Mei 30, 2024 Asimwe anadaiwa alichukuliwa na watu wasiojulikana nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera na juhudi za kumtafuta hazikuxzaa matunda hadi hapo Juni 17, 2024 mwili wake ulipopatikana ukiwa katika mfuko wa sandarusi huku baadhi ya viungo vikiwa vimenyofolewa.
Waziri Masauni amesema watuhumiwa hao wamekamatwawakiwa na vithibiti vya kutendea kosa hilo na kufafanua kuwa hawajabahatisha katika kuwakamaa watu hao.
“Hakuna hata mmoja ambaye amehusika na mauaji ya binti huyu malaika wa Mungu atakayrepona, tumefikia pazuri na kitakachofanyika itakuwa fundisho kwa wahalifu wengine, tupo vizuri katika kukabiliana na uhalifu na ndiyo maana hakuna mtu atakayefanya uhfifu asipatikane,” amesema Masauni
Credit: Bongo 5
___
Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime imewataja watuhumiwa waliokamatwa ambao walieleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hilo ni pamoja Baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni mganga wa jadi mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Maidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu.
Paroko huyo pia anatuhumiwa kuwa ndiye allyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.
Watuhumiwa wengine ni Dastan Kaiza mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada mkazi wa Kamachumu.
Pia soma:
- Update: Mwili wa Mtoto Albino (Asimwe) wakutwa hauna baadhi ya viungo
- Kagera: Kisa cha Mtoto mwenye Ualbino kudaiwa kuibiwa, RPC Makungu asema tayari wameanza uchunguzi
- Kufuta mauaji ya albino, ni kutokomeza kabisa Waganga wapiga ramli
- Kagera: Watuhumiwa tisa wa mauaji ya Asimwe Novart wafikishwa mahakamani na kusomewa shtaka la kuua kwa kukusudia