Kifo cha pesa Beach Kidimbwi

Kifo cha pesa Beach Kidimbwi

mtaani kinywaji kinauzwa kati ya TZS 40,000 - 80,000 kule kinauzwa mara tatu ya bei, hivi ni kwamba vinywaji vinakuwa na huduma nyinginezooo ama ni icho kimiminika kilichoko kwa chupa tuu
Ushaambiwa kinasindikizwa na shazi la warembo....kwani hao mshahara wao si ndo unatoka kwenye hiyo bei waliyoi - triple
 
Wewe hiyo milioni unaitafuta ili ukanunue bati uweke ndani usuibirie mwakani bei elekezi ya ufuta na mbaazi itakuwaje,mwenzio hiyo m ananunua Hennessy moja Tu hapo kidimbwi!! Tafuta hela
Na pengine huyo anayenunuwa whisky kwa 1 milioni si ajabu hata kiwanja hana..

Dunia uwanja wa fujo,,usifuate mkumbo.
 
Jumapili fulani nilikuwa na rafiki yangu mmoja aliyepiga mshindo wa hela ya mahali tumepozi mtaani. Jamaa akaniambia yooh Satoh wacha tukatembee mahali mida ya jioni, nikamuuliza wapi anataka twende maana mimi ni mwenyeji hapa mjini, akajibu twenzetu kidimbwi.

Nilisita maana sikutegemea kabisa kama angechagua kwenda huko mahali ila nikaona it's ok wacha tu twende, kwanza napasikia tu sijawahi kufika kwa kweli. Jioni ikafika tukajiandaa kisha haoo uelekeo wa mikocheni, roundabout ya Clouds tukamimina boda la kule chini Kawe Beach, Times FM, Mbezi beach then punde Kidimbwi hii hapa..tukafika.

TuLIfika mida ya saa 11, ni pa kawaida tu kwa kweli tofauti na jinsi panavyokuzwa. Basi ikafika usiku pakawa ni sehemu tofauti kabisa na jinsi palivyokuwa jioni wakati tumefika..Palikuwa pamechangamka sana, mataa ya rangirangi na watoto wakali kibaoo.

Niseme Tu ukweli kuna Wanawake warembo, warembo sana. Muda wote shingo haitulii kwa kuangalia uumbaji wa MUNGU, watoto wakali hadi unajiuliza mbona kam kuna wadada walipendelewa siku wanaumbwa!! (Ukitaka kupata kipimo sahihi kama una demu mkali au umeingia cha kike basi nenda nae Kidimbwi, ingawa ili kuepuka aibu ndogondogo ni heri ukaenda mwenyewe tu maana anaweza kukuona malaya sana kwa jinsi utakavyopata shida kuibiaibia kutazama watoto wakali)

Basi bwana 'mwanangu' ndy bosi na mimi nilikuwa kama 'chawa' wake usiku ule. malaya shobo kibao tulipokaa, mwonekano wa kishua ukiwadanganya kumbe muhuni mfukoni balance niliyokuwa nayo ni pesa ya kuamkia mihogo kwa mama Amina na supu ya kongoro tu. Jamaa ndiyo alikuwa tagi ubavu, ingawa sinaga zile swags za kushobokea pesa za watu(masikini jeuri) ila nilikuwa mtulivu sn huku tukila vitu vyetu

Mida km ya saa 4 ndy Kwanza pakawa km show imeanza ,nikaona kitu kilichonishangaza Sana ambacho kilinipelekea kukodoa macho kwa kustaajabu.Kuna mdada amebeba sahani alafu ndani kuna chupa moja ya kinywaji,pembeni kuna wadada kama wanne hivi wanakatika na kucheza vizuri sana huku wanaelekea meza fulani ambayo ipo mbali kidogo na tulipo.

Nikamcheki dada wa karibu aliyekuwa ananizongazonga akidhani Mimi ni wa kishua kumbe apecha alolo nikamuuliza 'hey lady,hawa warembo nini hiki wanafanya'? Akanijibu yule dada aliyebeba ule 'mbapa' ni kinywaji cha milioni moja na nusu(1.5mil) na anapelekewa 'Mnene' mmoja hivi kipande kile..aloo [emoji848] ..1.5mil ni kinywaji tu si uharibifu wa hela huu!!? Umasikini mbaya sana asee!!!

Jirani yetu pale ambaye alionekana ni mzoefu wa hili chimbo akadakia "mjomba mbona hiyo ni ishu ya kawaida sn hapa".

Akaniambia unakiona kile chumba pale (huku akionyesha kidole), nikajibu yeah nakiona,akasema Mzee Baba pale kuingia sharti uwe na milioni 1.. Yaani Haijalishi utakaa dakika moja au saa zima,pale unaadikiwa deposit ya 1m kisha unaagiza unachotaka ktk menu zilizoorodheshwa utumie,Yani wewe Tu unatumiaje shauri yako!! Nikazidi kujiona masikini na kujidharau (kimoyomoyo nikasema milioni moja si napata kiwanja vikindu ndani ndani huko[emoji28] hapa inakatika dakika kadhaa Tu si ufala huu,huku namkumbuka Mzee wa kinywaji cha 1.5m ).

Haikupita muda, nawaona wadada wengine wanakatika viuno wakitembea na mwendo wa madaha huku wanasindikizwa na nyimbo za majigambo kutoka Kwa DJ wanaelekea meza nyingine.Nikapenyezewa taarifa kuna mwamba mwingine amefanya km jamaa wa mwanzo amepelekewa kinywaji cha 1m..Safari hii nilikuwa nimeshazoea,si unajua kushangaa mara moja tu [emoji28].

Kuna kitu nilijifunza ule usiku;kwa watu waliofikia kilele cha Uhuru wa kifedha (financial freedom) kwao kutumia hela siyo yoyote bila kuuliza uliza wala kukagua wallet siyo tatizo kbs.Ule usiku nilijiapiza kutafuta pesa Kwa bidii zote.

Kwa hakika usiku ule nilishuhudia watu wakiteketeza pesa vibaya mno.Kwa kweli ulikuwa ni "usiku wa kifo cha pesa".

Siku nikipata pesa nitarudi tena kidimbwi!!
ishia hapo hapo mkuu, ngoja nami nikawasimulie kijiweni
 
Back
Top Bottom