Kifo cha Kanumba: Ni uzembe tu? Sio Lulu!

Kifo cha Kanumba: Ni uzembe tu? Sio Lulu!

kwa nini lulu na mdogo'ake kanumba wasingesaidiana kumpa huduma ya kwanza? Lulu hakwepeki kwenye hizo lawama, iweje atoe tu taarifa na kukimbia asitoe ushirikiano kumpatia msaada kanumba! Mimi nasema lulu hawezi kujinusuru ktk hzo lawama.

Nyinyi munaohukumu na kulaumu nadhani munasahau jambo moja au mawili. Kwanza ni kwamba munaangalia sasa documentaries za crime and investigation kwa hivyo munatarajia mambo huwa yanatokea kivile muda wote.

Pili mumesahau kwamba hapa ni Afrika, huyo ndugu yake hakuwa prepared to deal with such emergencies psychologically, na ndiyo maana akaona bora amuite daktari. Vile vile elimu yake imefikia wapi ili kuweza kuchanganua mambo kwa urahisi zaidi.

Lawama za kiSherlock Holmes hazisaidii kitu kwa kwetu Afrika.
 
.........Ila hadi uchunguzi ukamilike itachukua muda, na kipindi chote hicho Lulu atakuwa rumande labda kama atapata dhamana. Na hata kama akija kuachiwa huru......atakuwa na kovu ambalo halitapona maishani mwake yote.
Hatokuwa Lulu yule yule tuliomzoea. Namuonea huruma sana Lulu.

l
 
i can see this kanumba-lulu conundrum has turned into a field day for professional and bush lawyers alike...
 
Mkuu Nas Das.hakika umenena.yote uliyoongea yana ukweli mtupu,kama wanajamii F

tukielewana hakuna Police wala hakimu ambaye anaweza akamhukumu yule mtoto,
mengine tuyaache kama yalivyo na si kama tunaingilia uhuru wa police,atleast pawe
na pakuanzia,ni mara nyingi tumeshuhudia haki ya mtu ikinyongwa na kushangaa kama
kweli aliyehukumu ni Hakimu kweli na aliyesomeshwa kwa kodi za wananchi tena walalahoi
au alikuwa anazingatia misingi ya haki inasema nini!
R.I.P- S.KANUMBA
 
Wanabodi,

Kwanza tuendelee kupeana pole kwa msiba wa mpendwa wetu Stephen Kanumba.

Leo nimeisikia taarifa ya awali ya polisi ikielezea mwili wa marehemu umekutwa na jeraha kichwani na kushikiliwa kwa binti Lulu mwenye umri wa miaka 18 kuisaidia polisi katika uchunguzi huo!. Taarifa ya daktari kuhusu kilichosababisha kifo bado haijatolewa!.

Hili ni jukwaa la jamii inteligence likijikita zaidi kwenye facts na sio hisia na hoja hapa sio kupeana pole za msiba wala kumtetea huyu binti Lulu ambaye anataka kibebeshwa msalaba wa kifo cha Kanumba kama mhusika mkuu wakati ukweli halisi kuna kila dalili zinazoonyesha Kifo cha Kanumba japo kimesababishwa na ajali ya kuanguka na kujigonga, kinaweza kuwa kimesababishwa na uzembe wa watu fulani na sio huyu binti Lulu!.(kwanza nilipost kule jamii inteligence ikagoma)

Hoja hii inafuatia maswali mengi bila majibu ya ni nini haswa kilichotokea hiyo jana!.

Wewe kama uu mmoja wa mashabiki wa Kanumba na mpaka sasa una uchungu mkubwa na kifo hiki, nakishauri usichangie uzi huu maana utakosa objectivity na impartiatility kutokana na huzuni.

Hoja za msingi ni hizi.
1. Ugomvi ulitokea saa 6 usiku na mpaka majirani walisikia kelele. Mwili umefikishwa hospitali ya Muhimbili saa 11 Alfajiri, nini kilitokea hapo kati?.

2. Mdogo wa marehemu aliyekuwa nyumbani wakati huo ameongea kwenye TV kuwa aliposikia ugomvi akaenda kutoka kuingilia mlango ukafungwa kwa ndani, akaendelea kusikia vishindo ambavyo na majirani walivisikia, what did he do?, au mlango ukishafungwa basi ni kujiachia tuu liwalo na liwe, hapa sio kuna uzembe fulani?!.

