Kifo cha biashara ya Night Club

Kifo cha biashara ya Night Club

Night club(madisko ya usiku ya ndani) ilikuwa biashara nzuri na iliyovuma kwa muda mrefu miaka ya 90's hata miaka ya 2000, hata huko vijijini au wilayani kumbi za nyasi, mabwalo au kumbi za harusi ziligeuzwa sehemu za kupiga mziki siku za sikukuu au weekend

Kwa sasa muamko wa biashara hii umezolota sana tena sana mpaka wawekezaji waliokuwa wanafanya biashara hiyo wengine wameamua kufunga.

Mfano, Billcanas ilikuwa club kubwa kwa Tanzania nasema mm na ilikuwa kama mfano kwa club zingine kukopi maudhui ya club ile ila tangu ivunjwe nawengine kama wamesizi,

Club Continental, Masai, San Siro, na zingine nyingi zimekufa, Maisha club imeishiwa mvuto, ikachange ikawa maisha basement, the life club ila kama nikutapa tapa tu

Kule Mwanza club ambazo zinaonesha uhai kwa mbali ni Villa park(The village club), Club rockbottom(gold crest hotel), ila wengine wanafunga nakubadili majina, kama club 555, Club Galaxy zamani Fusion zamani saaana The stone, kule Isamilo kulikuwa na Club Lips ikafungwa wakaja Maisha Basement nao wakafunga, Rock N roll nayo kifo cha mende

TRabora kule kulikuwa na VOT Club, Bubbles night club, Four ways.. kwa sasa wanajoint mpya inaitwa Oxygen ni Bar ndio sehemu ya mziki na mtoko

Kifupi kwa sasa watu wanapenda open space kama beach yenye msosi na mziki mzuri, Bar yenye live band, Lounge ambayo ina djs, ila sio night club kwa sasa biashara hiyo ni ngumu

Vipi maeneo ulipo ni Club zipi zimefungwa kabisa..?
NAKUMBUKA PALE TANGA NAKO KUNA CLUB LACASSA CHIKA NAYO SIJUI INAENDELEAJE WAKUU
 
NEW CLUB GALAPO ilala naona ndio inayo bamba kwa sasa town ni nyomi la kufa mtu
 
Tatizo ni ubunifu wa DJs wetu wengi hakuna. Watu wanaenda huko kwaajili ya burudani na mburudishaji mkuu ni DJ, sasa hao waburudishaji wenyewe hawana jipya zaidi ya kupiga hit songs tena hawapigi nyimbo zenyewe kwa ubunifu unategemea nini? Upigaji muziki siku hizi kila mtu ni DJ, upigaji umerahisishwa sana na teknolojia na kuondoa ubunifu hasa kwa DJs wavivu.

Ndio maana hizo club zenye watu wengi zinajaa wanafunzi hasa wa vyuo lakini wafanyakazi wenye vipato vyao huwezi kuwapata kirahisi bila kuwa mbunifu.

Siku hizi watu wa burudani wanaenda kwenye madisko ya old skool ambayo vijana wa kileo hawayawezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukweli mtupu 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
imebaki Coppa Cabana tu hapo nyuma ya Nangwanda

Hiyo itakuwa Ntwara hiyo baada ya oil & gas kufa ntwara imefubaa maana angalau hata malaya wasafi walikuwa wanasafiri kuja ntwara kuwafuata wazee wa oil and gas, maneno yote sasa yako Pemba na Beira. Hapo CopaCabana wamejaa malaya wachafu tu.
 
Huko Mwz the Stone,rock n roll zimekufa kitambo sana hata kabla ya 2012 zilikua hoi tayari.

Club lips yenyewe ilikua inasua sua sana bfr 2014 ulikua ukiingia pale hakuna wateja.

Last time niko Mwz nimeingia hapo fusion ilikua inabamba ila nilikua sijui kama imeshakufa siku hizi.

Ila Villa wamejitahidi sana kuendelea kushikilia usukani kwny mambo ya Burudani kwa hapo Mwz,hongera nyingi kwa yule Mangi mmiliki wa Villa

Sent from my iPhone using JamiiForums

The stone mpaka 2014-2015 bado ilikuwa inafanya vizuri.. Vila kiukweli anajitahidi kushikilia usukani kwa Mwanza.
 
