Kifo cha Hayati Dkt. Magufuli kimeipasua CCM. Je, huu ndio wakati wa wapinzani kutusua kisiasa?

Hakuna wa kuipasua CCM yote unayoyaona ni mkakati ambao mlio nje hamuwezi kuelewa
Huo siyo Mkakati wala nini,kuna tifu kubwa ila tu ni kuwa walioshika mpini wana uwezo wa kuwadhibiti walioshika makali hivyo watamalizana kimya kimya kwani wote ni wapigaji inapokuja kwenye kutafuta madaraka wanakuwa kitu kimoja,ambaye atashupaza shingo anakololimbwa .

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Ni ujinga wa kiwango cha lami kwenda kuungana na Mbatia. Kila chama cha upinzani kipambane kivyake, adui ni ccm. Kuungana ni kutafuta migogoro isiyo na tija na mifano ipo wazi.
Lakini kumbuka sometimes umoja ni nguvu.
 
Wapinzani mnasubiria mpasuko wa ccm ,inamaana mmeishiwa mbinu?
 
Wapinzani wapo bize kudai Katiba mpya, ambayo japo ni muhimu lakini haiakisi changamoto zinazowakabili Watanzania wengi kwa sasa, hence kuibuka kwa "mashujaa" kama Polepole wanaotumia ombwe la kutokuwepo "msemaji wa wananchi."
 
Mbona hujasema kuwa mwalimu nyerere alitabiri upinzani utatoka humohumo..au upinzani nini tuanzie hapo.
Hawaelewi maana ya kauli hii Ya mwalimu, sijui wengi wamezaliwa umri sawa na vyama vya upinzani, ama vimewazidi umri, lakini ni brainwashing za ajabu sana zinaharibu watu.
Vyama havina hata misingi inayolingana na misingi ya taifa letu ,. Vitaongozaje taifa? Ndio maana upinzani utakaotawala nchi hii utatokea humohumo Ccm kwa wazalendo wachache waliobaki.
 
Well said mkuu, hawa jamaa sijui kama zinachaji sawasawa yani wanaacha kuangalia mapungufu ilikujijengea hoja za kuwapa nguvu kwa wananchi, wao 24/7 wanapambana na marehemu tuuuu.🤣🤣🤣 .
Nacheka sana mbaka nawaza kama kuna chadema wengine wenye akilitofauti na hawahumu jf then its Ok, lakini kama ndio hawahawa tunaoshindanao humu!!!!!
maccm yata tawala milele.
 
Tatzo upinzani hawako serious,ni wabinafsi Sana na hii ndo itawafanya miaka nenda miaka rudi wasifanikiwe, wakitaka waungane , kinyume Cha hapo hawatoboi,ccm wanaweza wakawa wanaonekanawamepasuka lkn linapokuja suala la kulinda chama kisipoteze utawala,huwa wanauwezo wa kuji mobilize hata dk ya 89,na sekunde 59',sekunde moja tu ukiwapa pumz wanakubadilishia matokeo ya mchezo, unapigwa gori ndani ya sec moja !!
 
2025 ipo wazi mbona wapinzani watapata viti vingi sana bungeni.
Hayupo tena mwenye nguvu ya kuwaamrisha wakurugenzi
 
Majibu sahihi ya mjadala itakua 2025 saiv mnafanya tu kutabili na kubashili.
 
Sasa ccm inao uwezo gani wa kujilinda,ccm Katu haiwezi jisimamia bila kubebwa na police.
Police wakikaa pembeni tu ccm bye bye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…