3. Baadae Lulu akaufungua mlango na kutoka kama alivyozaliwa na kumweleza huyo kijana Kanumba ameanguka hiyo ilikuwa ni around saa 6 usiku, huyo kijana ulikwenda chumbani na kumkuta Kanumba kama alivyozaliwa anagalagala chini huku povu likimtoka mdomoni, what did he do first?.

4. Anasema alimpigia simu daktari wake!. Hivi kweli unaitwa chumbani na kumuona mtu ameanguka anavuja damu anatapatapa, wewe utamtafuta kwanza daktari wake au kazi ya kwanza ni kumkimbiza mgonjwa hospitali ya karibu?. Pale kwa Kanumba mpaka hospitali ya Sinza Palestina ambayo ni 24/7 ni only 5 minites away!. Tukio limetokea saa 6 usiku mwili wapelekwa Muhimbili 11 alfajiri!. Kulitokea nini hapo?!. Hapo sio uzembe fulani huu?!.

5. Hivi ni kweli Kanumba alikuwa na daktari wake?. Jee alikuwa ana suffering something kiasi kwamba kuna daktari maalum ndio huwa anamhudumia hali iliyolazimisha lazima atafutwe huko aliko ndipo Kanumba apate huduma ya kwanza!. Kama tukio ni saa 6, daktari alipigiwa simu saa ngapi?, na alifika saa ngapi?, kumbukeni muda wote huo Kanumba anagalagala na kuvuja damu nyingi kumsubiria daktari wake afike?!. Huu sio uzembe fulani?.

6. Tunaelezwa daktari alipofika ndipo juhudi za kumkimbiza Muhimbili zikafuatia, huku kukipatikana tarifa za baadhi ya wasanii kufika hapo kwa Kanumba within minutes na wengine kukiri walimkuta mwili umeshaanza kuwa baridi, muda gani ulishapita toka tukio mpaka hao wasanii/majirani waliofika mwanzo and what did they do?!. Hapa kweli hakuna uzembe fulani?.

7. Tumeonyeshwa picha na TBC zikionyesha umati mkubwa wa wasanii ukiandamana kuupeleka mwili Muhimbili, ikumbukwe wakati tukio alikuwa kama alivyozaliwa ila mwili ulionekana umevishwa, hivyo emergence ya aina ile mgonjwa huwa anafunikwa tuu shuka na kuwahishwa hospitali, kupatikana muda mpaka kumvisha huu sio uzembe fulani?!.

8. Kama tukio ni la dharura tulitegemea watu wa kwanza ni majirani iweje wasanii wajazane kivile usiku huo mpaka na waandishi wa TBC?. Haiwezekani baada ya kutokea ajali hiyo ya kuanguka, badala ya kumpatia mgonjwa huduma ya kwanza ya kujaribu kuokoa maisha ya Kanumba, watu walikuwa bize kuwatafuta masuper star na waandishi wawahi tukio lile huku wengine wakiendelea kuhangaikia kuupiga picha mwili wa Kanumba licha ya kujua tayari ni dead body?!.

9. Kama hao waliofika wakanshika na kuona mwili umeanza baridi, ni muda gani daktari alifika?. Ni muda gani walijua Kanumba ameshafariki?, kama alifia nyumbani hawakujua hiyo sasa at that poit ni police case badala ya kuitana makundi ya wasanii na kuidramatise scene ya kifo cha Kanumba?!.

10. Mwisho kwa sababu ripoti ya daktari kutaja chanzo cha kifo haijatoka, naombeni tusimbebeshe mtoto Lulu msalaba wa kifo cha Kanumba!. Inawezekana ni Kanumba mwenyewe aliteleza, na hata kama ni kweli alimsukuma, kama alimsukuma in self defence, Lulu hana hatia yoyote kwa sababu kifo kitakuwa kimetokea kwa bahati mbaya bila kusudio la kutenda jinai ya mauaji!.

RIP SK The Great

Pasco.
Binafsi nilizipata taarifa hizi jana mchana.
But ntill now nilikua sijajua nini chanzo cha kifo chake.
Sasa nadhani naweza sema pia kuna kitu nyuma ya pazia.Kama kweli kulikua na misunderstanding chumbani,na majirani walisikia na wakafika eneo la tukio,why kwa kushilikiana na mdogo wa marehemu wasingevunja mrango?
There is some thing here,but let us wait first!
 
