Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Historia ya Umoja wa Kisovyeti imejaa simulizi nzito za siasa, mapinduzi na hofu isiyo na kipimo. Lakini miongoni mwa simulizi hizo, kifo cha Nadezhda Sergeyevna Alliluyeva, mke wa pili wa Joseph Stalin, bado ni fumbo kubwa linalowachanganya wanahistoria hadi leo.
Ingawa serikali ya wakati huo ilitangaza kuwa alikufa kwa ugonjwa wa appendicitis, ushahidi wa kihistoria unaonyesha kuwa kifo chake ilikuwa ni mpango wa siri wa Joseph Stalin. Swali kubwa limeendelea kubaki: Je, Nadezhda alijiua, au aliuawa? Na kama aliuawa, je, Stalin alihusika?
Nadezhda Alliluyeva alizaliwa mwaka 1901 mjini Baku katika familia iliyojikita sana katika harakati za mapinduzi ya Bolshevik.
Baba yake binti, Sergei Alliluyev, alikuwa mwanachama wa mwanzo kabsa wa Chama cha Russian Social Democratic Labour Party (RSDLP) na rafiki wa karibu wa viongozi wakuu wa mapinduzi, akiwemo Joseph Stalin.
Nyumba ya familia ya Alliluyev mara kwa mara ilitumika kuwaficha wanamapinduzi, akiwemo mwamba kabsa kwa jina la Vladimir Lenin pamoja na Stalin mwenyewe. Hivyo, Nadezhda alikulia katika mazingira ya siasa kali, hofu ya kukamatwa, na maisha ya mapambano yalikuwa sehemu ya maisha yake.
Nadezhda Alliluyeva alikuwa mwanamke mwenye mvuto wa kipekee, alikuwa mrembo wa ajabu. Mashahidi wa wakati huo na picha chache zilizobaki zinaonyesha mwanamke mwenye uso wa kuvutia, macho makubwa yenye huba, nywele nzuri sana tena nyeusi, na sura ya asili isiyopenda mapambo makubwa, kwa ufupi alikuwa ni natural halafu pisi kali.
Alipendelea kuvaa mavazi ya kawaida, kwa kufuata itikadi ya Bolshevik ya kupinga anasa, lakini hata katika unyenyekevu wake, urembo wake ulijitokeza wazi. Binti yake, Svetlana Alliluyeva, aliwahi kuandika kuwa mama yake alikuwa “mzuri, yaani urembo wa kimya kimya, si wa kujionesha, bali wa kuvutia kwa tabia na akili,” kwa lugha nyepesi alikuwa BEAUTY WITH BRAIN.
Nadezhda alimfahamu Stalin tangu akiwa mtoto mdogo. Stalin, aliyekuwa mkubwa kwake kwa takribani miaka 20, alikuja kuwa sehemu ya familia yao. Baada tu ya Mapinduzi ya Urusi ya 1917, uhusiano baina ya mwanadada Nadezhda na mzee baba Stalin ulianza kubadilika, na hatimaye walifunga ndoa mwaka 1919 bila sherehe yoyote ya kidini, kama ilivyokuwa kawaida kwa utamaduni wa Bolsheviks. Wakati huo Stalin alikuwa tayari mgane na baba wa mtoto mmoja.
Wanahistoria wa historia ya USSR hudai kuwa tofauti na wenza wengi wa viongozi wa Kisovyeti kipindi hicho, Nadezhda hakupenda kabsa maisha ya fahari. Alisoma, alifanya kazi, na hakutaka kuitwa “mke wa kiongozi.” Hata hivyo, aliishi pembeni ya mwanaume aliyekuwa na nguvu kubwa zaidi katika Umoja wa Kisovyeti—na pia aliyekuwa akizidi kuzama katika tabia ya ukatili na unywaji wa pombe.
Kwa nje, ndoa yao ilionekana kuwa ya kawaida ya kimapinduzi, lakini ndani yake kulikuwa na misukosuko mikubwa. Nadezhda alikuwa mwanamke anayejielewa, mwenye msimamo wa kisiasa, na aliyepinga tabia za kibabe kama beberu. Alikuwa pia na matatizo ya kiafya, yakiwemo maumivu makali ya kichwa na msongo wa mawazo, hali iliyozidisha mvutano katika ndoa yao.
Wanahistoria wengi, akiwemo Simon Sebag Montefiore katika kitabu chake Stalin: The Court of the Red Tsar, wanaeleza kuwa Stalin alikuwa mkali, mnyanyasaji wa maneno, na asiyejali hisia za mke wake haswa akiwa na viongozi wenzake, mwamba hakutaka kabsa kuonekana mdhaifu wa mahaba mbele ya makamanda wenzake.
Chanzo kikubwa cha migogoro kilikuwa tuhuma za usaliti, wanahistoria mbalimbali wameonesha kuwa kamanda Stalin alikuwa anapenda sana mademu. Na kama mke wa Stalin basi Nadezhda aliamini kwa 100% kuwa Stalin alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanawake wengi, akiwemo wake wa maafisa wa juu wa serikali na wafanyakazi wa Kremlin, mwamba alikuwa anapenda totoz hatari sana.
Ndani ya jumba la Kremlin kulikuwa na pisi moto moto na mwamba alikuwa akisambaza upendo. Mabishano yao yalikuwa ya mara kwa mara, hasa katika sherehe zilizohusisha pombe nyingi. Stalin, kwa mujibu wa baadhi ya wasomi hudai, alikuwa na tabia ya kumdharau Nadezhda hadharani, jambo lililomuudhi sana.
