The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Kwa wanaokumbuka kilichoitokea KANU nchini Kenya baada ya Daniel arap Moi kuachia madaraka mwaka 2002 watakumbuka maneno haya kutegemea na CCM itakavyoendesha utawala wake baada ya kifo cha John Magufuli. Kama watagombania madaraka au kuyatumia vibaya na upinzani ukajizatiti, unaweza kuwa mwisho wake.
Hata kule Zambia na Malawi haya yalitokea. Siitakii mabaya CCM. Ila kama watarejea mazoea yao ya kuwa chama cha majambazi, wajue mwaka 2025 wataonja shubiri. Hivyo, kuendeleza kazi na mema ya Magufuli siyo chaguo bali shurti la kuendelea kuiongoza Tanzania. Wasifanye kama ANC ambayo ilinusirika kuonja shubiri baada ya kuongozwa na fisadi Zuma.
Hivyo, CCM wajue wazi umma unawaangalia na una kumbukumbu hasa ikizingatiwa uhondo walioonja chini ya hayati Magufuli. NI wazo na ushauri wa bure. Sijui wanangu mnasemaje?