Kifo cha Dkt. Magufuli tunajifunza nini?

Hamna lolote, uongo tu. Tunachoona mikoani ni watu kulia kumpoteza kipenzi chao. Tuletee ushahidi wa hayo unayoyasema!
Acha kubisha bisha jambo usilolijua...


Kama kitu hujui haimaanishi kwamba hakipo...

Watu 8 wamekamatwa huko manyara kwa kusheherekea magu kufa.
 
Mapenzi ya Mungu ni tofauti na mtizamo wa binadamu anavoyatafsiri....
 
Kwa kifo chake nimejifunza umuhimu wa kutunza bia na k vant maana hujui siku ya kusherehekea kama utakuwa na akiba ya hela
 
viongozi mliobaki jufunzeni kusema ukweli hata kama ni mchungu, msiwe wanafiki.
JPM ametufundisha kusema ukweli hata kama hauwafurahishi baadhi ya watu.

Jasiri asiye yumba wala hakubali kuyumbishwa.

kiongozi ambaye hakufikiria tumbo lake bali watanzania wote.

kiongozi ambaye alisimamia sheria bila uoga wala aibu.

Kiongozi aliye fikiria masilahi ya watanzania kwanza kabla ya wengine. alitetea madini yetu na kubadilisha sheria kandamizi ili kulinda na kunufaika na madini yetu.

Kiongozi aliye chukuia kudanganywa na hivyo alitumia kila mbinu kuujua ukweli wa jambo kwa ufasaha na uhakika. mfano makinikia yaliyo kamatwa bandarini n.k

kiongozi ambaye hakubali kupokea majungu na fitina bila kwanza kujiridhisha.alibaini viongozi wengi waliachishwa kazi au kusimamishwa kazi kwa hila na kisha kuwarudisha.

aliwapenda sana watanzania wabunifu na wachapa kazi. aliamini kuwa kufanya kazi kwa bidiii ndio msingi wa maendeleo.

aliye dhamiria kujitegemea zaidi kuliko kuwa tegemezi.

aliye toa elimu buree kwa watanzania wote kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

aliye boresha na kujenga vituo vya afya vingi zaidi karibu kila wilaya.

aliye iunganisha mikoa yote na wilaya zote za tanzania kwa Lami.

aliye fanikiwa kusambaza umeme hadi vijijini.

iliye boresha huduma ya maji safi.
 
Wafu huzika wafu
 
Dah hakika tunamengi ya kujifunza, ila yote kwa yote nilikua napenda sana speech za mzee, haijawahi kutokea niangalie speech zake nisicheke ila ndo hivyo tena. Pumzika kwa amani mzee wetu. RIP MAGUFULI ..
 
Wema hawadumu na wema siku zote wana maadui wengi na maadui wana wafwasi wao hiki ndo nimejifunza.
Wema ?? Sababu ya hotuba kanisani kila siku ?
Ufisadi kwani uliisha au ulikuwa centralized tu ?

Tribalism ?

Urongo... sungura wana covid
 
Wema ?? Sababu ya hotuba kanisani kila siku ?
Ufisadi kwani uliisha au ulikuwa centralized tu ?

Tribalism ?

Urongo... sungura wana covid
Wakati mwingine hata vichaa wanajua kibaya na kizuri nashangaa ww sijui upo kundi gani
 
Nimejifunza kuwa upigaji umeanza kwa kasi ya spidi ya mwanga, tunaanzia hapa kwenye msiba, then tutaendelea. Ila SSH ana kazi.

Ninachotaka ni niendelee kupata maji ya uhakika na umeme kama nilivyokuwa napata.
 
Kinatufundisha tuache ubaguzi na tuishi kwa kuwapenda wenzetu hasa wale tunaopishana nao mawazo.
 
Nchi yetu ilichezewa sana kwa muda mrefu, tuliibiwa sana, tulipigwa sana kwenye mikataba mibovu, tulipigwa sana kwenye 10%

tulipigwa sana kwenye miradi mbalimbali,
thamani ya fedha zetu hatukuziona kwa kipindi kirefu.
Kupitia Magufuli alitufafanulia kila kitu na jinsi tulivyo kuwa tunaibiwa na njia/mbinu alizo tumia kubana myanya.

Magufuli alitufanya watanzania wengi tuelewe nchi yetu ilivyo kuwa inaibiwa na wajanja wachache wakishirikiana na baadhi ya viongozi wasio waadilifu.

Pumzika kwa Amani JPM, tunakuombea Mungu aipokee roho yako na aipumzishe mahala pema.
 
lakini pia ni vyema watanzania wenzangu tukumbuke kuwa Hayati Rais Magufuli alikuwa binaadamu tu kama sisi, inawezekana kuna mahala alitukwaza bila yeye kujua.
kwa niaba ya watanzania wote Tunamsamehe kwa roho safi kabisa na Mungu aipokee roho yake.
samehe saba mara sabini.
hakuna binaadamu aliye mkamilifu isipo kuwa Mungu pekee.
sisi sote kuna wakati tunakosea kwa kujua au bila kujua.
Pumzika kwa Amani JPM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…