Kifo cha kampuni ya mabasi SCANDINAVIA EXPRESS

Kampuni ya mabasi ya skandinanavia imehujumiwa kwa makusudi. Haikuwa kwa sababu ya madeni kwani makamouni yote hususan za usafirishaji zinadaiwa mpaka utosini. Makampuni mengi ambayo unayaona yana majina makuna yamepata hela kwa michoro, na yanamadeni kibao na hawatalipa na pamoja na hayo baadhi wanaoewa hata ruzuku.

Skandi alikuwa akilipa madeni yake vizuri na walioihujumu walitumia kigezo ati ilikuwa kampunu ya kiongozi mkuu fulani aliestaafu, jambo lilio la uzushi bali lilitumika ili wakidhi ubaya wao.

Skandi haikuwahi kuwa na uhusiani wa kibiashara hata ya urafiki na kioongozi wote wa kisisa nahaina uhusiano huo mpaka sasa na sidhani kama watakuwa nayo mbeleni, kwani skandi ilikuwa ikihudumia toka enzi za awamu ya kwanza ilipokuwa shida usafiri lakini walihudumia taifa nyakati hao walioipangia njama kuiuwa kukidhi kiu yao waliuwa nje ya nchi kwani hawakuwa tayari kuwa na tz kwenye matatizo. hali kadhalika Skandi wala haikuwa na wadau wengi kama msemaji mmoja humu alivosema, kwani hayo ni maneno ya mitaanii na vijiweni na wala haina uhusiano wa kisiasa.

Kilichowaponza Skandi kwa mtazamo wangu ni uzalendo wao, utaifa wao na jitihada yao ya kuleta mabadiliko jambo lililolipa tz sifa kitendo ambaco hao wasaliti hawakulipenda, kwani wao hufurahi matatizo yawrpo ili wao wafaidike.

Ingekuwa Skandi iko nchi nyimgine Serikali ingeingilia kuilinda na kuikwamua hata ingekuwa kweli imeelemewa na madeni jambo ambalo limepikwa.

Mbona kuna watu walipewa na wanaendelea kupewa fedha bure tz wakati hakuna walichofanya ? iweje skandi iliohudumia na kuwakwamuwa wa tz imefumbiwa macho ? Wa tz wenzangu tuweni macho na njama hizi za kuhujumu makampuni ya wa tz kwa kutengenezewa na kupokowa sababu za uzushi na sis tunayakubali tu. tusipokuwa makini wazalendo watapukutiwa wote ili wachache wasiojaa kiganja ndio watusaliti.

HATA ingekuwa skand ina madeni, mbona kutokana na taarifa za magazeti pamoja ni kuwa uzushi ilionesha kuwa deni lake lote halikufikia hata shiling bilioni 3 ? wakati assets zake ni nyingi na haoi hapo tunasikia kwenye magazeti hayo hayo serikali kupitia taasisisi zake imewapa baadha ya watu :target::yuck::frown:zaidi ya BILIONI 30 ambayo ni mara 10 ya hiyo na wamepewa bure ?

hatuoni hapa kuna namna za uoneaji skani ameonewa tu ?

Wa Tz tusishabikie haya mambo na tusimcheke skandi kwani kilichomponza ni uzalendo na si kingine.

mimi nimesafiri sana na skandi na naona mengi ambayo kama serikali yetu ingekuwa inayaangalia kwa makini isingeiwacha skani ikaonewa. Nadhani kwa kuwa ni njama za makusudi ni oia wakati wakihua wanaipoga vita skandi ikaharibiwa baadha ya makampuni yapewwe msaada hata wa bure wanunuwe na wakazanishe makampuni ya mabasi yao ILI SKANDI IKIANGUSHWA Wananchi wasilalame, lakini cha kustaajabisha, yametengenenezwa makampuni mapya kuanzia 2003 kama kuzitayarisha na mengine yaliyoko walipewa mikopo kiwepesi na wengine mikopo ya nafuu pamoja na wengine ruzuku tuu ili ifikiapo 2005 ikishughulikiwa skandi WALE WAJAZE PENGO, LAKINI LICHA YA HAO WALIOWATENGENEZA KUPEWA YOTE HAYO LAKINI HAWAKUWEZA HATA KUKARIBIA SKANDI, NA kwa hivo INGEKUWA SKANDI KALINDWA TU NA HAKUG=HUJUMIWA KUSUDI LEO SKANDI INGEKUWA MBALI KUENDELEA KUWEKA MFANO NA FAHARI KWA TZ, LAKINI LEO WASAFIRI WANASIKITIKA KUWA hakuna usafiri kama skandi mpaka leo na hata nchi za jirani wanatucheka wa tz.

