Kifo cha ghafla cha Mfugale sawa na Prof. Chachage: Kuna viashiria vyote vya kupewa sumu. Serikali ichunguze

Ni fumbo kwa kuwa tu kinakuja bila taarifa, ila baada ya hapo ni lazima sababu ijulikane.
Mkuu nimekwambia siyo lazima sababu ijulikane kwa asilimia mia, binadamu siyo Mungu anayejua kila jambo na yale yaliyo sirini.....
 
Miradi mikubwa kama Daraja la Busisi na Bwawa la umeme la nyerere lazima ife ili wapiga dili za vivuko na kampuni za uzalishaji umeme kama IPTL mpya zizalishwe!!!Watu kama mfugale ni mwarobaini wa kuzuia dili hizo sishangai akimfuata mwenda zake na miradi izikwe rasmi!!!NAJARIBU KU CONNECT DOTS TU WAKUU!!!
 
Umesikiliza maelezo ya waziri wake? Najua ugonjwa wake uliokuwa unamsumbua muda.
Ila kilichotokea muda mfupi kabla ya yeye kufariki kitaalam hakina uhusiano wowote na kupanda au kushuka kwa lile tatizo lake.
Ulitaka wakwambie Corona imemuuwa au?.
 
Sikuandika maoni yangu ila nimekupa taarifa zilizoandikwa na madakatari waliofanya utafiti wa kina kuhusu ugonjwa huu. Ninakubaliana nao kwa sababu hali ilivyokuwa hapa kwetu watu walikufa zaidi ya 6,000 (siyo mji mkubwa sana) lakini walikuwa hawaugui na kufa ghafla tu. Ilifikia kugeuza viwanja vya michezo ya ndani kuwa hospitali za dharura kwa vile mahospitali yalikuwa yamejaa.
 
Mkuu nimekwambia siyo lazima sababu ijulikane kwa asilimia mia, binadamu siyo Mungu anayejua kila jambo na yale yaliyo sirini.....

Ni maamuzi au matumizi ya akili tu, Mungu alitupa kila kitu.
 
Kifo kinapotokea ghafla Post moterm ni jambo la muhimu ili tatizo lililosababisha mauti kwa mhanga liweze kupatiwa ufumbuzi ili isitokee kwa mwingine. "The deads like the living but the living run away from the dead". Matokeo ya post moterm yameleta ufumbuzi kwenye mambo mengi ikiwemo magonjwa na jinsi ya kuyakabili, upangaji wa mauaji na jinsi ya kudhibiti, kuwaondoa watu katika hatia kutokana na kuhusishwa na vifo vya wengine. hii habari ya kuwa mpaka ndugu watake haijakaa sawa kabisa.
 
Huelewi kilichoandikwa basi.

Hao madaktari wamesema kwene ripoti yao kwamba hakuna dalili nyingine zozote, na kwamba walichoandika ndicho kichukuliwe kama hitimisho juu ya ugonjwa huo?

COVID-19, bado ina'evolve', hakuna anayejua dalili zote na madhara yote inayosababisha kwa watu wote wanaopata ugonjwa huo.

Kwa hiyo, wewe hapo unakazania maoni ambayo hujui yanazungumzia kitu gani, na unayakomalia kweli kweli kama unavyoonyesha hapa.
Lakini hiyo si ajabu, kwa sababu unajulikana kukomalia mambo ambayo hata hayana msingi wowote, kama ule uwanja wa ndege wa Chato.
 
Ndio. Mtu analalamika kuwa naumwa wanamwambia kapumzike ofisini badala ya kumkimbiza hospitali. Inatia shaka hata familia wanaposema hata hospitali hawajasema sababu ya kifo. This is very unprofessional kama sio yamepangwa. Waondoe haya mashaka yaliyoonyeshwa na familia ya marehemu.
 
HUYO KAFA KWA "MALIPO MARA 2" KWA WAKANDARASI. Acha akasalimiane na mwendazake! wezi wakubwa!
 
Binadamu bana, haya sasa tumechunguza kapewa sumu, DEJAVU haya atarudi kuwa hai??

Kifo hakikosi sababu! Mfugale kafariki POLE kwa familia apumzike kwa amani.
Kina Azory, Ben walipotea nao pia POLE kwa familia.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Najaribu kufikiri tu , kama marehemu alikuwa anajiuliza swali hili baada ya kifo cha hayati , Nini hatma ya kazi yangu?
Basi hicho kikao kilikuwa na muingiliano wa jibu wa hilo swali.

NB :
Ubaya wa inshu za kuondoa roho ni kuwa, wanaoratibu lazima waondolewe kwa njia hiyo....ndio maana kuna mmoja tayari kapewa siku zisizozidi 1835 za mwisho mwisho...
 
Tuacheni uzushi, Afrika vifo vyote ni vya kulishwa sumu, kuuawa na kurogwa! Hakuna kifo cha kawaida! Tuacheni ramli chonganishi, hii siyo sawa kabisa!
 
Mimi kama shabiki wa Yanga, nauliza tu Kesho tunaamka saa ngapi ndugu zangu.??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…