakini alikwishandaa mtandao.
Vyanzo vingine vinadai, Al Rashid alisafiri ndani ya MV Bukoba kuelekea Mwanza akiwa katika kutafuta mali ghafi za kutengeneza bomu-chafu, hakufika.

Baada ya kifo Chake, Kundi la Al Qaeda liliwatuma Fazul Mohammed Abdullah na Wadih Al Hage ili kuhakikisha kuwa kweli Al Rashid amekufa na kwamba kifo hiko kilitokana na ajali na sio mauaji ya kupangwa.
 
Kama kweli huyo gaidi alikua kwenye MV Bukoba CIA hawashindwi kuzamisha meli yenye watu 1000 ilimradi wampate mtu wao.
 
Sia
Mkuu paragraph ya 3 kutoka mwisho hapo sijakuelewa vizuri.
Alikuwa anasafiri kuelekea Bukoba. Mbona Mv Bukoba ilipata ajali ikiwa inatoka Bukoba kuitafuta Mwanza.?
Siachi JF ng'oo yaani nimecheka stress zote kwishney.
 
Hizi mambo za ugaidi zinatumika sana kuondoa uhai wa witness people, pamoja na ile meli kuanguka na kuua watu zaidi ya 800.

Kitu nilichojifunza hapa ni hawa magaidi kutumia pesa haramu kuwekeza kwenye nchi zilizo kwenye mipango yao ya kigaidi.

Kuna tatizo sana hapo.
 
Habari kama hizi nimeshawahi kusoma sana na kwa jinsi zinavyopangika na tarehe zake unaweza na nimewahi kunasa katika kuziamini na kuchukia watu bila msingi.Iko siku zilianndikwa zikamhusu mtu ninayemfahamu na kuzunguka kote Kenya,Tanzania,Msumbiji na kwengineko lakini takriban mia kwa mia tulijua ni uongo. Yule mhusika akacheka na kupuuzilia mbali na akamuelekea Mwenyezi Mungu kwa litakalomkuta.Sisi nasi tukafanya kama yeye.Twashukuru labda wale waliotunga uzushi ule nao walishtuka kwamba wamezidisha chumvi nao wakakaa kimya.Na mpaka leo yule jamaa yuko salama Mungu amemlinda.
Kwa mfano kwenye kisa cha huyo alRashid yawezekana muandishi hawezi kuonesha shamba lake huko Mwanza na miradi yote mengine iliyotajwa inayomuhusu ikawa ni miradi ya kuganga njaa tu na hakuwa na madhumuni mabaya kama ilivyoorodheshwa.
 
Mkuu paragraph ya 3 kutoka mwisho hapo sijakuelewa vizuri.
Alikuwa anasafiri kuelekea Bukoba. Mbona Mv Bukoba ilipata ajali ikiwa inatoka Bukoba kuitafuta Mwanza.?
Vyanzo vingine vinadai, Al Rashid alisafiri ndani ya MV Bukoba kuelekea Mwanza akiwa katika kutafuta mali ghafi za kutengeneza bomu-chafu, hakufika.
 
Vyanzo vingine vinadai, Al Rashid alisafiri ndani ya MV Bukoba kuelekea Mwanza akiwa katika kutafuta mali ghafi za kutengeneza bomu-chafu, hakufika.
Mwanzo alisema alikuwa katika matayarisho ya kuripua balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania na kwamba hakuishi na kuona mafanikio ya matayarisho ya kazi yake. Huyu hata Mwanza hakufika lakini tuliambiwa mabomu yaliripuka.Nani aliyemalizia kazi yake. Na kwa nafasi yake aliyokuwa chini ya Osama,ni nani huyo aliyekuwa hodari kuliko yeye aliyechaguliwa na kumalizia kazi.
 
Mwanzo alisema alikuwa katika matayarisho ya kuripua balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania na kwamba hakuishi na kuona mafanikio ya matayarisho ya kazi yake. Huyu hata Mwanza hakufika lakini tuliambiwa mabomu yaliripuka.Nani aliyemalizia kazi yake. Na kwa nafasi yake aliyokuwa chini ya Osama,ni nani huyo aliyekuwa hodari kuliko yeye aliyechaguliwa na kumalizia kazi.
Haitegemewi mtu wa aina ya Al Rashid asheherekee siku ya kuzaliwa, labda pengine ilikuwa ndio siku yake ya kufa. Mei 21, 1996 alimaliza kazi wakati akiandaa kazi ya kulipua ofisi za ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya. Hakuishi kuona ndoto hiyo ikitimia. Lakini alikwishandaa mtandao.
 
