Kifo cha biashara ya Night Club

Kifo cha biashara ya Night Club

Kiongozi umeongea ukweli kabisa DJs wa leo ubunifu zero, yani unaenda club DJ anapiga nyimbo za kusikiliza radioni siyo club
tena sehemu zingine Dj mkongwe akiwa hayupo, hawa wadogo wanaplay recorded tu ilimradi siku iishe
 
Aaah....!entrance fee ushatoa lock kwa gin kadhaa...,!!Sasa kwann uende huko kupakazana majasho tu
 
Ndo Mana kila nikitimba Moshi pale pub Alberto 24 hours night club panasuasua kwa wengi wa watu ila niliambiwa Red stone ndo habari ya Moshi ....labda next time nikienda Moshi nitatimba.


Maisha club hamna kitu pale panaboa kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dodoma kuna Lounge moja ipo barabarani imefuatana na Logde nyingi nyingi sijui inaitwa iko poa sana mwaka juzi nilitimbaga nikaenjoy watoto wazuri wapo wa kutosha, ila maisha club tangu waitoage kule Oysterbay sijawahi enda club tena..
 
hiyo ni shida kubwa, unaend athe life club unatoa 1000, na gharama ya vinywaji, wakati Tips unatoa 10000 unakunywa na unacheza nakuenjoy

Hapo tips hiyo kumi unakunywa bia ngapi mzee...

Pale ukitaka ku enjoy unaenda na laki 3 yako mfukoni sio elfu 10
 
Night club(madisko ya usiku ya ndani) ilikuwa biashara nzuri na iliyovuma kwa muda mrefu miaka ya 90's hata miaka ya 2000, hata huko vijijini au wilayani kumbi za nyasi, mabwalo au kumbi za harusi ziligeuzwa sehemu za kupiga mziki siku za sikukuu au weekend

Kwa sasa muamko wa biashara hii umezolota sana tena sana mpaka wawekezaji waliokuwa wanafanya biashara hiyo wengine wameamua kufunga.

Mfano, Billcanas ilikuwa club kubwa kwa Tanzania nasema mm na ilikuwa kama mfano kwa club zingine kukopi maudhui ya club ile ila tangu ivunjwe nawengine kama wamesizi,

Club Continental, Masai, San Siro, na zingine nyingi zimekufa, Maisha club imeishiwa mvuto, ikachange ikawa maisha basement, the life club ila kama nikutapa tapa tu

Kule Mwanza club ambazo zinaonesha uhai kwa mbali ni Villa park(The village club), Club rockbottom(gold crest hotel), ila wengine wanafunga nakubadili majina, kama club 555, Club Galaxy zamani Fusion zamani saaana The stone, kule Isamilo kulikuwa na Club Lips ikafungwa wakaja Maisha Basement nao wakafunga, Rock N roll nayo kifo cha mende

TRabora kule kulikuwa na VOT Club, Bubbles night club, Four ways.. kwa sasa wanajoint mpya inaitwa Oxygen ni Bar ndio sehemu ya mziki na mtoko

Kifupi kwa sasa watu wanapenda open space kama beach yenye msosi na mziki mzuri, Bar yenye live band, Lounge ambayo ina djs, ila sio night club kwa sasa biashara hiyo ni ngumu

Vipi maeneo ulipo ni Club zipi zimefungwa kabisa..?
ni kweli aisee club imekuwa kama ushamba hiv ila lounge mzee baba ni hatare...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Focus Electronic, Luyobya, One Way, ...! Miaka 90 nikiwa kwa muda maeneo ya huko. Nasikia siku hizi maeneo ya huko kila kijiji kina DJs...! vurugu tupu.
 
Huko Mwz the Stone,rock n roll zimekufa kitambo sana hata kabla ya 2012 zilikua hoi tayari.

Club lips yenyewe ilikua inasua sua sana bfr 2014 ulikua ukiingia pale hakuna wateja.

Last time niko Mwz nimeingia hapo fusion ilikua inabamba ila nilikua sijui kama imeshakufa siku hizi.

Ila Villa wamejitahidi sana kuendelea kushikilia usukani kwny mambo ya Burudani kwa hapo Mwz,hongera nyingi kwa yule Mangi mmiliki wa Villa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom