Kifo cha kampuni ya mabasi SCANDINAVIA EXPRESS

Kifo cha kampuni ya mabasi SCANDINAVIA EXPRESS

Nadhani Kituko ndo amesema kweli, it does not make sense huyu owner alieanzia chini kwa mtaji wake aje ashindwe kwavile kachukua mkopo. Kama issue ni kuruhusu share na wengine nadhani ndo ameharibikiwa hapo - Jamani tusikate tamaa kuwa haiwezekani isipokuwa tafuta sababu unaweza kukuta biashara fulani unayoona imekufa pengine mwenyewe kaicha na kaona nyingine nzuri na kahamishia mtaji huko inapeta.
Kikubwa ni kuangalia wanaokuijia wakuongeze mtaji wanafanya biashara gani/ imefikia wapi?
Kuna shemeji yangu alistaafu miaka 4 anaishi vizuri tu kwa biashara ya baa na guest na nyumba 5 amepangisha hakuwa na tatizo ni nyumba hasa zenye hatimiliki mjini hapa. Alitokea rafiki akamshauri aweke rehani nyumba zote kisha wapewe mtaji yeye rafiki anunue korosho kupeleka India kwa mwezi inaingiza 10m. ndio ulikuwa mwanzo wa kufilisika na mwisho kufariki kabisa kwa huyo mtu within 2 months only baada ya benki kunyang'anya vyooote.
Biashara fanya mwenyewe tamaa ya mtaji toka chama, rafiki, sijui raisi itabidi udance to their tune, which is not possible

...Mama Joe! hapo sijui niseme kuwa na ujinga wa rafiki yako (RIP) nao umechangia mno?? Mtu atakukonvisije uweke nyumba zako TANO rehani ili mpate mtaji wa kupeleka korosho India, for Christ sake!? Si angeanza na moja, kisha mbili huku akiwa amejiwekea malengo kuwa ikifika nyumba tatu hajaona la maana basi he/she calls it a day na anabaki na nyumba zake mbili!!??
 
aisee hivi Abood huyu mheshimiwa waziri/naibu waziri na yule wa Morogoro ni ndugu?

labda ni majina tu, majina ya kiislam mengi hayana "sirname", hii ya kwetu ya kibantu, huwa ni first name ya mtu na first name ya baba.
na huyu waziri anatokea zenji
 
uendeshaji wa ile kampuni nao ulikuwa mbovu. Huyu mzee alisomesha wanawe na baada ya kumaliza akawakabidhi mali zake waendeshe, hawa watoto hawakuwa makini kabisa, kuna wajanja walikuwa wanawazunguka na kuchota hela watakavyo. kuna kijana mmoja alifanya kazi pale alitumia ujanja ujanja na alivuna sana mpaka kujenga baadaye walimshtukia wakamfukuza.
 
kuna kampuni pia ya Buffalo, sasa hivi ipo ipo tu lakini enzi zake ilikuwa basi nane zinaondoka kwenda AR na 8 zinashuka, barabarani hakuna wa kuzigusa, lakini sasa hivi naona ni kama 2 tu? wchambuzi wanadai pia kulikuwa na mkono wa wakubwa ila JK alivoingia, nadhani akawaambia 'waache' na pengine kufilisiwa.

Scandinavia ilikuwa imekuwa na a good public image, nadhani kuna makosa walifanya, hawajatengemaa tangu wakati walipotikiswa na mabenki kama CRDB. Mfano basi la Mombasa linaweza kuondoika na watu 6 tu, na ni kila siku, apo kuna biashara kweli? Mi nilimshihudia dereva wake akiuza mafuta kuganga njaa!
 
Bhaghosha,

Niwaulize huyo KISARIKA si ndie huyu advocate arie fariki majuzi nyumbani kwake na amezikwa moshi last may 2009,??? maana na hao mnao wataja ni washirika wake kwa kumbukumbu nazo zikumbuka.

Na huyo Adv. Kisarika nasikia huko kwao kuna mahali kanunua shamba kubwa na kuwanyima wenyeji njia,

Mkichunguza sana hawa ma Adv. wetu humu nchini wana mambo mazito sana mkiwachunguza wengi wao ni wana uchu sana na hela na kukamata viwanja vikubwa mno pita kiasi na vingi huwa ni scandle ful ful.