wasafiri tunasubiri Skandi irudi tena kuhudumia, lakini kwa namna alivonyanyaswa na kuonewa sijui kama atarudi a=kuhudumia au sio, maana sisi wasafiri tunaelwewa kuwa alivinjwa moyo na hakuona sababu ya kuendelea na kuhudumia hii sekta, maana sidhani kama hata ALIPOAMUA MWENYEWE kusimamishi kuna mhusika waekta hii aliejaribu hata kuwauliza nini kilichotokea. Lakini hatuhui, ila wenyewe ndio watakaojua na nadhani wameamuwa kukaa kimya kabisa.

Hayo ndio yangu machache lakini tusizungumzie masuala ya skandi kama washabiki tu maana hii ni athari kwa watanzania.

Chunguzeni muone wangapi ambao wamesaidiwa kusema uongo kuwa wamepata hasara kwenye mtikisiko wa uchumi na kupewa fedha za bure iweje hii kampuni hata isiulizwe,

Wajameni tuweni macho nas uonevu wa aina hii na inaweza mfika mtiu yeyote.

tumesikia majuzi hapa wasafirishaji walitaka kugoma, na hiyo wangefanikiwa sababu skandi haipo, laiti skandi ingekuwapo hayo yasingetokea maana tumeshuhudia mara nyingi huko nyuma migomo kama hii ilitaka kutokea lakini kwa skandi licha ya kuonewa hakuungano nalo, migomo hiyo haikufanyika,

Hayo ni yangu machache wajameni



Mbona kuna watu wamepewa fedha BURE hapa tz wakati hakuna
 
Trillion 1.9 ilitolewa "kukwamua" mtikisiko wa uchumi Tanzania.
Imeshindikana vipi kwa Scandnavia?
 
Wanasiasa ndio wamefilisi kampuni ,utayaona mabasi kibao kuwabeba wanachama,wapenzi,mashabiki wa CCM tena buure,tetesi nasikia wanasiasa wa kipindi cha mkapa nao walikuwa na hisa kwenye kampuni.Na mwisho wafanyakazi wa hiyo kampuni ndio wameiua kabisa hasa wale mameneja(wote walikuwa waarabu na wahindi)wao ndio walikuwa wanafanya dili za kuweka mafuta hewa kwenye hayo mabasi pia mizigo walisafirisha na hela kuweka kibindoni,wengi wa waliokuwa wafanyakazi wa hiyo kampuni wametajirika
 

Ama kweli hapa JF kuna mengi. Hongera saana Bwn Simba kama ni kweli tunaiombea CO yetu SCANDNAVIA ipone irudi mahali pake. CO hii ililetea taifa letu heshima mpaka nje ya mipaka ya Tanzania. Mtu akifanya vizuri apongezwe. Kuhusu hao mafisadi wanaohujumu uchumi hata wa wafanya biashara wenzao hawalitakii mema Taifa letu la Tanzania. Uchumi wa Campany moja unaligusa taifa zima. Serikali iangalie jinsi ya kusaidia wafanyi biashara wazuri pindi wakiwa na misukosuko ya biashara.
Kufanikiwa kwa Company moja ni mafanikio ya taifa, vyanzo vya kodi vinaongezeka, upana wa wigo wa ajira unapatikana, chukua mfano wa USA (Mwana Kijiji tusaidie).Tusikae na kuchekelea Commpany zikifail ujue kuna watu watakosa ajira watu watalala njaa, watoto hawataenda shule. Serikari itafute jinsi ya kuingilia kati kusaidia sio kubeza. Na mabenki hasa TZ yaangaliwe sana,au itungwe upya sheria ya biashara ya mabenki, KUANZIA BOT, isiwe kazi ni kufilisi badala ya kuinua uchumi wa nchi.
 
Tujiulize Dar Express amewezaje kukaa kwenye game muda wote huu bila kuyumba? Ina maana hana mikopo bank? Mimi naamini management ni issue hapa.
 
Tujiulize Dar Express amewezaje kukaa kwenye game muda wote huu bila kuyumba? Ina maana hana mikopo bank? Mimi naamini management ni issue hapa.

