Kifo cha Lowassa: Rekodi ziendelee kuwekwa sawa vingenevyo historia itapotea

Ni kweli Edward Ngoyai Lowassa ni Mmeru na sio mmasai. Tuliyomfahamu tungali watoto tunalijua hilo. Sema alizaliwa masaini na alikijua kimasai angali mtoto kama ilivyokua kwa familia yake yote iliyokua ya kifugaji. Pia wazee wa kimasai walimpitisha kimila kua kabila lao na pia kumsimika uongozi wa kijadi kama Laigwanan. Halafu jambo wasiolijua wengi wameru japo kilugha wanakaribiana na wamachame wao wana mila sawa na wamasai. Sio rahisi ukubalike kama mmasai hujapita jando kama yao na kupata rika ya kimasai.
 
Urafiki haupimwi kwa muda tu. Unaweza mpata rafiki mwishoni mwa maisha yako ukatamani, ungemjua toka zamani.

Ukizungumzia kugombea urais wa JMT, Lowassa hakugombea kupitia kwetu CCM bali kupitia CHADEMA, na hicho pia huwezi futa kwa sababu ni mojawapo ya heshima na achievements kubwa alizopata katika maisha yake.
 
Nakubaliana na wewe; sasa nini kiigizwe na kipi kiachwe- hiyo ndiyo hoja yangu
 
Kabila la mtu linapimwaje? Mimi nikiamua kuwa mmakonde, kuna shida? Je, kuna wameru wengine waliojiconvert kuwa Wamaasai?
Mkuu huwezi kubadili kabila-Obama alikuwa mjaluo na akabaki mjaluo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…