KWA MSAADA WA MASHIRIKA MBALIMBALI..

Mungu awarehemu wote waliopoteza maisha katika ajali ya meli ya MV BUKOBA, tarehe kama ya leo, miaka 22 iliyopita.
Umbali wa maili kama 30, sawa na kilometa 56, meli hiyo ilizama mita 25 chini ya maji ya ziwa Victoria. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1979, meli ya MV Bukoba ilikuwa chini ya umiliki wa Shirika la Reli; TRC, pamoja na meli zingine za MV Serengeti ya ziwa Victoria na MV Mwongozo ya ziwa Tanganyika na zingine huko ziwa Nyasa. Shirika la Reli lilichukua jukumu la kuendesha huduma za meli baada ya jumuia ya Afrika mashariki kuvunjika mwaka 1977.
Tarehe 21 mei 1996, meli ilitoka Bukoba ikiwa na abiria wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 1000. Abiria 443 walikuwa katika daraja la kwanza na la pili huku daraja la tatu likiwa na abiria wengi kuliko uwezo wake. Meli hiyo ilikuwa uwezo wa kubeba tani 850, lakini mara kwa mara katika safari zake ilibeba mizigo mingi yenye uzito mkubwa zaidi.
Kapteni Joseph Muguthi, aliyekuwa kapteni wa chombo hicho, mkenya aliyehudumu katika jeshi la maji la Kenya na mwandishi wa gazeti la Nairobi Daily News, alilaumu mamlaka kwa kupuuza mambo muhimu katika huduma za usafiri wa majini. Upungufu wa vifaa vya uokozi, waendesha meli wasiokuwa na ujuzi, kutokuwa na ratiba maalum ya kufanya marekebisho na kutokuwepo kwa utaratibu mzuri wa ukaguzi, zilitajwa kuwa sababu zilizopelekea ajali ya MV Bukoba. Jambo moja la kushangaza ni kwamba, ilibidi waokoaji watoke Afrika ya kusini, na kweli walifika, kuokoa mabaki ya meli. Taarifa za kiserikali zinadai watu 864 walipoteza maisha, vyanzo vingine vinadai watu zaidi ya 1000 walipoteza maisha.
Baadhi ya maofisa wa TRC walifunguliwa mashitaka baada ya tukio hilo. Na mwaka 1997, kitengo cha usafirishaji wa majini kilijitenga kutoka TRC na kujitegemea.

Wanaume, Wanawake na watoto walipoteza maisha. Mnara wa kumbukumbu ulijengwa kuwaenzi marehemu hao, na Rais Benjamin Mkapa alitangaza siku tatu za maombolezo.
Mungu awarehemu.

Hata hivyo, miongoni mwa ndugu waliopoteza maisha, alikuwako pia mmoja wa watu hatari duniani wakati huo. Jina lake hasa la kuzaliwa ni Ali Al Amin 'Ali al-Rashid, Lakini katika shughuli zake alijulikana kama Abu 'Ubayda al-Banshiri. Jina hilo alijipa akiwa nchini Pakistan miaka ya 1980 hadi 1989 akiwa katika mapambano dhidi ya vikosi vya umoja wa nchi za muungano wa ki-isovieti, akishirikiana na Ahmed Shah Massoud aliyekuja kuwa kiongozi wa Takriban wakati mauti yakimfika Al- Rashidi.

Haifahamiki hasa alizaliwa tarehe gani, lakini ni mwezi wa tano mwaka 1950 huko mjini Cairo nchini Misri. Al Rashidi, pengine alijua siku moja atakufa kwa bomu au kwa risasi, au kwa mateso ya CIA huko Guantanamo Bay, lakini alikufa kwa maji wakati akiwa mtu mwenye nguvu katika Al Qaeda, nafasi ya pili tu baada ya Osama Bin Laden wakati huo.

Al Rashid alianza kuwa mtumishi katika jeshi la polisi la Misri. Lakini serikali ya Misri iliwafukuza askari wengi waliokuwa waislamu wenye misimamo mikali, Al Rashid akiwa mmoja wao.