Mkuu Pasco,
Katika hili mie sina haja ya kutafuna maneno!! Hata kama nimehuzunishwa na kifo, bado napinga kwa nguvu zote huyu binti kuhusishwa na hiki kifo! Ikumbukwe kwamba, Kanumba kwa Lulu ni Kama Daud kwa Golliath…..!! Sina shaka yoyote kwamba, kutokana na wivu wa kimapienzi, Marehemu alianza kumshushia kisago Lulu! Bila shaka, kwa jinsi wanaume tulivyo, asilimia kubwa ya wengi wetu tungechukua uamuzi wa marehemu wa kuanza kumshushia binti kipigo!
Kwa upande mwingine, Lulu alikuwa na haki ya kujitetea! Kama nilivyosema hapo awali, Lulu kwa Kanumba ni sawa na Daud kwa Golliath! Ninachomaanisha, asingeweza kuchapana nae hivyo suluhisho pekee kwake ilikuwa ni kujinasua toka mikononi mwa marehemu! Kama chumba kisingekuwa kimefungwa (may be kilifungwa ili kichapo kitolewe sawasawa na asiwepo wa kukimbia) basi suluhisho la Lulu lingekuwa kutimua mbio! Lakini kwavile mlango ulikuwa umefungwa, Lulu alilazimika kwanza ,kumsukuma marehemu ili apate nafasi ya kutimua mbio na kufungua mlango! Jambo hili, lingefanywa na yeyote yule with exception of very few! Hata ningekuwa mimi, nisingekuwa na njia mbadala zaidi ya hiyo ya kumsukuma Kanumbe ili nipate uchochoro wa kutimua mbio! Hivyo, vyovyote iwavyo, Lulu hakuwa na namna zaidi ya hiyo ingawaje ni bahati mbaya hatua yake ya kujiokoa imezaa mauti kwa mwenzake! Tukija kwa mdogo wake Kanumba, huyo ndie mpuuzi kuliko wote….!!! Nazani ujinga kama sio upumbavu aliofanya ni kutaka kujaribu kuifunika hii issue kwavile aliona ingekuwa skendo kwa kaka yake!! Bila shaka, wakati akichelea kuchukua hatua ya kumpeleka hospitali au kuita majirani (ili kuficha skendo) kumbe ndo alikuwa anakaribisha kifo kwa kaka yake! Na hata hiyo hatua yake ya kuanza kwanza kumuita “daktari” wa Kanumba ilikuwa na lengo lile lile la kuficha skendo!
WASWAHILI WANASEMA, MFICHA MARADHI KIFO UMUUMBUA……hiki ndicho kilichotokea kwa Mpendwa wetu Kanumba!


Well said! I tend to agree with this line of thinking.
 
Hello Mr. Pasco,
Nimevutiwa sana na tafakuri ya mazingira ya kifo cha Kanumba. Kiukweli mimi binafsi niligubikwa na simanzi nzito ingawa niko mbali sana kwa sasa takribani mwaka mmoja niko china. Kanimba ni mmoja wa wasanii ambao niliwakubali sana katika tasnia ya filamu na hata akanifanya nikubali bongo muvie, na siku ya tukio nilikua naangalia muvie yake ya "Crazy Love", na niliumia sana kwenye scene ile ya yeye kupigwa baada ya kukutwa na mke wa mtu, akapigwa hata akapoteza timamu zake kwa muda. Mimi sina mengi juu ya hukumu yake kwani Allah ndiye hakimu.

LAKINI,

Nikafunguka fahamu na kujiuliza maswali wa kadha, ambayo pia yamenifanya nijiunge na jamii forum kwani sikua mwanachama wa platform hii. Kiukweli haya ni majambo ya kiinteligensia kweli na labda kuna vyombo ambavyo viko responsible kushughulikia kwa mujibu wa katiba yetu, ila mwananchi mwema hakatazwi kutoa mchango wa kuliona hili kwa upana kwani hata hao ambao wanahusika kwa sasa watategemea watu ambao walikuapo kwenye tukio. Nilijiuliza maswali mengi na si kwa mantiki ya kumgandamiza Lulu, ila swali langu ni kama ifuatavyo;

1. Nini kilifanya Lulu aondoke ilhali yule ni mpenziwe na sidhani kulikua na kitisho chochote kwake kutoka kwa bwana bosco ambacho kilimfanya yeye akimbie?