Chunguzeni mtajionea nanyi
 
...Mama Joe! hapo sijui niseme kuwa na ujinga wa rafiki yako (RIP) nao umechangia mno?? Mtu atakukonvisije uweke nyumba zako TANO rehani ili mpate mtaji wa kupeleka korosho India, for Christ sake!? Si angeanza na moja, kisha mbili huku akiwa amejiwekea malengo kuwa ikifika nyumba tatu hajaona la maana basi he/she calls it a day na anabaki na nyumba zake mbili!!??

we acha tu alimshawishi sana sana na issue ni kuwa ilikuwa inahitajika more than 100million cash kuanzia biashara ndo chanzo cha kumfuata yeye ili akope wapate mtaji. Unajua ukimuamini mtu hasa nyie wanaume unaona hawezi kukupa wazo baya na kweli wazo lilikuwa zuri, ila market ya korosho ghafla ikageukia India, hivyo wakabaki hawana means na korosho mkononi na matumizi mengine yameishazimaliza zile 100m, alipokea 20m tu ya miezi miwili kisha kimya........ hadi benki wanakuja kumshtua ilikuwa shock! Biashara lazima ujue kinafanyika nini hasa sio urafiki, undugu sasa wengine hawaelewi hiyo.
 
Halafu walikuwa on time hata kama wana abiria mmoja! nadhani hili pia lilichangia kuanguka kwa kampuni maana walikuwa wanapata hasara!

Makampuni mengine waliwaangalia tu...sasa makampuni kama Abood, Hood, dar express yapo siku zote mbona hayafilisiki? Au hayakuchukua mikopo?

Kifo cha Scandinavia Express hakikutokana na tatizo la kibiashara. Hapana. Kimetokana na siasa. Kuna baadhi ya wanasiasa waliingiza pesa zao, kama yalivyo makampuni mengine ya akina Shabiby na kadhalika. Kwa bahati mbaya, wanasiasa hawa walikuja kukosana wakati wamchakato wa kumpata mgombea urais kupitia CCM mwaka 2005. Kwa bahati mbaya sana wale walioshindwa kuingiza mgombea wao ndio waliokuwa na mtaji mkubwa, na hivyo kutokana na hasira na kukomoana, waliamua walichomoa mtaji wao. Hawakuishia hap, walishawishi vyombo vya fedha vilivyokuwa vikiwaunga mkono kudai marejesho ya mikopo kwa mkupuo mmoja. Kitendo hiki kilisababisha kuyumba na hatimaye kifo cha SES tunachokishuhudia kwa sasa. Ni ugomvi baina ya 'wanamtandao' na wasiokuwemo ndani ya mtandao wa JK. Aidha tusisahau kuwa wanasiasa wote walikuwa wamechukua mikopo mikubwa 'isiyorasmi' kutoka katika 'kampuni yao' ya SES kwa ajili ya kugharimia shughuli za kisiasa.
'Bagambila balinsi'..... wanye masikio na wasikie sasa. Habari ndiyo hiyo!
 
mnh! haya nd' maisha wakuuuu mana haya mabasi yalikuwa yanisaidia sana kupata fedha zangu za matumizi kipindi kile niko huko shule mkoani................
 
Mh jamani All who have dropped their point are all heavy.
You really have points U gays.
If you devote to something make sure You follow the right principles and make sure You achieve the goals ahead You. Do business jointly while your eyes are widely open otherwise You die kifo cha mende.
There some people one can count on business and othets no. Because others are only thinking of eating and not benefit.
 
Owner ni Huyu Mkuu:

Mr. Mohamed Abdullah
Scandinavian Express Services Ltd.
P.O.Box 2414, Tel: 2850847/9
Fax: 2850224, Mob: 0754-336611
E-mail: Scandinavia@raha.com
Dar es Salaam

Mara nyingi usilolijua linakusumbua,baadhi ya wakubwa ambao walikuwa wameweka pesa zao walipozivuta ndo chombo kilipoenda mrama wakuu....
sasa zaidi yahapo sisemi lakini ndo ukweli huo.
 
Kuna watu waliotowa msingi wa kuianzisha Kampuni hii (kimali na kikazi) ilipokuwa ndogo sana, mtafuruku ukaanzia enzi hizo ilipokuwa inaanza kujulikana na kukubalika kupata mikopo kede-kede, kuna katika waliotowa msingi kwa kuanzishwa kwa kampuni hii, mawazo yao hayakusikilizwa na Mo akawaona kuwa ni wajinga, ya ama akaachana na kusikiliza mawazo yao ya ama akaamuwa kuwapa hesabu zao na watokomee.

Mo, akajaza mashemeji kuwa ni mameneja wa kampuni, hawa mashemeji, most of them walikuwa na very minimal education, na walitumia uzoefu wa kukurupuka na kufanya kazi kienyeji bila mpangilio maalum. Matokeo ndio haya tunayoyaona.