Usiku wa tarehe 7 Novemba 1932, wakati wa maadhimisho ya miaka 15 ya Mapinduzi ya Oktoba, ndipo tukio la mwisho lilianza. Baada ya gwaride kubwa lililofanyika pale Red Square, Stalin na mkewe walihudhuria chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kliment Voroshilov ambaye kwa wakati huo alikuwa ni miongoni mwa wanasiasa na afisa wa jeshi la Sovieti mwenye nguvu sana, kama ulipata kutazama filamu ya **The Right Stuff ya mwaka 1983 utaona maajabu ya huyu mwamba ambaye ni mmoja wa watu wenye nguvu kipindi hicho.
Katika maandimisho hayo kulikuwa na unywaji mkubwa wa pombe na vodka, na mabishano yakazuka tena. Stalin alipiga tungi kiasi akawa mwisho kabsa, sasa wakati akitoa hotuba nzito na kauli kali kuhusu maadui wa umoja wa USSR akikazia maneno “to eliminate all enemies of the states.”
Sasa Masikini Nadezhda, kwa ishara ya upinzani alikaa kimya, hakunyanyua glasi yake wakati ambao ukumbi wote ulinyanyua glasi juu kwa ishara ya kuunga mkono hotuba hiyo. Kitendo hicho kilimkera sana Stalin. Na kuonesha kuwa amepandwa na hasira kali, Stalin alimshushia mvua ya matusi na kejeli nyingi sana Mke wake, Nadezhda aliona ni vyema kuamua kuondoka kwa hasira na kurejea nyumbani kwake ndani ya Kremlin.
Picha linaanza! Asubuhi ya tarehe 9 Novemba 1932, Nadezhda Alliluyeva alipatikana amekufa katika chumba chake, akiwa amepigwa risasi moyoni kwa bastola ndogo aina ya Mauser. Silaha hiyo alikuwa amepewa hivi karibuni na kaka yake Pavel kwa madai ya kujilinda. Ripoti rasmi ilisema alikufa kwa ugonjwa wa appendicitis, lakini ukweli huu ulifichwa kwa nguvu kubwa.
Wafanyakazi wa Kremlin walihojiwa, wengine kufukuzwa kazi na wengine hata kukamatwa na kuwa chini ya ulinzi, huku hata watoto wake hawakuambiwa ukweli.
Katika kitabu chake Twenty Letters to a Friend, binti yao Svetlana Alliluyeva aliandika kwa uchungu kuhusu kifo cha mama yake, akionyesha mashaka makubwa juu ya simulizi la serikali huku akidai kuwa kuna jambo nyuma ya pazia katika kifo cha Mama yake. Wachapishaji wa mlengo wa kushoto, Harper wazee kushupalia mambo wakakidaka kitabu hicho na kukichapisha nakala za kutosha, Svetlana na wanahistoria wengine wanasema mazingira ya kifo hicho hayakuwa ya kawaida ukizingatia muda mchache kabla ya mauti kumkuta Nadezhda hakuwa kwenye mahusiano mazuri na mumewe.
Kwa nini serikali ifiche ukweli kama ilikuwa ni kujiua tu? Kwa nini hofu kubwa kiasi hicho?
Wanazuoni kama mkanada Bwana Robert Service na mwanahistoria mashuhuri ndani ya Urusi Prof Oleg Vitalyevich Khlevniuk wameeleza kuwa kifo cha Nadezhda kilimuathiri sana mzee baba Stalin, lakini pia kilionyesha upande wake wa giza. Mzee baba Prof Khlevniuk ni mtaalamu na mbobevu katika historia ya Umoja wa Soveti, hivyo kabla ya kusema kuwa anazungumza uongo basi ana mengi anayafahamu ndani ya Kremlin. Baadhi ya wachambuzi wanaamini kuwa huenda alisukumwa kisaikolojia hadi kujiua kutokana na manyanyaso.
Wapo wengine wanaenda mbali zaidi wakisema kuwa huenda aliuawa ili kunyamazisha upinzani wake wa ndani, huku watu kama Nora Seligman Favorov akiunga mkono kuwa ukosoaji wa wazi wa bi mdada ndio ulimchomesha, kwani Nadezhda alikuwa akimkosoa Stalin waziwazi kuhusu sera zake kali, hasa ukandamizaji na njaa iliyokuwa ikiua mamilioni ya wasovieti wakati huo.
Baadhi ya watu ndani ya Kremlin walidai kumsikia Mwamba akisema kuwa Mpaka kufikia **Nadezhda kuamua kujipiga risasi basi ni moja ya usaliti mkubwa sana kuwahi kutokea kwake. Na mpaka Stalin anafariki hakuwahi kwenda kutembelea kaburi la marehemu mke wake.
Hadi leo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaomthibitisha Stalin kumuua mkewe. Lakini mazingira ya siri, uongo wa serikali, na tabia za Stalin vinaacha maswali mazito yasiyo na majibu. Kama alivyoandika Montefiore, “kifo cha Nadezhda kilikuwa jeraha la ndani katika maisha ya Stalin, lakini pia ni dirisha la kutazama ukatili wa utawala wake.”
Kifo cha Nadezhda Alliluyeva kinabaki kuwa moja ya mafumbo makubwa katika historia ya karne ya 20. Je, alikuwa mhanga wa ndoa yenye sumu? Je, alijitoa uhai kwa kukata tamaa? Au je, alikuwa mhanga wa mfumo alioulea tangu utotoni? Jibu kamili labaki limezikwa pamoja naye katika makaburi ya Novodevichy, huku kivuli cha Stalin kikiendelea kulizunguka hadi leo.