Halafu tafakuri ya muvie alizoigiza kanumba kaka zinanipa mshutko juu ya nguvu za hawa watu wanaitwa "Illuminati", inasadikiwa by saa saba usiku wa tarehe saba bwana kanumba alifariki dunia akitokea kuoga. Kuna vitu kadha hapa vya kuvitafakari, saa saba (7), tarehe saba (7) na jina lake likiwa na herufi saba (7), jumla yake ni zile triple seven (777) zinazohusishwa na kafara ya daraja ya juu kabisa kwa hawa freemason, na kuoga kumerepresent "Rain Man". Nina wasiwasi tukio hili ni zaidi ya Lulu, kwa kuwa kwa ninavyomjua mimi Lulu hana ubavu wa kumsukuma the great, na Lulu alikua kama alivyozaliwa, freemason wanawatumia wanawake kama agent of evil, naye lulu alikua katika umbo lile la ibilisi tena kwenye ijumaa kuu (siku ya saba katika juma). Utajiuliza kwa nini muda wote huo kama ulivyoeleza hapo juu, saa sita mpaka saa kumi na moja alfajiri, kivipi?, hapo palikua na mipango inafanyika. Na pia huyu jamaa wa nigeria anaeitwa Ramsey alikua Bongo few weeks ago, unajua alikuja kufanya nini? huyu ndie walie act muvie pamoja ile ya Evil Kingdom, unapata somo gani kutoka muvie ile? jiulize kwa kina utapata majibu. Kwa hivyo kwa tafakuri yangu mimi Lulu alikua scapegoat kufanikisha lengo la kafara ya juu kabisa na hivyo High profile celebrity Kanumba karata ilimwangukia na wengine wanafuata muda utakapofika.

Karibuni tuchanganue.
 
Mbona madkatri wanakataa kutibu watu mpaka waonyeshwe hiyo PF3?
bht umeji- mislead, madaktari watakataa kama watakuona kuwa una uwezo wa kwenda kuchukua hiyo PF 3 na hujafanya hivyo. na sio wanakataa, hapana. wanatia shaka juu ya kuumia kwako. jaribu kufikiria ajali ya majeruhi zaidi ya 20 walio na hali mbaya, uzoefu unaonyesha kuwa wanatibiwa kwanza PF 2 baadae. sababu kubwa ni kwamba chanzo cha majeraha yao kinajulikana.
 
haka kabint ndiyo kanajua ukweli wote, kwa jinsi baadhi ya blogs zinavyoripoti kwamba hataki kutoa ushirikiano na polisi na anataka lazima wakili wake awepo na vilevile yote anayozungumza yarekodiwe, sifikirii kama mtu unaweza ukaua mtu hiwe kwa bahati mbaya ama maksudi ukapata na ujasiri wa kuyadai yote hayo, kuna kikubwa zaidi ya hii ya kusukumana kimapenzi. ni hisia zangu tu lakini.
 
haka kabint ndiyo kanajua ukweli wote, kwa jinsi baadhi ya blogs zinavyoripoti kwamba hataki kutoa ushirikiano na polisi na anataka lazima wakili wake awepo na vilevile yote anayozungumza yarekodiwe, sifikirii kama mtu unaweza ukaua mtu hiwe kwa bahati mbaya ama maksudi ukapata na ujasiri wa kuyadai yote hayo, kuna kikubwa zaidi ya hii ya kusukumana kimapenzi. ni hisia zangu tu lakini.

Kama kweli hataki kutoa ushirikiano hadi apate uwakilishi wa kisheria basi yuko sahihi kabisa.
 
Jamani kwanini tusisubiri ripoti ya daktari na maelezo yake ndiyo tujadili?

Mtaniuliza kwanini... Sababu,kwamba, hatujui kama alidondoka mwenyewe,ama alisukumwa,hapa DNA itahusika kwenye nguo za marehemu,hasa maeneo ya kifuani ama tumboni.. Na hata zikionekana,zinachunguzika kama ni zamazingira ya kusukuma ama ya kupapasa,ama vinginevyo...

Lulu ndiye anayejua huko walikokuwa walikuwa wapi na walikuwa wamekaa na watu gani .... Na anatakiwa kueleza uhusiano alio nao na Kanumba kipindi cha uhai wake.. Hii itasaidia kujua kama anamjua vizuri na kama SK alikuwa na tatizo lolote la afya...

