Kifo cha mtoto albino kinataka amri ya Rais sio masikitiko ya Rais

Kifo cha mtoto albino kinataka amri ya Rais sio masikitiko ya Rais

Tatizo watanzania mnapenda sana kufanyiwa maigizo na wanasiasa. Mama angeongea kwa povu ndo mngeshangilia hata kama hakuna hatua itakayochukuliwa. Mama kaamua kufanya kazi kwa utaratibu na sio kupayuka majukwaani. Au mnataka mama naye aseme "I wish i could IGP?" ndo mridhike?
 
Akiwa kwenye Kongamano la Maendeleo ya Habari, Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha masikitiko kutokana na kifo cha mtoto mwenye ulemavu wa ngozi kule Kagera.

Rais ametaka watu waliokuwa kwenye kongamano wasimame na kumuombea. Hata hivyo hakutoa kauli ya kimamlaka kutaka waliohusika wakamatwe.

Natoa wito wa kusoma, tukio lile la kusikitisha linataka Kauli ya Amri ya Rais, sio sala na maombi huku watu wanaendelea kufa.
Umeongea cha maana sana! Huyu hakujiandaa kuwa hapo! Alivamiwa TU!
 
Back
Top Bottom