Kifo cha biashara ya Night Club

Mkuu unapAjua elements wewe??
Ukiona club inakufa ujue kuna club nyingine inabamba


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Jitu linatoa mfano wa BILLICANAS na kudai biashara ya night club hailipi. Hiv huko Kisiju mnafundishana ujinga?
 
Biashara ya Night club kupotea ni vigumu tatizo ni collation zilipo na ubunifu uliopo na aina ya DJ aliopo hii ndio hufanya club idumu au ipotee


Umeongelea Bills kabla ya kuvunjwa location yake nilikuwa pazuri panafikia DJ wazuri ubunifu mzuri mabadiliko ya Mara kwa Mara yakiafanya bills ibambe

Njoo mwanza Club rockbott, na the Galax zipo kati kati ya jiji panafikika ila ukiangalia hizi club huwa kama zinamtoano kuna kipindi rockbotto inakuwa na wateja wengi kuna kipindi wanapungua wanaenda Galax nini hapo DJ ndio hufanya hutoano
tena sehemu zingine Dj mkongwe akiwa hayupo, hawa wadogo wanaplay recorded tu ilimradi siku iishe
Jambo lingine ubunifu siku hizi wenye hizi biashara faida anaiweka kwenye vinywaji kwaiyo Yale mambo ya kingilio mlangoni elfu kumi ukifika na ndani ununue vinywaji wabobezi wa starehe wanaojua viwanja huwapati, watakimbilia lounge kwenye mziki mzuri madhari mazuri hakuna kingilio bia zako tu, tunaona mjini leo pub zinavyojaza ila mziki wa pub tofauti na night club huo ndio ukweli hata DJ awe mzuri vipi kwenye pub huwezi cheza ukafurahi kama upo night club kwani Mara nyingi hizi lounge au bup huwa zina sehemu finyu, na wengi huenda kwa target ya kunywa tu si kucheza mziki suala la kucheza huja baada ya vyombo kukolea na mziki kunoga

Hivyo wamiliki wa hizi night club wabadilike kidogo waache masuala ya kingilio, watarget kwenye vinywaji yani mtu atoe elfu kumi apewe kuponi ya bia tatu, hii inasaidia sana kushawishi watu kuingia mziki, hii kitu arusha ipo sijui kama arusha siku hizi kuna vingilio vya disco ni pesa unapewa kuponi ukingia unapeleka counter maisha yanaendelea

Jambo lingine lililozorotesha hii biashara ni baada ya disco toto kupigwa marufuku, unajua haya masuala ya burudani ni kama muendelezo furani zamani tuliokuwa tukienda disco toto kila juma pili bills ndio hao tulioanza kwenda disco la wakubwa that time sisi wadogo tukienda disco toto tulijifunza kucheza mziki uko tulishindana tuliigana so kipindi hicho mtu unawaza mziki tu siyo pombe, sasa leo hii na ndio maana hata club hazina vibe sababu wanaoenda wengi asilimia 80 ndio wanaanza kwenda mtu mtu mzima hata kucheza mziki ajui yeye anataka totoz na pombe sababu hana back ground ya mziki hii nayo sababu

Vyuoni uko mtu kafika first year ajui vibe la disco maana kakua mziki aliocheza ni kipaimala, graduation za shule, disco toto halijui ajacheza utotoni uyu unafikilia ukimwambia twende club atakuelewa akikuelewa ataenda ila ataishia kukaa kwenye sofa sasa club watu wakikaa kaka sana vibe halipo

My take
Disco toto lirudi siku za juma pili ila siku za sikuku lizuiliwe maana source ya kuzuia disco toto ni vifo vya wale watoto tabora uko siku ya sikuku ya iddy.
 
City pub, Maisha club na City lounge kwa wale wa Mbeya vipi bado zinafanya vizuri maana nakumbuka enzi za 2014 kurudi chini..
Mdau umenikumbusha maisha club mbeya tulikiwaga na project sumbawanga yani ikifika week end lazima tuwashe gari tuje mbeya kukamata totoz za mzumbe pale hatari maisha club alikuwa inashiba balaa hiyo ni mwaka 2013 mwanzoni, pia kukawa na green lounge sijui bado vipo ebu wana mbeya tuambieni bwana mbeya uko wapi sasa panashika mji
 
That's true brother,, nowadays kuna song selectors tu wanachofanya ni kupiga nyimbo zinazo hit tu bila kujali kama beat na rhythm zinaendana,, hakuna mpangilio,, ujue kuna DJ's wachache sana anaweza kupangilia nyimbo zingine hata hauzijui lakini ukaingia dancefloor bila kupenda,,
 
Jitu linatoa mfano wa BILLICANAS na kudai biashara ya night club hailipi. Hiv huko Kisiju mnafundishana ujinga?
hizi ni biashara za msimu ndugu lijue hilo, hata hapo Tips, Element, Next Door ni suala la muda tu, itabaki historia... na anguko kubwa la hizo biashara huwa ni menejimenti
 
Mkuu unapAjua elements wewe??
Ukiona club inakufa ujue kuna club nyingine inabamba


Sent from my iPhone using JamiiForums
hiyo Elements pia itapita hizi biashara hamzifahamu kiundani, atatokea zaidi ya Elements na Elements itasahaulika
 
safi sana chief
 
Hakuna muziki wa kuchezeka club
 
Dodoma kuna Lounge moja ipo barabarani imefuatana na Logde nyingi nyingi sijui inaitwa iko poa sana mwaka juzi nilitimbaga nikaenjoy watoto wazuri wapo wa kutosha, ila maisha club tangu waitoage kule Oysterbay sijawahi enda club tena..
Platinumz park?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…