Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Picha: Gari lililosababisha kifo cha Hayati Sokoine
Katika hali ya kushangaza, watoto na baadhi ya ndugu wa aliekuwa waziri mkuu wa Tanzania, Hayati Sokoine, wanataka uchunguzi ufanyike wa mwili wa marehemu ili kubaini kama ni kweli kifo chake kilitokana na ajali au laa.
Uamuzu huo ulofikiwa mara baada ya mwili wa Hayati Sokoine kuzikwa upya mwishoni mwa mwaka jana baada ya kabuli la awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi katika milima ya Oldonyo Lengai.
Taarifa zinasema wanafamilia hao wanakusudia kuomba kibali serikalini ili wataalamu waufanyie uchunguzi mwili huo kubaini chanzo cha kifo chake.
Kulingana na taarifa za gazeti la Tanzanian Daima la tarehe 07/04/2013,ambapo habari hii imeelezwa kwa kirefu zinasema uamuzi huo ni kutokana na hofu kuwa huenda kifo chake kilitokana na hujuma za wale waliokuwa wakimpinga hayati Sokoine katika vita vyake vya kupambana na wahujumu uchumii wakati huo.
Imeelezwa mh.Lowassa ni miongoni mwa watu waliohudhuria mazishi hayo yalifanyika saa saba za usiku mwishoni mwa mwaka jana.
CHANZO:TANZANIA DAIMA ONLINE.