Na itasaidia na mambo mengine.. Forensic si kazi ndogo...
 
bht umeji- mislead, madaktari watakataa kama watakuona kuwa una uwezo wa kwenda kuchukua hiyo PF 3 na hujafanya hivyo. na sio wanakataa, hapana. wanatia shaka juu ya kuumia kwako. jaribu kufikiria ajali ya majeruhi zaidi ya 20 walio na hali mbaya, uzoefu unaonyesha kuwa wanatibiwa kwanza PF 2 baadae. sababu kubwa ni kwamba chanzo cha majeraha yao kinajulikana.

Hata kwangu haingii akilini kabisa...yaani kwa mfano wakuone unabubujikwa na damu na una hatari ya kupoteza damu nyingi na hivyo kupelekea kupoteza uhai halafu wakatae kukupa huduma kisa huna hiyo PF3.

That just defies common sense to me. Nadhani kama ulivyosema, wanaangalia pia na mtu ana hali gani.
 
haka kabint ndiyo kanajua ukweli wote, kwa jinsi baadhi ya blogs zinavyoripoti kwamba hataki kutoa ushirikiano na polisi na anataka lazima wakili wake awepo na vilevile yote anayozungumza yarekodiwe, sifikirii kama mtu unaweza ukaua mtu hiwe kwa bahati mbaya ama maksudi ukapata na ujasiri wa kuyadai yote hayo, kuna kikubwa zaidi ya hii ya kusukumana kimapenzi. ni hisia zangu tu lakini.

Hata nawe, pale yanapokukuta jitahidi kuyadai haya....kama una mwasheria wako, make sure anaratibu zoezi hilo! Usisahau kwamba, kuna maelfu kwa maelfu ya watu wanaingia hatiani si kwavile wametenda kosa husika bali wameshindwa kujitetea....kauli ya kwanza inaweza kukufunga usipokuwa makini; therefore, do undermine her kwa lolote lile lakini si hili la kutaka kwanza mwanasheria wake awepo!!
 
Nilikwisha sema kwenye thread nyengine, huyu binti kivyovyoye hawezi kuonekana mkosa! Kwanini;
1 binti amekutwa na majeraha, ina maana kuwa kulikua na fights, hivyo binti huyo alikua anajilinde "SELF DEFENSE"
2 ugomvi ulianzia kwenye simu kama inavyosemwa, simu ni personal property, kitu cha private, kumpokonya na kuanza kumshambulia ni kosa!
3 hakuna silaha ilotumika, Kanumba kateleza au kasukumwa yote mawili ni possible, km nlivokwisha sema self defense ni haki yake binti.
4 walikitwa uchi?! Ee! Binti akisema kuwa alikua analazimishwa ngono je? Balaa
5 Kanumba alikua na huyu binti tangu alivokuwa under 18?!! Hii ni dhambi, km msemavyo biblia inavosema "mshahara wa dhambi kifo" Kanumba amepata mshahara wake! Alistahiki kifungo cha miaka 30 kwenda mbele

Namalizia huyu binti kutokana na facts na story ilivo na kama alivohadithia nduguye kanumbe basi binti ni INNOCENT! ushabiki uwekwe pembeni.
 
Wabe, hawa watoto wetu wa .com kuna vitu huwezi amini. Mimi nimeanza kunywa pombe five years baada ya kuanza kazi na mpake leo sivuti hata sigara japo nilishajaribu kuvuta kila kitu.

I'm now a father of 6, 4 teens na two minors. Hawa teens wakubwa akiwemo huyo binti wa 18, wameshafanya almost everything!. With such a team. you have to be friends na watoto wako, nani miongoni mwao watakuambia mwenzao amewahi kufanya nini!. Nimeshaitwa kwenye kesi kibao za shule mpaka sasa niko kwenye kamati mbili za shule tofauti!.

Nakubali mwana umleavyo ndivyo akuavyo, ila amini usiamini, unajitahidi to give the best to your kids, halafu mtoto anakuja kuwa na tabia za ajabu kwa kufanya mambo ya ajabu na kushangaza mpaka kushindwa kuamini!.

Ziko baathi ya tabia za ajabu za watoto wetu mpaka zinatishia kuhatarisha ndoa zetu, kwa kuhisi au "umesingiziwa nini?"!

Unaweza kukuta kwenye hiki kisa cha Lulu, kiLulu chenyewe wala hakijali kihivyo wala hakijui kimefanya nini wala consequenses ni nini, utakuta anaetesema na kulia zaidi ni mama yake!

ha ha haa!

umesema kama baba, kama mzazi sina la kuongeza. wazazi lets play our part mengine Mungu atusaidie...
 
Back
Top Bottom