Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)


Bahati mbaya wengi wanaongozwa na ushabiki tu juu ya kanumba! Anyways.....ngoja tusubiri report zaidi.
 
Bahati mbaya wengi wanaongozwa na ushabiki tu juu ya kanumba! Anyways.....ngoja tusubiri report zaidi.
Si mzazi alitoa idhini. Alisema anaufahamu uhusiano wao na mama kanumba yeye ni dada yake.
 
mimi sikuwahi kuwa shabiki wa the Great but sioni kama ana kosa lolote hapo,kila mtu anajua ni jinsi gani ukiwa star bongo wanawake wanavyosumbua kwanza hakuanzia kwa K alikuwa nao wengi na kuna cku alikuwa na mdogo wake wa kiume mdogo pmj na rafiki yake sehemu fulani namimi nilikuwepo meza ya jirani na wao story ni wanaume mwanzo mwisho huyu yule. Ukweli utajulikana na km K alikuwa anambaka kutokana na umri alioukana kabla bac kila mwanaume aliyempitia Lizy ashtakiwe nyie c mnataka haki itendeke?
 

Mkuu ni kweli kabisa usemayo,mbona mzazi huyu kachelewa.
 
kwani ukitongozwa.lazima ukubali?kama aliona umri wake mdogo,angekataa.na nyumba anajengewa,anaemjengea anamjua mwenyewe.tabia ya huyu lulu tu,haikuwa nzuri.kweli kanumba na yeye ana makosa,ila na huyu mtoto ameanza mambo ya kikubwa wakati yu mdogo.nina uhakika sio kanumba peke yake aliekuwa nae kimapenzi.
 

[h=2]Babake Kanumba atoa siri nzito Dar[/h]




Yawekwa hadharani nyumbani kwake Dar
Mapya yaibuliwa kisa cha kutomzika mwanae




Marehemu Steven Kanumba (kushoto) wakati wa uhai wake akiwa na baba yake mzazi Charles Kanumba nyumbani kwao mjini Shinyanga.


Baba mzazi wa aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini, Marehemu Steven Kanumba, amevunja ukimya kwa kuibuka na kueleza sababu iliyomzuia kuhudhuria mazishi ya mwanaye.

Marehemu Kanumba aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Aprili 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam, alizikwa Jumanne wiki hii bila baba yake mzazi, Charles Kanumba, kuwepo. Hali hiyo iliibua mjadala miongoni mwa watu mbalimbali.

Mzazi huyo jana alieleza sababu iliyomfanya ashindwe kutoka mkoani Shinyanga kwenda Dar es Salaam ambako mazishi ya mwanaye yalifanyika na kuhudhuriwa na halaiki ya watu wakiwemo mashabiki wake, wasanii wenzake, viongozi wa serikali, makundi mbalimbali na wananchi kwa ujumla.

Nyumbani kwa Marehemu Kanumba jana eneo la Sinza Vatican, kulivuta waandishi wa habari na wapiga picha ambao walialikwa kusikiliza barua iliyokuwa imeandikwa na Mzee Charles Kanumba.

Akisoma barua hiyo iliyowasilishwa na wawakilishi wake watatu, mmoja wa wawakilishi hao, Chrisant Msipi, alisema kuwa baba mzazi wa marehemu hakufika kwenye mazishi hayo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na malaria.

Katika barua hiyo, baba wa marehemu amenukuliwa akieleza kuwa, alikuwa anajisikia vibaya na alipokwenda katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kupima afya yake alikutwa ana malaria 15 na kuandikiwa sindano za saa.

Kupitia barua hiyo, aliongeza kuwa, ilipofika saa 12:00 jioni alizidiwa na alipopimwa kwa mara ya pili kuangaliwa shinikizo la damu (BP) alikutwa ana 180 kwa 140, kitu ambacho alisema alitakiwa kupumzika zaidi hospitalini chini ya uangalizi wa madaktari.

