Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Tuesday, April 10, 2012

KILICHOMUUA KANUMBA HIKI HAPA


MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza. Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.
"Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion," alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) "Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka" alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
"Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji."
"Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki."
Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Alisema sehemu ya maini na majimaji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.
Baba mzazi azungumza Baba mzazi wa mwigizaji huyo, Charles Musekwa Kanumba alisema kwamba alipata taarifa za kifo cha mwanawe Jumamosi saa 10:00 alfajiri baada ya kupigiwa simu na dada wa marehemu, Sara Kanumba. "Sara aliniuliza: ‘Una taarifa yoyote kuhusu mwanao Kanumba?' Nikamjibu kuwa sina taarifa yoyote, ndipo aliponieleza habari za kifo hicho. Aliniambia Kanumba hatupo naye tena amefariki kwa kuanguka, amekorofishana na mpenzi wake." alisema taarifa hizo zilimsababisha aishiwe nguvu kwa kuwa kilikuwa kifo cha ghafla… "Basi kuanzia hapo, nilianza kupigiwa simu za kupewa pole, ndipo nilipoamini kumbe mwanangu amefariki."
Akizungumzia kuchelewa kufika msibani, alisema kumetokana na tatizo la mawasiliano. Awali, alikuwa amepanga mtoto wake Kanumba akazikiwe Mwanza kwa babu yake ndiyo maana hakufika mapema msibani. "Nilikuwa nimepanga apitishwe hapa kwangu Shinyanga aagwe, halafu tumpeleke Mwanza kwa babu yake kumzika huko lakini alipokuja mama yake alinishauri kuwa huko kutakuwa na nafasi ndogo kwa sababu watu ni wengi pia alikuwa na marafiki wengi, wengine wa kutoka nje ya nchi kwa hiyo alinishawishi na tukakubaliana kumzika Dar es Salaam," alisema.
Pia alikanusha uvumi kuwa hajafika msibani kwa kuwa walikuwa na ugomvi na marehemu akisema walishamaliza tofauti zao. Alisema anatarajia kufika leo usiku tayari kushiriki mazishi hayo.
Wabunge kilio Jana, baadhi ya wabunge waliofika nyumbani kwa marehemu Kanumba waliangua vilio wakati walipotoa salamu zao za rambirambi.

Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata hakuzungumza na badala yake aliimba kipande cha wimbo uliozungumzia kifo na maneno ya wimbo huo yalionekana kuwagusa wafiwa na kusababisha vilio kuanza upya huku baadhi wakipoteza fahamu.
Mbunge mwingine, Neema Mwinyimgaya aliongeza majonzi masibani hapo alipounganisha msiba huo na wa mama yake… "Mama yangu amefariki miezi mitatu iliyopita, huko uliko mama, nakuomba umpokee kijana mwenzetu," alisema mbunge huyo na kushindwa kuendelea.
Wabunge wengine waliohudhuria msiba huo ni Ismail Aden Rage (Tabora Mjini), Aboud Juma (Kibaha Vijijini), Mussa Azan Zungu (Ilala), Abbas Mtemvu (Temeke), Peter Serukamba (Kigoma Mjini) na Ritha Kabati (Viti Maalumu).
Kova na mchango wa Kanumba Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema anakumbuka mchango wa Kanumba katika kuzuia uhalifu jijini.
"Tulishirikiana naye pamoja na wasanii wengine kuandaa bonanza maalumu ambalo lilidhamiria kukabiliana na uhalifu hapa jijini na kwa kweli mchakato ule ulifanikiwa kwani uhalifu ulipungua kwa kiasi kikubwa" alisema Kova.
"Kifo chake kimekuwa cha ghafla mno na nafikiri kujiweka tayari (kiimani) ni jambo ambalo kila mmoja anatakiwa kuwa makini nalo katika maisha yake," alisema Kova.
Ratiba ya mazishi
2:30 - Msafara kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia Barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi hadi Viwanja vya Leaders Club.
3:30 - Misa ya kumuombea na salamu mbalimbali.
6:00 – Kuaga
9:00 - Kuelekea Makaburi ya Kinondoni

 
wanajaribu kumsafisha huyo dogo! mtikisiko wa ubongo unasababishwa nanini mbona hawasemi?
 
kumbukeni Kanumba alitoka bafuni yawezekana miguu yake ikikuwa na majimaji na wakati wa purukushani labda Lulu alimsukuma kidogo akakosa balance akateleza na kuangukia uchogo.

