The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 9,436
- 10,944
Kwamba Mume wa marehemu hajulikani jina au jina limehifadhiwa Kwa sababu za kiuchunguzi?
Wanaume tambueni kwamba ukiona msomi tena mtumishi usiwe na moyo mdogo vinginevyo yatakukuta.
=========
DAR ES SALAAM - MWILI wa mfamasia wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke, Magdalena Kaduma umekutwa umefukiwa pembezoni mwa nyumba aliyokuwa akiishi huku sababu ya kifo chake kikiwa hakijulikani.
Jeshi la Polisi linamshikilia mume kwa uchunguzi. Inadaiwa kuwa tangu alipoondoka nyumbani kwake Desemba 4, mwaka huu kuelekea kazini kwake, hakuonekana nyumbani hadi Ijumaa 6 saa 9:00 alasiri ndugu zake na wajumbe wa Mtaa Hondogo, Kata ya Kibamba, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam walipobaini mwili wake ukiwa umefukiwa meta 15 kutoka ilipo nyumba yake.
Mashuhuda wa tukio hilo, akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa wa Hondogo, Leonard Sabuni, walisema kuwa walikuta mwili huo ukiwa umevimba na kuanza kutoa harufu.
Katika tukio hilo, mume wa Magdalena ambaye hajafahamika jina, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kutokana na kifo hicho huku mfanyakazi wa ndani wa kiume aliyekuwa akiishi pamoja nao, akidaiwa kuwa ametoroka.
Akizungumza na HabariLEO kuhusu tukio hilo, Sabuni alisema kuwa juzi (Ijumaa) saa 4:00 asubuhi, wazazi wa Magdalena wanaoishi Tabata ulipo msiba kwa sasa, walifika ofisi za mtaa kutoa taarifa ya kupotelewa mtoto wao tangu Jumatano ya Desemba 4, mwaka huu.
“Niliwaambia kuwa tumepokea taarifa yao, lakini walisisitiza kwamba twende nyumbani tukatafute, wajumbe wangu walitoka na kwenda nao nyumbani lakini baadaye wakashauri kwenda Kituo cha Polisi Gogoni,” alisema Sabuni.
Habari Leo