mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 14,205
- 19,142
Mawakala wa mabeberu walikuwa wanajitahidi Sana kuiaminisha Dunia kuwa Watanzania wako kwenye mateso Sana chini ya utawala wa Rais Magufuli. Waliamini watanzania walio wengi watafurahi Sana na kushangilia Magufuli atakapoondoka madarakani au atakapofariki.
Kinyume chake mabeberu na mawakala wao (wakiongozwa na mkimbizi aliyeko ughaibuni huko ulaya) wamelazimika kushuhudia kwa macho yao umati mkubwa sana uliojitokeza kwa hiari kumuaga shujaa wao Magufuli!! Cha ajabu hata vyombo vyao vya habari kama BBC world service ukiingia kwenye tovuti yao hutakuta habari hii.
Laiti kama nyomi hii ya watu waliojitokeza kumsindikiza shujaa wao, ingekuwa ni maandamano ya kuipinga serikali ya Magufuli, vyombo vyote vya habari duniani vingeipa uzito wa kwanza habari hii kwa wiki nzima! Lakini kwa sasa ukifungua tovuti ya BBC news hutaona habari hii, kwa nini??
Sababu ni aibu!! Siku zote hivi vyombo vimetumika kuiaminisha Dunia kuwa Magufuli hajali watu wake, Magufuli ni mbaya, Magufuli ni dikteta. Waliaminishwa kuwa Magufuli akiondoka watu watafurahi!! Sasa kuionesha Dunia hali halisi ya watanzania walivyokuwa wanampenda kiongozi wao hawawezi!! Hawawezi kujiumbua uongo wao!! Ila wameona japo hawawezi kukiri kuwa Magufuli alipendwa Sana!! Labda anaweza kuzidiwa na baba wa Taifa tu mwl Nyerere!
Kinachowauma zaidi ni utulivu ulivyotawala!! Lingine kinachowauma zaidi ni jembe lililopokea kijiti!! Mama la nguvu Bi Samia Suluhu!! Kwanza kwa kuwaonesha jeuri hakuvaa ile "hirizi" ya wazungu wanayodai inawakinga na corona!! Hilo jopo lote la kitaifa halikuvaa hiyo "hirizi" usoni!!
Hiyo hirizi haijaweza kuwaokoa wao, itatuokoaje sisi? Hiyo Kinga ikitangulizwa mbele ya Mungu inageuka kuwa hirizi. Ukimtanguluza Mungu kwanza halafu hiyo Kinga inafuata inakuwa ni Kinga ya kawaida tu!! Sisi watanzania tumemtanguliza Mungu na Mungu ametuponya!! Mabeberu mtasubiri sana kuona vibaraka wenu wanapata nafasi nchini mwetu.
Nawahakikishia mabeberu watajuta!! Kwa hili jembe lililopokea kijiti, watasema ni afadhali ya Magufuli!! Uzalendo wa huyu mama mpaka nchi utasikia raha! Na mabeberu hawapendi kiongozi awe mzalendo wa nchi yake! Mabeberu wanapenda kiongozi awe wakala wao ilu waweze kuinyonya nchi!! Kwa Bi Samia Suluhu wameula wa chuya!!