Kifo cha Dkt. Magufuli tunajifunza nini?

Mara kadhaa alisikika akisema;

"Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu"

hakuwa mnafiki mara zote alisema ukweli hata kama unaumiza lkn alisema hakuficha kitu,.
wananchi wlipenda sana style hii, maaana iliwafanya wananchi wazidi kumuamini na kumkubali kuwa ni Rais wao.
kwa aina yake hiyo ya uongozi wananchi walifahamu kila kitu kilicho kuwa kina fanywa na serikli yao.
 
Naona umeamua kabisa kumuongelea Kipopoo zaidi! No chop chop hata kwa Mama Samia!![emoji38][emoji3]
 
Umati wa watu kwenda kumuaga mwendazake magufuli pia ni ujumbe mzito kwa viongozi wakuu ndani ya serikali,, hakika wanatakiwa kuwa wazalendo kwa nchi yao, pia wawe waadilifu na kutimiza matakwa ya watu maana hata magufuli nae aliamua kuchagua upande wa wananchi kulko viongozi wenzake ndani ya ofisi, tutumikie watu jaman kwa manufaa ya nchi yetu,,,
 
Baada ya kushindikana kwa miaka mingi tangu nchi yetu ipate uhuru,

Magufuli aliweza kuhamisha makao Makuu kutoka DSM kwenda Dodoma.
 
Tangu tarehe 17 mwezi march Tanzania imekumbwa na simanzi isiyo na kifani mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha rais Magufuli.
Mamilioni ya watanzania wameangua kilio kila kona kwamba sasa mwokozi wao ameondoka, cha kushitusha ni kwamba wananchi wa hali ya chini kabisa ndiyo wanaoongoza kwa kilio kinyume na tulivyokuwa tumeaminishwa kwamba Magufuli alikuwa ananyonga wanyonge!
Kitendo cha hayati rais Magufuli kuagwa na mamilioni ya watanzania huku wakiangua vilio njia nzima na kutandika kanga zao chini ili mwili upite imeenda kinyume kabisa na wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu na genge lake.

Kwa jinsi msiba huu unavyoenda naamini utakuwa darasa tosha kwa wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu ,Godbless Lema, Chahali, Ngurumo, Mange Kimambi na wengine wengi, sasa wataelewa kumbe watanzania siyo vilaza.
Wataelewa kumbe watanzania wanajua yupi anapigania haki zao kwa vitendo na ni yupi ni mpiga makelele nyuma ya keyboard.

Kwa mapenzi haya yanayoonyeshwa na Watanzania kwenye msiba huu ni lofa tu atakayeendelea kuamini kwamba eti Tundu Lisu aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Wito wangu kwa wasaliti wa nchi hii wanaoshangilia msiba kwamba sasa Magufuli ameondoka watarudi Tanzania na kuanza tena kutumika kuiba rasilimali za nchi hii kama walivyokuwa wanafanya huko nyuma wajue tu kwamba wanapoteza muda.
Watanzania siyo vilaza ,wanajua fika Tundu Lisu aliwatisha kwamba watashitakiwa MIGA ikiwa watabadili sheria za madini.
Tundu Lisu aelewe kuwa hawezi kuwa rais wa Tanzania kwa kushinda Twitter akikejeli kila lililojema kuhusu nchi yetu,
Tundu Lisu kupitia msiba huu atakuwa ameelewa na kupata darasa kwamba ukitaka kupendwa na Watanzania tumikia watanzania na siyo kutumikia Acacia.
 
Nimejifunza kwamba hakuna watu wanafiki hapa duniani kama Watanzania.

Nimejifunza kwamba kama usipojali maumivu ya wengine na wewe kuna siku watu hawatojali maumivu yako.

Nimejifunza kwamba masikini wanaogopa matajiri watapumua na kuendelea zaidi kiuchumi kuliko wao, hili ndyo linawaliza zaidi.

Nimejifunza kwamba kifo huwezi kukizuia hata kama unapesa na nguvu kiasi gani.


Nimejifunza kwamba kumbe inawezekana kumlazimisha mtu kuwa na furaha au kuwa na huzuni.
 
Mataifa mengine walimtamani sana Rais Magufuli angalau angekuwa Rais wa nchi zao japo kwa muda tu.

Magufuli alionyesha namna na jinsi Rais anavyo takiwa kuwa.

he was simple president, committed to his citizen,

Hakuacha kusema wazi kwa wananchi juu ya ugumu na uozo alio kuwa anakabiliana nao ktk utendaji wake wa Urais,
tunategemea pia Rais wetu Samia atafuata style hiyo ili wananchi wamwelewe.
 
Tunapo Muanga Kipenzi chetu JPM, tunapo toa heshima zetu za mwisho tukumbuke kuwa na sisi haswa viongozi na wewe pia kuna siku utalala kimya.

ni muhimu tukumbuke na tujifunze kutenda haki na tuache fitina na majungu kwani vitu hivyo havifai ktk maisha ya binaadamu.

kama unamuaga halafu huna cha kujifunza basi tambua kuwa wewe sio binaadamu wa kawaida. Jitafakari.
 
korona haina mkubwa,mdogo,dikteta, mnyonge, tajiri wala maskini......wote wake na kwa style yake....
 
Nimejifunza kuwa duniani hapa tunapita. Hakuna sababu ya kujimwambafai na kujiweka kama mungu-mtu.


YESU NI BWANA
 
Tuishi kwa kumtegemea MUNGU maana hatujui siku wala saa ya kuondoka
 
Nimejifunza zaidi kumtegemea na kumtanguliza Mungu katika kila jambo.

Pia kuwa mwepesi kukiri uwezo wa Mungu aliyeniumba hadharani bila kificho.

Hayati JPM alilisisitiza sana kwenye speech zake kutomuacha Mungu.
 
Tumejifunza UZALENDO kwa matendo sio maneno tu.

kwa kweli kabla ya hapo nilikuwa bado sijui maaana ya uzalendo kwa vitendo.

JPM aliifanikiwa kujenga uzalendo kwa watamzania.
 
Mandela aliishi miaka tisini na tano,
Desmond Tutu yuko hai mpaka leo.
Wema hawadumu na wema siku zote wana maadui wengi na maadui wana wafwasi wao hiki ndo nimejifunza.
 
Hakika Hayati Magufuli alikuwa Kipenzi cha watanzania wengi.
mwenye macho hambiwi tazama.
mambo yanajionyesha yenyewe.

kwa maombi, sala na machozi ya watanzania hawa wanao mlilia na kumuomba basi hakika Mungu atapokea sala zao.
Huyu ni Dikteta Joseph Stalin siku anaagwa mwezi March 1953,katika utawala wake inakadiriwa watu 9ml waliuawa.
 
Leo hii watoto wetu wanaenda shule buree, wazazi hatuna presha ya kutafuta Ada.
haikuwezekana tangu nchi yetu ipate uhuru, lkn JPM aliweza.

Pumzika kwa Amani JPM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…