Kifo cha Mandojo pigo kwa wapenzi wa Bongofleva middle age

Kifo cha Mandojo pigo kwa wapenzi wa Bongofleva middle age

hii tabia ya wananchi kujichukulia atua mkononi ni wakati sasa jeshi la polisi kulivalia njuga

Kuna usiku maeneo fulani tulimuokoa mtu aliyeitiwa mwizi kumbe waliomuitia mwizi ndio walikuwa wezi wenyewe wanataka kumuibia.

Binafsi nilishawahi kukurupushwa na vibaka usiku maeneo fulani, wale jamaa kama wangeniitia mwizi ningeweza kufa na mimi.

Kuna haja sasa watu kustaarabika na kuvihusisha vyombo vya dola baadala ya kukimbilia kupiga.
 
Wapo wenye hali nzuri sana tu, ndio maana akifariki kutatolewa michango mingi, si bure jeneza litanunuliwa na Mtu mmoja tu...ila akiwa Hospitalini husikii hilo

Halafu kuna Waigizaji, Watangazaji na Waimbaji
Wangeanza kuhimizwa hao mmojammoja na wasanii ili wasafishe mapito.
 
Dodoma kumekuwaje ? Juzi hapo walimbaka binti wa watu leo ni mengine,

Rest Easy.
 
Leo hii, ulimwengu wa muziki umepata pigo kubwa sana kwa kifo cha Mandojo, msanii maarufu aliyejulikana kwa umahiri wake wa kuimba na kupiga gitaa. Mandojo, ambaye jina lake kamili ni Joseph Francis, amefariki kwa njia isiyosadikika—kupigwa hadi kufa baada ya kudhaniwa kuwa ni mwizi.

Tukio hili la kusikitisha limeacha pengo kubwa si tu kwa familia yake na mashabiki, bali pia kwa ulimwengu mzima wa muziki ambao umemshuhudia Mandojo akichanua kama mmoja wa wasanii wakubwa wa kizazi chetu hasa Mwaka 2004. Mara ya kwanza tulionana Arusha Mwaka 2018 rafiki yangu Abel akinikutanisha na wewe na ukaahidi ukija Mbeya utanitembelea. Toka hapo ukawa Kaka yangu from another mother.

Mandojo alikuwa na kipaji adimu ambacho kiliwavutia wengi. Alikuwa na uwezo wa kipekee wa kuchanganya sauti yake laini na ya kipekee na ala ya gitaa, kuunda muziki uliogusa roho za watu wengi. Uimbaji wake ulikuwa na nguvu za kipekee; sauti yake ilikuwa kama mto uliojaa upole na faraja, lakini yenye uwezo wa kupasua mioyo kwa hisia kali.

Gitaa lake, ambalo lilikuwa kama rafiki wa dhati kwake ukiachana na Swahiba wake wa muda wote Domokaya, lilijua siri zote za moyo wa Mandojo. Kwa miaka mingi, walikuwa kama mwili na roho, wakisukumana huku na kule, wakitengeneza muziki uliowafanya wengi kuzama kwenye mawazo na kutafakari.

Gitaa lake sasa limesalia na huzuni, likitamani mikono ile yenye upendo na ujuzi ingekuwa hapo kuligusa tena, lakini sasa limebaki na kumbukumbu tu za zile nyakati nzuri walizoshirikiana na Mandojo. Gitaa hilo litamkumbuka sana Mandojo, likilia kwa sauti ya ukimya.

Kifo cha Mandojo ni pigo kubwa sana kwa jamii yetu. Ni kifo cha kipaji, ndoto, na furaha ya wengi. Ni pigo ambalo limeacha majonzi na maswali mengi; kwa nini kipaji kama hiki kikatiliwe uhai wake kwa njia ya kikatili kiasi hiki? Hakuna maneno yanayoweza kueleza uchungu wa kupoteza msanii wa kiwango cha Mandojo, aliyekuwa na ndoto na uwezo wa kubadilisha maisha ya wengi kupitia muziki wake.

Tunapoomboleza kifo chake, ni muhimu tuendeleze urithi wake. Tuna wajibu wa kuhakikisha kwamba haki inapatikana kwa Mandojo, na kwamba jamii inajifunza kutokana na kifo hiki cha kusikitisha. Kwa njia hii, kipaji chake hakitapotea bure, bali kitakuwa kumbukumbu ya nguvu za muziki na umuhimu wa haki katika jamii yetu.

