Kifo cha pesa Beach Kidimbwi

Kifo cha pesa Beach Kidimbwi

Yaani tajirj aende kidimbwi...acha ufala. Tajiri wannafanya yale wanayofanya waarabu kaka....kwenye boti lako unawakaribisha warembo unawapa mbwa wako wagegegdane nao huku wee unagonga monde yako tartibu
Nikosa kufichua siri za kina sa100 na rostam na gsm hapa ...
 
Kuna kijana mmoja wa forex anaitwa Moneyhollic huwa anakuja pale kidimbwi na chawa wake wakina Dullvani,Mose Iyobo........Dogo na gang yake anaacha pale kidimbwi zaidi ya 5 million per one night
Kweli sio mchezo
 
Halafu zile mioto wanapiga na kamziki wakati mwingine wanawatisha tu wasiojua. Wanabeba Hennessy 10 na Moet 10 wakifika wanaacha Hennesy chupa mbili na Moet mbili nyingine wanarudisha.
Na sometimes pia hawalipi wanasign tu bill mpaka wanadaiwa kwa aibu. Ukiacha wenye pesa za ukweli wengi wao wanafanyaga zile mbwembwe kuvutia slay queens na kuwa na majina mjini.
Dar kwenye sehemu za starehe kuna siri nyingi sana.
Hao wengi wanapesa za mawazo,madalali wa nyumba na magari ndio wapiga kelele,ila maisha yao mwisho huwa mabaya
 
Mm bado nailaumu serekali kwa kutofatilia Bei hzo na kod inayolipwa na hao kina kidimbwi utakuta jamaa hawa kwa mwaka wamekadiriwa milion tano hi siyo sawaa kbsa kinywaji Cha milion moja alfu uje utuambie kod Kia's gani imeingia serekali nakuambia haitazid milion tano
Acha akili ya kimasikini wewe. Umeambiwa wanalipa kwa EFD machine, kwa hiyo kodi inalipwa IPASAVYO.
 
Nimependa hapo kuhusu “financial freedom”...tutafute hela!! Ila ajabu matajiri huwaoni wakifanya hayo wala huwakuti kidimbwi
Wanaoenda Kidimbwi wana hela ya supu tu mkuu, wenye hela wanaenda kwenye mahoteli kule zanzibar au Serengeti, kulala tu kwa siku USD 10,000 narudia tena USD sio hii pesa yetu ya madafu(kwa sauti ya mzee wa Msoga)
 
Acha kabisa ila bwana bwana kuywa pombe ya million kumi pata unga first grade lakini mwisho wa siku utaishia kwenye mbususu tuu. Hakuna starehe duniani isiyo ishia na kugegegeda mbususu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Jumapili fulani nilikuwa na rafiki yangu mmoja aliyepiga mshindo wa hela ya mahali tumepozi mtaani. Jamaa akaniambia yooh Satoh wacha tukatembee mahali mida ya jioni, nikamuuliza wapi anataka twende maana mimi ni mwenyeji hapa mjini, akajibu twenzetu kidimbwi.

Nilisita maana sikutegemea kabisa kama angechagua kwenda huko mahali ila nikaona it's ok wacha tu twende, kwanza napasikia tu sijawahi kufika kwa kweli. Jioni ikafika tukajiandaa kisha haoo uelekeo wa mikocheni, roundabout ya Clouds tukamimina boda la kule chini Kawe Beach, Times FM, Mbezi beach then punde Kidimbwi hii hapa..tukafika.

TuLIfika mida ya saa 11, ni pa kawaida tu kwa kweli tofauti na jinsi panavyokuzwa. Basi ikafika usiku pakawa ni sehemu tofauti kabisa na jinsi palivyokuwa jioni wakati tumefika..Palikuwa pamechangamka sana, mataa ya rangirangi na watoto wakali kibaoo.

Niseme Tu ukweli kuna Wanawake warembo, warembo sana. Muda wote shingo haitulii kwa kuangalia uumbaji wa MUNGU, watoto wakali hadi unajiuliza mbona kam kuna wadada walipendelewa siku wanaumbwa!! (Ukitaka kupata kipimo sahihi kama una demu mkali au umeingia cha kike basi nenda nae Kidimbwi, ingawa ili kuepuka aibu ndogondogo ni heri ukaenda mwenyewe tu maana anaweza kukuona malaya sana kwa jinsi utakavyopata shida kuibiaibia kutazama watoto wakali)