Na ukichanganya na kilevi.. Huwezi jua..

Ila crime scene huwa inakuwa photographed. Kama kuna nondo,au nini itaonekana na itachekiwa alama za vidole kama vinarelate na yeyote..

Ila mi bado nauliza kwa hao wanaomuita binti huyu muuaji,wanadhani motive yake hasa ni nini?
 
Alikuwa anasali AICT.Aliwahi na kuimba katika Neema gospel AICT chang'ombe.Mungu amlaze mahali pema peponi Ameni
Kweli kabisa mkuu, hata sasa nasikiliza clouds kwaya aliyokuwa anaimbia hapo zamani ndo inaimba.
 
wanajaribu kumsafisha huyo dogo! mtikisiko wa ubongo unasababishwa nanini mbona hawasemi?

Ripoti ya daktari imesema "mdondoko","au "kupigwa na kitu kizito tena butu " yaani inatakiwa iwe a heavy blow...

Kwa akili ya kawaida kabisa sioni Lulu anavyohusika na kifo kile ....

Hata motive siioni..!
 
Nimekuja kugundua kuwa,jamvini humu ni watu waachache sana wenye weledi na mambo ya kichunguzi..
 
Safi sana nafurahi sana kanumba anapata maziko anayostaili RIP our Tanzanian Ramsey.
 
Lulu kasafishwa kwa 100% kama taarifa ndio hii......
Nilikuwa namuonea huruma ..ila kashikashi aliyo kwisha ipata ni adhabu tosha kujitia utu uzima

kasafishwaje wakati haijasemwa huo mtikisiko kwa Kanumba umesababishwa na nini? Kuna mambo hayajawekwa wazi bado nadhani yaliyobaki ni ya kipolisi zaidi kwa upelelezi..
 
Jamani mbona mmeanza kuhukumu kabla nyie hamjahukumiwa..
Marehemu kishapumzika zake ni mungu pekee anayetoa huku yake ..
Kilichobaki ni sisi kuangalia matendo yetu kama yanampendeza mungu
Nani kakwambia the great kapumzika?
Nipe andiko kwamba mtu akifa kapumzika!
 
Steven Kanumba kama alivyofahamika, kwa sasa ni marehemu.

Kifo chake naweza kusema kuwa kimewagusa watu weengi ukizingatia alikuwa ktk fani ya maigizo, na ni mmoja kati ya waigizaji ktk runinga anayetajwa kuwa maarufu sana hapa nchini na nchi za jirani.

Hakuwa msanii mkongwe, lakini amekuwa na nyota ya kupendwa na kuvuta hisia za wengi kwa kipindi hiki kifupi alichojiunga ktk fani hiyo.

Kifo chake pia kimekuwa faraja kwa vyombo vya habari hasa Televisheni na Redio ambazo hazina vipindi vya kueleweka.
Pia hata Magazeti ambayo hayana ya maana ya kuandika, nayo pia yamejaza picha za marehemu na udaku wa hapa na pale.

Kifo cha kijana huyu pia kimeita hata viongozi wa ngazi mbalimbali za kisiasa hapa nchini.
kimemuita mpaka Rais wa nchi na kumlazimu aahirishe safari yake ambayo ilikuwa na manufaa kwa taifa na kuja kujumuika ktk msiba.