Historia yake inaanzia mwaka 1981 wakati wa mauaji ya Rais Anwar Al Saddat wa Misri. Moja ya wahusika wa mauaji hayo ni Abd-Hamid ‘Abd al-Salam, aliyekuja kuwa shemeji wa al-Rashidi, baada ya wote kuoa ndugu wa familia moja, huko Kenya. Ni mwaka 1983 ambapo Al Rashid alifunga ndoa na Hafsah Sa'd Rwashan.

Al Rashid na mkewe walihamia Jedda Saudi Arabia katika nyumba iliyomilikiwa na Osama Bin Laden, na baadye walihamia Medina katika nyumba ya Mohammed Matawi. Hapo waliishi kwa siku kumi tu, na kisha kutimkia Pakistan. Mke wa Al Rashid, Hafsah alikuja kueleza kuwa safari hizo ziligharamiwa na mtu asiyemjua. Katika mji wa Peshawar huko Pakistan, Al Rashid alijiunga katika kambi la mafunzo la Sada, akijitambulisha kama Abu Ubayda. Ndipo alipokutana na Ayman Al Zawahiri, aliyemtambulisha kwa Osama Bin Laden.
Osama alimkubali sana Al Rashidi. Walikuwa marafiki na walianzisha makundi mengi ya jihadi huko Pakistan. Mafanikio yao makubwa yaliyowapa umaarufu ni katika kile kilichoitwa "Battle of Jaji".
Katika mapambano hayo makali ya mjini Jaji, kikosi cha akina Osama na Al Rashid kiliwashinda kikosi maridadi cha jeshi la sovieti kilichoundwa na makomandoo wa Spetsnaz, wenye ujuzi mkubwa sawa na Navy Seal ya US, au Sayeret Matkal ya Israel.
Lakini baada ya mapambano hayo, baadhi ya vikosi vya jihad vilishindwa kutoa ushirikiano kwa Osama na wenzake.
Mkutano wa siku nne wa Tarehe 17-20 Agosti 1988, Al-Rashidi akiwa na Osama bin Laden, Wael Julaidan na
Mamdouh Mahmud Salim walijadili na kuanzisha Al Qaeda. Ingawa jina hilo lilikuwapo awali, lakini kundi rasmi lilianzishwa katika mkutano huo.

Kwa maneno yake Osama bin Laden, mnamo October 21, 2001, anakumbusha, kwamba "jina la Al Qaeda ni la zamani sana. Lakini kaka Al Rashid alianzisha mafunzo ya vijana wa kupambana dhidi ya manyanyaso ya wasovieti, ndipo jina Al Qaeda, "The base" lilipokolea"

Kundi la Al Qaeda lilijikita zaidi nchini Afghanistan na kuanzisha Makambi mengi ya mafunzo. Mwaka 1990, Al Qaeda walifikiria kutanua mapambano nje ya Afghanistan, wazo lilopelekea kuanzisha shughuli zake nchini Sudan. Lakini kwanza ilibidi wapitie Yemen, na mwaka 1992 walifika Sudan. Al Rashid aliratibu shughuli za Al Qaeda huko Yemen na katika Pembe ya Afrika, Sudan, Somalia, Kenya, Tanzania na Uganda.
Mwaka 1993, mkutano wa Al Rashid na Osama bin Laden uliamua kuanza kushambulia vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyopo nchini Somalia na kwingineko Afrika. Baadae wazo hilo lilikua na kujumuisha balozi za Marekani.
Ili kuficha shughuli zao, Al Rashid na wenzake Muhammed Atef, and
Mohammed Sadiq Odeh walianzisha biashara ya uvuvi mjini Mombassa, Kenya mwaka 1994.
Pia, Al Rahid na Wadih Al Hage walianzisha makampuni ya kuuza Vito vya thamani, Dhahabu na Tanzanite kutoka Mererani, Arusha, kwa ajili ya kupata fedha za kuendesha shuguli zao.
Taarifa za shirika la kijasusi la ndani la Marekani, FBI, zinadai kwamba Al Rashid alimiliki ardhi mjini Mwanza, alikuwa na kampuni iliyoitwa Taheer Ltd aliyoianzisha mwaka 1993, ambayo kwa mujibu wa "global witness ", kampuni hiyo ilijihusisha na biashara ya Magendo ya Alimasi, kutoka Mwadui na/au Congo, pamoja na shughuli za kutakatisha fedha.
Rafiki yake Al Rashid, Wahid Al Hage alimiliki kampuni ya Tanzanite King, iliyojihusisha na biashara ya madini ya Tanzanite pamoja na Almasi zilizopatikana kimagendo kutoka kampuni ya Taheer Ltd.
Ili kuficha zaidi shuguli zao za kigaidi, Al Rashid na Al Hage walianzisha mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya kusaidia watu masikini katika pembe ya Afrika, mfano, "Mercy International Relief Agency" na
"Help Africa People".