Mo is a good man, he thought he is doing the best for the company but unfortunately he was destroying it, its a miracle it took this long to go down.
 
Mkuu,

makampuni mengi ya Mabasi hayana maisha marefu. Nikiwa Moshi nakumbuka kulikuwa na Makampuni yalivuma kama Lang'ata, Ngorika, Yellow, TAMT nk. Lakini yote sasa hivi Kwishnei.

Ngorika bado wapo wanajikongoja taratibu, kwa sasa wana mabasi ya Dar - Arusha na Arusha - Tanga

Hivi nani mmiliki/wamiliki wa Scandinavian Express? Kuna kipindi nilikua nasikia tetesi kuwa John Momose Cheyo(Mapesa) alikua mmoja wa wamiliki ila sina uhakika.

Si kweli, mmiliki halisi wa Scandinavia ni Bwana Mohamed Abdullah, na huyu bwana ndie mwenyekiti wa wamiliki wa mabasi ya abiria Tanzania (TABOA)

Mh jamani All who have dropped their point are all heavy.
You really have points U gays.

Tafadhali tuombe radhi, sisi sio mashoga!
Koma kabisa!
 
Jamani mnajua jumapili niliangalia komedi original kile kipande cha aliefulia,ndo nikazinduka kuwa hii kampuni haipo,sikutegemea kama ingekuja kupoteza umaarufu kirahisi hivyo.
 
...Mimi nimetoka Lushoto siku ya jumatatu. Nakumbuka kupishana na mabasi mawili matatu ya Scandnavia. Ina maana wanaruhusiwa bado kuendelea na biashara ama yalikuwa yamekodishwa tu??
 
ni masikitiko makubwa, ni kampuni ambayo nilikuwa naitumia sana kwa safari zangu za humu nchini. Sumaye alikuwa na mkono wake sana pale, alivyoondoka tu, aliondoa shea zake na baadhi ya mabasi yaliuzwa kwa kampuni ya Mohamed Trans. Mbeleko ya Sumaye ilivyo achia wameshindwa kuhimili.
 
Mamaaaa weeeeeeee! Daaaaaaaa! hivi naota!!
yaaani wamefuliaaa!
Masikini sasa itabidi watafute biashara ingine kwani siku hizi inaangaliwa Pesa wewe unapeleka abiria mmoja Arusha unatengemea nini? angeiga mifano ya Shabaha na sasa Shabco, Saibaba, Buffalo Harambee, Serengeti na mengine kibao yanavyofanya kazi. Swali je kama angepewa tenda ya usafiri Dar es salaam angeweza???????????? jibuni wadau

wamefulia au wametulia?
 
Its sad coz ilishajijengea jina bora kabisa ndani na nje ya nchi, na wengi wetu tulishaiamini kwa kutuma mizigo yetu na pesa sehemu mbalimbali, but mkuu....... no matter how sad we are ukweli unabaki palepale kwamba WAMEFULIAAAAAA
 
tatizo kubwa ni management,tabu ya waswahili wakishakuwa na hela wanafikiri wanaweza kufanya kila kitu.
haya ndio matatizo ya kufanya biashara kubwa katika mfumo mdogo(sole propriotor)
alianza vizuri lakini management ilimuangusha
yanasemwa mengi kwamba eti aliingia katika biashara nyingine,
partiner wengine walijitoa na mengine mengi.
lakini ninachofikiria kuna kila sababu ya kusaidiwa kama inawezekana aibuke tena kwani ukiacha mengine kampuni imekuwa inafanya kazi kwa uaminifu hasa kwa wateja.
inamiliki mali nyingi za majengo ambozo zinaweza kubadilishwa
vilevile imaajili watu wengi na maisha yao yanaitegemea kampuni hii achilia mbali kodi ambayo imekuwa ikilipa kwa serikali.
ikiwa wageni wanaweza kusaidiwa wakafanya biashara zisizo tusaidia moja kwa moja na wakaondoka bili kutulipa kodi kwa nini huyu asiangaliwe akasaidiwa kama inawezekana
 
Kuanguka kwa kampuni ya mabasi ya scandinavia kulichangiwa na mambo mengi ambayo uongozi uliyafanya kwa maelekezo ya wana hisa.

Mabasi yalitumika sana kwenye kampeni za chama tawala.Mkutano wa Kikwete jangwani 2005 ndiyo yaliwachukua wananchi kutoka Kibaha, Bagamoyo, Kisarawe na Mkuranga kuwaleta Jangwani na kuwarudisha makwao baada ya mzee kudondoka uwanjani.

Mabasi yalikuwa yanasafiri hata kama idadi ya abiria ni ndogo
 
Back
Top Bottom