Mandojo hatakuwa nasi tena, lakini sauti yake itaendelea kuishi milele kupitia nyimbo zake. Gitaa lake litabaki na kumbukumbu ya mwimbaji ambaye alilijua zaidi ya yeyote, na sisi, tutakumbuka Mandojo kama msanii mkubwa ambaye alituacha kabla ya wakati wake. Tumepoteza kipaji, tumepoteza rafiki, lakini zaidi ya yote, tumepoteza sauti iliyokuwa na uwezo wa kuleta nuru katika giza.

Pumzika kwa amani, Mandojo. Sauti yako itaendelea kusikika, hata kama wewe mwenyewe hautakuwa nasi tena. Gitaa lako litakuimbia nyimbo za majonzi, likikukumbuka milele.

View attachment 3066909

Pia soma=> Mwanamuziki wa Bongo fleva Mandojo afariki Dunia
Ila anaonekana alikua anakula cha Arusha sana
 
Hawa wasanii sio wa kuwaonea huruma wakifulia, hebu ona wanavyoipamba CCM

Matukio kibao yanatokea nchii hii wako kimya hawatumii ushawishi wao kwenye jamii kukemea

Wakipatwa na matatizo eti jamii tuwakumbuke big NO

Kanye ulipokula
This is insensitive, stupid and psychotic
 
Lazima alikuwa mwizi Kuna mwingine Yuko kigamboni wa enzi hizohizo 2004 ukimwona wakikuambia mwizi huoni sababu ya kukataa
 
Wapo wenye hali nzuri sana tu, ndio maana akifariki kutatolewa michango mingi, si bure jeneza litanunuliwa na Mtu mmoja tu...ila akiwa Hospitalini husikii hilo

Halafu kuna Waigizaji, Watangazaji na Waimbaji
Nyie ujamaa unawasumbua.. Mnataka watu wakae wanachangia watu... Come on.. Hata Yesu alisema masikini mnao siku zote. Msibani lazima tuje kushirikiana lakini mawazo ya Michango futa
 
Ila kwa muonekano tu wa uyu mwamba ni wazi kabisa alikuwa anaizo tabia coz sometimes alosto zinawaelemea, ata ivyo isingekuwa rahis watu kumtambua kuwa uyu ni mandojo sabab wasanii wa kale hawatrend sana kwa mionekano yao kumtambua kirahisi kuwa uyu ni fulani. Mfano leo umuone PNC sio rahis kumtambua japo alivuma kipindi hapakuwa na media
 
Lazima alikuwa mwizi Kuna mwingine Yuko kigamboni wa enzi hizohizo 2004 ukimwona wakikuambia mwizi huoni sababu ya kukataa
Unamzungumzia Jose mtambo au?
Mkuu tusiwe wepesi kufanya judgement - Kuhusu Mandojo tusubiri taarifa sahihi kuhusu nini hasa kilitokea, tusihukumu mapema
 
Unamzungumzia Jose mtambo au?
Mkuu tusiwe wepesi kufanya judgement - Kuhusu Mandojo tusubiri taarifa sahihi kuhusu nini hasa kilitokea, tusihukumu mapema
Aliyekuwa anakurupushana nae usiku gizani ndie aliita mwiziiiiiii , usiku badala awe studio anakurupushana na watu ! Msitete wanahitaji msaada

Kuhusu uliyetaja Mimi sijamtaja
 
Hawa wasanii sio wa kuwaonea huruma wakifulia, hebu ona wanavyoipamba CCM

Matukio kibao yanatokea nchii hii wako kimya hawatumii ushawishi wao kwenye jamii kukemea

Wakipatwa na matatizo eti jamii tuwakumbuke big NO

Kanye ulipokula
Hiii kweli wasanii kwenye baadhi ya mambo ambayo sio fair yanayofanywa na viongozi huwa hawakemei licha ya kua na platform ya kufanya hvo yakiwafika wanataka support ya wananchi
 
Naona upotoshaji mwingi wa nini hasa kilimkumba marehemu, bila shaka CCM tayari wamevamia uzi.
 
Back
Top Bottom