Kampuni hii ilikuwepo kwa miaka mingi, nadhani iliibuka baada ya Kwacha na Nyota Bus kufifia na kupotea,ikapotea miaka ya mwisho ya 80s na mwaka 1992 iliibuka upya na kufanya mambo ya kisasa ktk sekta hii ya usafirishaji.

Siasa za Kibongo,za wanasiasa wetu za kutaka kuwa na hisa kwenye kila kitu kinachofanya biashara kwa mafanikio ndo kimepelekea Scand kufikia hapo na pia wivu kutoka ktk makampuni yanayoendeshwa kiujanjaujanja kama vile kuamini bila wapiga debe biashara ya bus haiendi. Kwa Scand hakukuwa na nafasi ya mpiga debe.

Ndiyo kampuni ambayo madereva na wafanyakazi wengine walikuwa wameajiriwa wakilipwa mishahara na kuchukua likizo na off pia,na hata mafao yao yalikuwa wazi. Naamini kampuni hii bado ipo na itarudi vizuri tu kuendeleza pale ilipoishia kwa vile madereva na baadhi ya wafanyakazi wengine bado wapo na wanakula salary kama kawaida.
 
Taarifa za kuaminika atarudisha tena huma zake hivi karibuni na kwa kweli hat amie nitarudi huko kwani Sumry naye ni uozo tu yeye hajamfikia scandinavia!! anaiga lkn bado Sumry mzuri ni zile za kisasa lkn yale mengine ni rangi tu ndani hamna kitu nilipanda safari moja la tunduma tulijazwa kama nyanya na vitunguu kwanza ni seat 3 kwa 2 kitu ambacho Scandi alijitahidi sana na hili na usafi !!
Ktk biashar akuna upside down za maisha so tumwache arudi tena habari nilizonazo kuwa itakuwa bbora zaidi ya zamani!!

KUHUSU VIFURISHI HUYU NI AGENT WA DHL LONG TIME HATA WAKATI MABASI HAYAJAANZA SAFARI ZAKE SO HIYO NI TENDA YAKE YA HALALI TANGU ZAMANI!
 
Watoto wa MOHA ndio wameichukua wanataka pia kujihusisha na mabasi yaendayo kasi ya jiji la dar. ambayo tumeambiwa yanakuja soon. Japo sijui how soon is soon.
Huyo MOHA ndio nani tena
 
jamaa alikuwa na madeni makubwa arafu garufu ya ufisadi pia ilimponza kwan...
 
Binafsi nilipenda sana mabasi na huduma za hii kampuni, hususan miaka ya 2003/2006. Mabasi mazuri, huduma za ndani lukuki! Ilikuwa hata watoto wadogo wanasafirisha bila shida yoyote, na coverage yao ilikuwa nzuri hadi nje ya nchi. Nadhani zilikuwa miongoni mwa marcopolo za mwanzo hapa tz, na miongoni mwa luxury za hali ya juu. Sasa miaka ya hivi karibuni ~ 2008 ndipo mizengwe ikaanza. Nikaja kusikia ni kampuni ya wakubwa wa serikali kipindi kile, mara ya wahindi mara ya fulani. Hadi sasa sijajua kwa nini kampuni ile imekufa, na nini kilikuwa nyuma ya pazia? Kama kuna mtu mwenye taarifa juu ya hili namuomba atujuze jamani
 

Nakumbuka mpaka kufikia mwaka 2009 hawa jamaa walikua wamebaki na basi moja tu litokalo Dar kwenda Arusha na by that time ofisi zao za pale Arusha zilikua zipo shagala bagala kama dampo.Kuna mdau alinitonya kwamba hii kampuni ilikua inadaiwa kodi kubwa na serikali sababu walikua na mabasi mengi sana sasa baada ya serikali kuamua kutaifisha yale mabasi ndipo wamiliki wa haya mabasi walipoamua kuyatoa mabasi yao kwenye hii kampuni na kuyaweka kwenye route zingine pamoja na kuyabadili rangi na majina.Hicho ndicho ninachokifahamu.
 
Kilicho pelekea kifo cha Scandinavia Express ni mitandao ya siasa za Urais ktk uchaguzi wa 2005. Jamaa hawakuchangia mtandao ulioshinda! Baada ya watu kuingia Magogoni wakaanza kulipa visasi! Tunaelewa biashara zetu nyingi ambavyo zinafanyika kwa mikopo,wanahisa kutumia majina bandia nk. Kwa jamaa wakaondoa mabasi na mengine wakayakimbiza Kenya wakasajili huko!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…