City pub, Maisha club na City lounge kwa wale wa Mbeya vipi bado zinafanya vizuri maana nakumbuka enzi za 2014 kurudi chini..
 
Bar ni kula na kunywa huku ukisikiliza ngoma mbalimbali taratibu
 
Life style imebadilika Na Maisha kwa jumla yamebadilisha
Zipo sababu kadhaa lakin Moja wapo
1) Kukua kwa Technolojia maana Siku hizi huhitaji kwenda night club kusikiliza Au kupata burudani ya Muzic
2) Mitandao ya Kijamii; enzi zetu Club mbali ya Kuwa sehemu ya kustarehe Na kujiliwaza Na marafiki Siku hizi huhitaji kwenda Club kukutana Na marafiki Muda wote unao Kwenye ma Group ya Wasap Na kuchart daily so Hata 'kumisiana' kumepungua
 
The stone mpaka 2014-2015 bado ilikuwa inafanya vizuri.. Vila kiukweli anajitahidi kushikilia usukani kwa Mwanza.

2014 nilikua pale the stone nimeenda kama mara 2 najikuta tuko sio zaidi ya 10 na hapo ni saa 9 usiku kuelekea.,baada ya fusion kubamba tu the stone ikajifia.

Mwz ina shida moja ikiibuka club mpya tu ya zamani inajifia chap mpk kuna muda hua nawaza labda wala bata ni wachache,club kama lips ndani ina bonge la eneo fresh tu lkn sababu ya kufa hata haieleweki.

Jamaa wa Villa kuna kipindi aliona ataenda na maji ikabidi club ifungwe iwe under construction then kufunguliwa tu ikaanza kubamba tena,jamaa anajua kwenda na soko.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Life style imebadilika Na Maisha kwa jumla yamebadilisha
Zipo sababu kadhaa lakin Moja wapo
1) Kukua kwa Technolojia maana Siku hizi huhitaji kwenda night club kusikiliza Au kupata burudani ya Muzic
2) Mitandao ya Kijamii; enzi zetu Club mbali ya Kuwa sehemu ya kustarehe Na kujiliwaza Na marafiki Siku hizi huhitaji kwenda Club kukutana Na marafiki Muda wote unao Kwenye ma Group ya Wasap Na kuchart daily so Hata 'kumisiana' kumepungua

Hamna kitu poa kama kupiga story na washkaji huku mnakula tungi+good music,mambo ya kuchart kwny magroup ya whatsap na kumisiana washkaji huo ni UMAMA.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
siku hizi bar tu zina burudani nzuri kuliko night clubs.. na bar hakuna kiingilio..

mfano dar ukienda tips ambayo ni bar unaenjoy kuliko ukienda life club ambayo ni night club... na hapo tips ni bure huku life club kuna kiingilio...

watu wengi wanaamua kwenda hizo bar za kisasa kuburudika usiku kucha
Tips iko wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2014 nilikua pale the stone nimeenda kama mara 2 najikuta tuko sio zaidi ya 10 na hapo ni saa 9 usiku kuelekea.,baada ya fusion kubamba tu the stone ikajifia.

Mwz ina shida moja ikiibuka club mpya tu ya zamani inajifia chap mpk kuna muda hua nawaza labda wala bata ni wachache,club kama lips ndani ina bonge la eneo fresh tu lkn sababu ya kufa hata haieleweki.

Jamaa wa Villa kuna kipindi aliona ataenda na maji ikabidi club ifungwe iwe under construction then kufunguliwa tu ikaanza kubamba tena,jamaa anajua kwenda na soko.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Hii tabia ya club mpya kuibuka nakuua club kongwe iko morogoro...

Hapo mwanzo ilikuwepo 4 star ikafa.. Ikaja maisha club nayo chali baada ya vibes kuja nayo vibes ikafa baada ya nyumbani lounge a.k.a samakisamaki hii ime maintain hadi leo...

Ikaibuka downtown club nayo ni kama imejifia baada ya mo town iliyokuwa 4 star ya zamani kurudi...

Kwa morogoro mo town na samakisamaki ndio kuna bamba though napependa sana mo town maana kuna Kyuma kibao za wanafunzi wa sua na mzumbe na mara mojamoja naibuka flomi hotel..
 
Back
Top Bottom