Barua hiyo iliendelea kueleza kuwa, hadi anawatuma wajumbe hao kwenda Dar es Salaam kupeleka ujumbe huo alikuwa anajisikia vibaya na hali ya afya yake haikuwa nzuri.

Alieleza kuwa kutokana na hali hiyo, Watanzania wasimfikirie vibaya kwa kutofika katika msiba na mazishi ya mtoto wake.

Aliongeza kuwa, taarifa zilizozagaa zikidai kuwa hakuhudhuria mazishi ya mtoto wake kutokana na kutokuelewana si za kweli, ila alitamani sana kuwepo lakini afya yake haikumruhusu.

Mbali na Msipi aliyekuwa kiongozi wa msafara huo, ujumbe huo pia uliwashirikisha Michael Kanumba na Mjanaeli Kanumba.

Naye Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi, alisema kuwa kwa sasa hakuna kazi yoyote ya marehemu Kanumba itakayotolewa bila idhini ya familia yake na TAFF. (Habari zaidi soma ukurasa wa 24)

Kwa upande wake, Mama wa Marehemu, Frolence Anjelo, alisema anawashangaa watu kujipatia kipato pasipo kupata ruhusa kutoka kwa familia ya marehemu Kanumba.

Aidha, Anjelo alitoa salamu za shukrani kwa Watanzania wote walioshiriki katika mazishi ya mtoto wake tangu kifo hadi siku ya mazishi.

Marehemu Kanumba alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi Aprili 7, mwaka huu, baada ya kudaiwa kutokea ugomvi kati yake na msanii mwezake anayedaiwa kuwa mpenzi wake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ (18).

Lulu juzi alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya mauaji.

Hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiza kesi za mauaji na kesi hiyo itatajwa Aprili 23, mwaka huu.

Ingawa Lulu hakutakiwa kujibu hadi upelelezi wa kesi hiyo utakapokamilika na kuhamishwiwa mahakama kuu, alidai kuwa hana miaka 18 kama ilivyodiwa kwenye hati ya mashitaka ila umri wake ni miaka 17.





CHANZO: NIPASHE
 

Niko nyuma yako mkuu.
 

naamin ukiona mtu anamwaga haja kubwa hadharani nawe hutomuiga siyo! Hata kama wengine walikuwa wanatembea na hako katoto, bado hai halalishi! Kwa status yake marehemu alitakiwa awe kioo vijana waige kutoka kwake! Na sio kwenda kurubuni vitoto vidogo!
 


Natumaini mwalimu wake Halima Mdee ataiprinti ampelekee atakapokwenda kwenye kipindi!
 
Jamani kwa nini tusiseme walikuwa ktk kufundihsna the great alikuwa mwalim wake na mlinzi wake na ndio maana alipoona anapigiwa sim na
wazee wapenda vitoto akawa anataka kumnyoosha!
 
Naamini kati ya watanzania wenye matatizo ya akili huyu mzee anayejiita baba yake lulu ni kiongozi wao..kifupi mzee ni chizii.

1- alikuwa wapi wakati mwanae anadhalilisha familia yake kwenye magazeti kwa matukio ya aibu kiasi wengi tuliamini hana wazazi?

2- alikuwa wapi kumuachia mwane afanye tafrija kubwa ya kutimiza miaka 18 hapo mwaka jana ilihali akijua kuwa mwanae ana miaka 16 tu?

3- alikuwa wapi kuangalia mwanae anaendesha gari la kwake mwenyewe wakati anajua huyo ni mtoto na hajatimiza umri wa miaka 18 inayomruhusu kuajiriwa na kulipwa pesa aweze kununua gari kwa pesa yake?

4- alikuwa wapi anapomwona mwanaye kwenye tv akitangaza kuwa kafikisha miaka 18 na anajenga nyumba inayokaribia kuisha huko kimara?