Haitegemewi mtu wa aina ya Al Rashid asheherekee siku ya kuzaliwa, labda pengine ilikuwa ndio siku yake ya kufa. Mei 21, 1996 alimaliza kazi wakati akiandaa kazi ya kulipua ofisi za ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya. Hakuishi kuona ndoto hiyo ikitimia. Lakini alikwishandaa mtandao.
Vyanzo vingine vinadai, Al Rashid alisafiri ndani ya MV Bukoba kuelekea Mwanza akiwa katika kutafuta mali ghafi za kutengeneza bomu-chafu, hakufika.

Baada ya kifo Chake, Kundi la Al Qaeda liliwatuma Fazul Mohammed Abdullah na Wadih Al Hage ili kuhakikisha kuwa kweli Al Rashid amekufa na kwamba kifo hiko kilitokana na ajali na sio mauaji ya kupangwa.
Simulizi nzuri...Kwa msomaji aelewe: unaposoma simulizi kama hizi ni vyema ukatafuta na vyanzo vingine kuhakiki ukweli wake na sio kuamini tu.
 
Nakumbuka vyema iyo siku tukiwa Kule mwanza.....mzee wangu aliamishiwa kikazi Kule MZA.....

Nakumbuka vyema miti ya Nyerere zamani iliitwa nje ya jiji la mwanza jirani na Sasa lake oil gas...

Kuzama Kwa Mv bukoba kulitufanya kuogopa sana usafir wa meli nakumbuka for the first time nimechaguliwa kuji Unga na Moja ya shule kongwe Tanzania...Niliogopa sana meli Kule tuli ita "BATA"
Nyegera waitu nyingi sana Kule 😊

Baadae tukazoea ni miaka Mingi Sasa sijawai Rudi Kule namkumbuka rafik wa Dhati wa baba angu na co_worker alikaa Rwamishenye....Nilienda badilisha misosi pale😊😊

Mm pia Niwewai nusurika kuzama ziwa Victoria several times....

Endeleen kupumzika Kwa amani wote wote walio poteza maisha kwenye Mv bukoba....
 
Touching ...
 
AJALI YA MV BUKOBA ILIUA WATU NA MTU.

Mungu awarehemu wote waliopoteza maisha katika ajali ya meli ya MV BUKOBA, tarehe kama ya leo, miaka 22 iliyopita.

Umbali wa maili kama 30, sawa na kilometa 56, meli hiyo ilizama mita 25 chini ya maji ya ziwa Victoria. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1979, meli ya MV Bukoba ilikuwa chini ya umiliki wa Shirika la Reli; TRC, pamoja na meli zingine za MV Serengeti ya ziwa Victoria na MV Mwongozo ya ziwa Tanganyika na zingine huko ziwa Nyasa. Shirika la Reli lilichukua jukumu la kuendesha huduma za meli baada ya jumuia ya Afrika mashariki kuvunjika mwaka 1977.

Tarehe 21 mei 1996, meli ilitoka Bukoba ikiwa na abiria wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 1000. Abiria 443 walikuwa katika daraja la kwanza na la pili huku daraja la tatu likiwa na abiria wengi kuliko uwezo wake. Meli hiyo ilikuwa uwezo wa kubeba tani 850, lakini mara kwa mara katika safari zake ilibeba mizigo mingi yenye uzito mkubwa zaidi.