Basi bwana 'mwanangu' ndy bosi na mimi nilikuwa kama 'chawa' wake usiku ule. malaya shobo kibao tulipokaa, mwonekano wa kishua ukiwadanganya kumbe muhuni mfukoni balance niliyokuwa nayo ni pesa ya kuamkia mihogo kwa mama Amina na supu ya kongoro tu. Jamaa ndiyo alikuwa tagi ubavu, ingawa sinaga zile swags za kushobokea pesa za watu(masikini jeuri) ila nilikuwa mtulivu sn huku tukila vitu vyetu

Mida km ya saa 4 ndy Kwanza pakawa km show imeanza ,nikaona kitu kilichonishangaza Sana ambacho kilinipelekea kukodoa macho kwa kustaajabu.Kuna mdada amebeba sahani alafu ndani kuna chupa moja ya kinywaji,pembeni kuna wadada kama wanne hivi wanakatika na kucheza vizuri sana huku wanaelekea meza fulani ambayo ipo mbali kidogo na tulipo.

Nikamcheki dada wa karibu aliyekuwa ananizongazonga akidhani Mimi ni wa kishua kumbe apecha alolo nikamuuliza 'hey lady,hawa warembo nini hiki wanafanya'? Akanijibu yule dada aliyebeba ule 'mbapa' ni kinywaji cha milioni moja na nusu(1.5mil) na anapelekewa 'Mnene' mmoja hivi kipande kile..aloo [emoji848] ..1.5mil ni kinywaji tu si uharibifu wa hela huu!!? Umasikini mbaya sana asee!!!

Jirani yetu pale ambaye alionekana ni mzoefu wa hili chimbo akadakia "mjomba mbona hiyo ni ishu ya kawaida sn hapa".

Akaniambia unakiona kile chumba pale (huku akionyesha kidole), nikajibu yeah nakiona,akasema Mzee Baba pale kuingia sharti uwe na milioni 1.. Yaani Haijalishi utakaa dakika moja au saa zima,pale unaadikiwa deposit ya 1m kisha unaagiza unachotaka ktk menu zilizoorodheshwa utumie,Yani wewe Tu unatumiaje shauri yako!! Nikazidi kujiona masikini na kujidharau (kimoyomoyo nikasema milioni moja si napata kiwanja vikindu ndani ndani huko[emoji28] hapa inakatika dakika kadhaa Tu si ufala huu,huku namkumbuka Mzee wa kinywaji cha 1.5m ).

Haikupita muda, nawaona wadada wengine wanakatika viuno wakitembea na mwendo wa madaha huku wanasindikizwa na nyimbo za majigambo kutoka Kwa DJ wanaelekea meza nyingine.Nikapenyezewa taarifa kuna mwamba mwingine amefanya km jamaa wa mwanzo amepelekewa kinywaji cha 1m..Safari hii nilikuwa nimeshazoea,si unajua kushangaa mara moja tu [emoji28].

Kuna kitu nilijifunza ule usiku;kwa watu waliofikia kilele cha Uhuru wa kifedha (financial freedom) kwao kutumia hela siyo yoyote bila kuuliza uliza wala kukagua wallet siyo tatizo kbs.Ule usiku nilijiapiza kutafuta pesa Kwa bidii zote.

Kwa hakika usiku ule nilishuhudia watu wakiteketeza pesa vibaya mno.Kwa kweli ulikuwa ni "usiku wa kifo cha pesa".

Siku nikipata pesa nitarudi tena kidimbwi!!
Lipia tangazo
 
Maccm ndiyo yanachambia pesa zetu watz huko vidimbwi kwa kuagiza vinywaji vya mamilioni ....kweli nimekubali kuwa ccm ni maviii
Vip hukumwona Rostam azizi huko vidimbwi
Aisee Rostam ?....analia bia kwake masaki
 
Na pia matajiri wakueleweka huwezi kumuita Kidimbwi mkaongelea mambo ya msingi.

Na sio matajiri tu, hata watu wenye ajira zao serious huwezi mpeleka kidimbwi.

kidimbwi ni sehemu ya starehe sio sehemu ya kufanyia maongezi.... Pale unakwenda kufurahisha nafsi na ubongo.....ukiangalia angalia matako ya mabinti, ukapewa zile huduma maarufu kutoka kwa binti zetu wale...

Ukitaka maongezi na business meeting zipo sehemu zake...
 
Daaah mkuu me nisiwe mwongo mara moja moja huwa naenda ku-double haha...kwanini hawakutaki ?
Kuna mwanangu aliliwa pesa nyingi mle ndani sisi tukawa tunagonga mitungi sasa kuna mchina alilewa akaangusha wallet toilet wahuni tukapita nayo kwenda kulia bata bagamoyo,

Ule msako tuliopigwa sio wa nchi hii mkuu
 
Back
Top Bottom