5- alikuwa wapi anaposikia mwanae anaenda club na analewa pombe chakari plus scandal za ngono wakati yupo firm 2-4?

Nadhani haki ya kwanza anayotakiwa kuiona inatendeka ni yeye kuhukumiwa kwa poor parenting aliyomlea mwanae kiasi cha kuishia "kufunzwa na ulimwengu"...naomba haki itendeke na ianze na huyu mzee wa kichaga asiyejua kulea kazi kulewa...what a irresponsible stipidy n poor daddy he is???
 
baba yake lulu alikuwa wapi sik zote kumkanya bintie!! leo anaibuka anasema binti yake ana umri wa miaka 16 mbona lulu alipofanya sherehe ya kutimiza miaka 18 hakusema lolote alikaa kimya, lulu alipohojiwa na zamaradi na salama hakusema lolote alikaa kimya??? leo hii anaibuka anasema mwnae ana miaka16 tuamini lipi miaka 16 ya baba, 17 ya lulu mahakamani, miaka 18 ya mahojiano ya tv zetu na ile party ??

wanazidi kujichanganya tu ingekuwa mm ningekaa kimya nisinge ongea lolote, kwani kwa mtazamo wangu wanajaribu kuficha kitu bila ya kuwa na mawasiliano mazuri mwisho wa siku wanakorogana wao kwa wao, watulie wakae kimya wajipange vizuri haya ya kila mtu kuzungumza lake litawatokea nyongo
 
sijamtetea kanumba,ndio maana nilisema,na kanumba nae ana makosa.ni bora haki tu itendeke,kwa mujibu wa sheria na sio kwa sababu ya kuonewa huruma
 


KABISA MKUU HUYU MZEE AMEKURUPUKA NA ALIYEMKURUPUSHA HAKUMSAHURI VIZURI AKAJIPANGE UPYA??

Lulu analeseni ya gari aliipataje akiwa na umri wa miaka 15 or 16 sheria inasemaje hapa?? yaania huyu mzee ataibua mambo mengi ambayao hatukustaili kuyajua, hili la kuendesha gari ni tosha kuwa mwanae ameidanganya serikali ama wamehonga ili apate leseni ikiwa hakustahili kuwa na leseni ya kuendeshea gari, ni kosa jingine hilo yaani kosa juu ya kosa. Au anataka kusema vijana wa IGP Mwema na Kova hawako makini na kazi yao wanatoa leseni za magari kwa kuangalia jina na sura???

Je passport yake lulu inaonyesha amezaliwa lini??
 
Natumaini mwalimu wake Halima Mdee ataiprinti ampelekee atakapokwenda kwenye kipindi!


Mdee upo hapo?

My Take:
Kama kuna mtu ana dhamira ya kweli ya kumsaidia huyu mtoto basi isiishie katika kumsaidia aepukane na songombingo la kifungo tu, bali amsaidie pia kujitambua na kuondokana na ulimbukeni wa ustaa wa kibongo na kuishi maisha ya stara. Vinginevyo tunabaki kule kule kwenye kumtumia mtoto huyu kwa faida binafsi za kujitafutia umaarufu. Already ameshatumika vibaya mara nyingi huko nyuma and let nobody else take undue advantage of her situation for any selfish benefits any more.
 
Watu wanaposema "haki itendeke" wanaelewa wanachomaanisha? Je, mahakama ikiridhika kuwa Lulu aliua kwa kukusudia na imhukumu kifo?

itakuwa imetenda haki pia, kwani sheria ni msumeno inakata kotekote tuache ifanye kazi yake, hao wanadai lulu hanakosa,kanumba ana makosa wote hatujui ukweli wenyewe anaujua lulu peke yake kwani yy ndio aliebaki na mungu, akitudanganya sawa akisema ukweli sawa pia
 
Thread nyingine! :nono::nono: tittle kama watu wanafanya kazi kwa Shigongo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…