Kapteni Joseph Muguthi, aliyekuwa kapteni wa chombo hicho, mkenya aliyehudumu katika jeshi la maji la Kenya na mwandishi wa gazeti la Nairobi Daily News, alilaumu mamlaka kwa kupuuza mambo muhimu katika huduma za usafiri wa majini. Upungufu wa vifaa vya uokozi, waendesha meli wasiokuwa na ujuzi, kutokuwa na ratiba maalum ya kufanya marekebisho na kutokuwepo kwa utaratibu mzuri wa ukaguzi, zilitajwa kuwa sababu zilizopelekea ajali ya MV Bukoba. Jambo moja la kushangaza ni kwamba, ilibidi waokoaji watoke Afrika ya kusini, na kweli walifika, kuokoa mabaki ya meli. Taarifa za kiserikali zinadai watu 864 walipoteza maisha, vyanzo vingine vinadai watu zaidi ya 1000 walipoteza maisha.

Baadhi ya maofisa wa TRC walifunguliwa mashitaka baada ya tukio hilo. Na mwaka 1997, kitengo cha usafirishaji wa majini kilijitenga kutoka TRC na kujitegemea.

Wanaume, Wanawake na watoto walipoteza maisha. Mnara wa kumbukumbu ulijengwa kuwaenzi marehemu hao, na Rais Benjamin Mkapa alitangaza siku tatu za maombolezo.
Mungu awarehemu.

Hata hivyo, miongoni mwa ndugu waliopoteza maisha, alikuwako pia mmoja wa watu hatari duniani wakati huo. Jina lake hasa la kuzaliwa ni Ali Al Amin 'Ali al-Rashid, Lakini katika shughuli zake alijulikana kama Abu 'Ubayda al-Banshiri. Jina hilo alijipa akiwa nchini Pakistan miaka ya 1980 hadi 1989 akiwa katika mapambano dhidi ya vikosi vya umoja wa nchi za muungano wa ki-isovieti, akishirikiana na Ahmed Shah Massoud aliyekuja kuwa kiongozi wa Takriban wakati mauti yakimfika Al- Rashidi.

Haifahamiki hasa alizaliwa tarehe gani, lakini ni mwezi wa tano mwaka 1950 huko mjini Cairo nchini Misri. Al Rashidi, pengine alijua siku moja atakufa kwa bomu au kwa risasi, au kwa mateso ya CIA huko Guantanamo Bay, lakini alikufa kwa maji wakati akiwa mtu mwenye nguvu katika Al Qaeda, nafasi ya pili tu baada ya Osama Bin Laden wakati huo.

Al Rashid alianza kuwa mtumishi katika jeshi la polisi la Misri. Lakini serikali ya Misri iliwafukuza askari wengi waliokuwa waislamu wenye misimamo mikali, Al Rashid akiwa mmoja wao.

Historia yake inaanzia mwaka 1981 wakati wa mauaji ya Rais Anwar Al Saddat wa Misri. Moja ya wahusika wa mauaji hayo ni Abd-Hamid ‘Abd al-Salam, aliyekuja kuwa shemeji wa al-Rashidi, baada ya wote kuoa ndugu wa familia moja, huko Kenya. Ni mwaka 1983 ambapo Al Rashid alifunga ndoa na Hafsah Sa'd Rwashan.

Al Rashid na mkewe walihamia Jedda Saudi Arabia katika nyumba iliyomilikiwa na Osama Bin Laden, na baadye walihamia Medina katika nyumba ya Mohammed Matawi. Hapo waliishi kwa siku kumi tu, na kisha kutimkia Pakistan. Mke wa Al Rashid, Hafsah alikuja kueleza kuwa safari hizo ziligharamiwa na mtu asiyemjua. Katika mji wa Peshawar huko Pakistan, Al Rashid alijiunga katika kambi la mafunzo la Sada, akijitambulisha kama Abu Ubayda. Ndipo alipokutana na Ayman Al Zawahiri, aliyemtambulisha kwa Osama Bin Laden.

Osama alimkubali sana Al Rashidi. Walikuwa marafiki na walianzisha makundi mengi ya jihadi huko Pakistan. Mafanikio yao makubwa yaliyowapa umaarufu ni katika kile kilichoitwa "Battle of Jaji".

Katika mapambano hayo makali ya mjini Jaji, kikosi cha akina Osama na Al Rashid kiliwashinda kikosi maridadi cha jeshi la sovieti kilichoundwa na makomandoo wa Spetsnaz, wenye ujuzi mkubwa sawa na Navy Seal ya US, au Sayeret Matkal ya Israel.
Lakini baada ya mapambano hayo, baadhi ya vikosi vya jihad vilishindwa kutoa ushirikiano kwa Osama na wenzake.

Mkutano wa siku nne wa Tarehe 17-20 Agosti 1988, Al-Rashidi akiwa na Osama bin Laden, Wael Julaidan na
Mamdouh Mahmud Salim walijadili na kuanzisha Al Qaeda. Ingawa jina hilo lilikuwapo awali, lakini kundi rasmi lilianzishwa katika mkutano huo.

Kwa maneno yake Osama bin Laden, mnamo October 21, 2001, anakumbusha, kwamba "jina la Al Qaeda ni la zamani sana. Lakini kaka Al Rashid alianzisha mafunzo ya vijana wa kupambana dhidi ya manyanyaso ya wasovieti, ndipo jina Al Qaeda, "The base" lilipokolea"

Kundi la Al Qaeda lilijikita zaidi nchini Afghanistan na kuanzisha Makambi mengi ya mafunzo. Mwaka 1990, Al Qaeda walifikiria kutanua mapambano nje ya Afghanistan, wazo lilopelekea kuanzisha shughuli zake nchini Sudan. Lakini kwanza ilibidi wapitie Yemen, na mwaka 1992 walifika Sudan. Al Rashid aliratibu shughuli za Al Qaeda huko Yemen na katika Pembe ya Afrika, Sudan, Somalia, Kenya, Tanzania na Uganda.

Mwaka 1993, mkutano wa Al Rashid na Osama bin Laden uliamua kuanza kushambulia vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyopo nchini Somalia na kwingineko Afrika. Baadae wazo hilo lilikua na kujumuisha balozi za Marekani.

Ili kuficha shughuli zao, Al Rashid na wenzake Muhammed Atef, andMohammed Sadiq Odeh walianzisha biashara ya uvuvi mjini Mombassa, Kenya mwaka 1994.

Pia, Al Rahid na Wadih Al Hage walianzisha makampuni ya kuuza Vito vya thamani, Dhahabu na Tanzanite kutoka Mererani, Arusha, kwa ajili ya kupata fedha za kuendesha shuguli zao.

Taarifa za shirika la kijasusi la ndani la Marekani, FBI, zinadai kwamba Al Rashid alimiliki ardhi mjini Mwanza, alikuwa na kampuni iliyoitwa Taheer Ltd aliyoianzisha mwaka 1993, ambayo kwa mujibu wa "global witness ", kampuni hiyo ilijihusisha na biashara ya Magendo ya Alimasi, kutoka Mwadui na/au Congo, pamoja na shughuli za kutakatisha fedha.

Rafiki yake Al Rashid, Wahid Al Hage alimiliki kampuni ya Tanzanite King, iliyojihusisha na biashara ya madini ya Tanzanite pamoja na Almasi zilizopatikana kimagendo kutoka kampuni ya Taheer Ltd.

Ili kuficha zaidi shuguli zao za kigaidi, Al Rashid na Al Hage walianzisha mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya kusaidia watu masikini katika pembe ya Afrika, mfano, "Mercy International Relief Agency" na
"Help Africa People".

Haitegemewi mtu wa aina ya Al Rashid asheherekee siku ya kuzaliwa, labda pengine ilikuwa ndio siku yake ya kufa. Mei 21, 1996 alimaliza kazi wakati akiandaa kazi ya kulipua ofisi za ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya. Hakuishi kuona ndoto hiyo ikitimia. Lakini alikwishandaa mtandao.

Vyanzo vingine vinadai, Al Rashid alisafiri ndani ya MV Bukoba kuelekea Mwanza akiwa katika kutafuta mali ghafi za kutengeneza bomu-chafu, hakufika.

Baada ya kifo Chake, Kundi la Al Qaeda liliwatuma Fazul Mohammed Abdullah na Wadih Al Hage ili kuhakikisha kuwa kweli Al Rashid amekufa na kwamba kifo hiko kilitokana na ajali na sio mauaji ya kupangwa.

Credits;
Abu Ubaidah al-Banshiri, GlobalSecurity.org
Al-Qaeda gains first members, GlobalSecurity.org
Status of Embassy Bombings Investigation, FBI Executive Summary. Nov. 18, 1998.
Lake Victoria tragedy, Tanzania in May 21". Arai's Zanzibar, Tanzania Page. Arai Shin-Ichi.View attachment 782547 View attachment 782548
R.I.P
 
Back
Top Bottom