Kila kona ya wasio na kazi au wasio na ya maana ya kufanya basi habari imekuwa ni ya kifo cha Kanumba, kwenye basi kanumba, mahospitalini kanumba, stendi kanumba, bar Kanumba, wakristo nao hawaelezi tena kufa na kufufuka kwa Yesu kristo bali nao wameshikwa na kifo cha Kanumba, kila kona ni Kanumba, Kanumba, Kanumba.

wengine wamejaribu kukurupuka na kusema msiba huu ni wa kitaifa.
Wengine wamekuja na wazo eti mwili wa Kanumba ukaagwe ktk uwanja wa Taifa.
Wengine tumewasikia wakikaririwa wakisema kwa nini hakufa Ray badala ya Kanumba?
...Stupid

Binafsi najaribu kuuangalia uwezo wa Kanumba kikazi.
Ni wazi kuwa Kanumba alikuwa ni msanii wa kawaida tu ila nyota yake pamoja na yale aliyowahi kukaririwa Baba yake akiyasema ndiyo yamefanya kijana huyu aonekane ni mkali zaidi hapa nchini.

Kanumba movie zake nyingi ni za kawaida na tumeshashuhudia movie zake nyingi zikikosolewa sokoni na wapenzi wa sanaa hiyo.
Haya ni lazima yasemwe hata kama katangulia mbele ya haki.


kwa miezi ya karibuni uwezo wa uigizaji wa hawa mahasimu wawili yaani Ray na Kanumba umepata ushindani mkubwa toka kwa mtu ambaye anaaminika kuwa yuko ktk chati ya juu kwa sasa, akifahamika kama JB ama Jacob Steven.
Je nini kimefanya Ray na Kanumba waporomoke ktk chati ile na kumpisha bila hiana JB?

binafsi kuna mambo matatu yaliyonifanya nimshushe Kanumba na kumdharau.
1. kwa siku za karibuni Kanumba alikaririwa akisema yeye hana mchumba na wala hanywi Pombe, lakini kifo chake kimedhihirisha kuwa Kanumba alikuwa ni Mzinzi na mlevi pia.
Hivyo ni wazi kuwa Kanumba alikuwa ni msanii muongo mwennye kutaka kuonekana msafi machoni mwa watu


2. Pia Kanumba kwa siku za karibuni amesikika akidai kuwa Baba yake pamoja na mama yake wa kambo walimtesa sana pindi alipokuwa anaishi nao.
Wenye akili wakahoji je walikutesa vipi?
Lakini likaja jibu kuwa Kanumba alipokuwa kwao alikuwa anachunga Mbuzi na kuosha vyombo.
Hayo ndio mateso ambayo Kanumba aliamua kumuanika Baba yake na kupelekea kutoelewana kati yao.
Hapa dogo alikosea...


3.Pia jamii iliamini kuwa Lulu ana uwezo mkubwa wa kuigiza.
Hivyo ilimkabidhi Kanumba mtoto huyo ili akisimamie kipaji cha mtoto huyo lakini Kanumba hakufanya hivyo bali alimtumbukiza mtoto huyo kwenye dimbwi la ngono.


Sasa je kwa machache hayo Kanumba kaifunza nini jamii inayovutiwa na kazi zake za sanaa?

Acheni chuki zenu bwana.
Tanzania mpira wa miguu, tensi, riadha, mbio za magari, dats, gof na michezo mingine hatupo katika ramani hata
ndani ya afrikatu.
kanumba ndo alikua ameanza kututoa kimasomaso wa tz afrika na nje ya afrka.
kwa mtu mwenye akili lazima akubali mchango wake chanya kwa taifa.
yeye kama ulivyo wewe lazima alikua na matatizo yake (ambayo labda ndo ayo ulosema), kwa hyo chamsingi ni kuchukua chanya zake na kuacha hasi zake. kwani we ni mwema sana?????
tumeshuhudia mara nngapi wasanii wakifanya maonesho/shoo kwa ajili ya kuchangisha kuisaidia jamii? ni kwa nini tusifanye michango kama hiyo sisi watu wa kawaida?jibu ni kua hatuna ushawish. ukiita tamasha wewe nani atakuja kukuskiza/kukuangali??
huo/hyo ndo siafa ya kanumba.
Mwisho wa siku tunabaki kutumia/kusikiza/kuangalia burudani za nje tu kisa chuki zenu. miziki mingine mfano ya kinigeria inayopigwa ni ya kawaida/mibovutu ila inapewa promo kweli na ya kwetu mizuuuri imewekwatu kapuni.

RIP brother.
 
Mzee Jangala mbona mzima wa afya yupo nyumbani kwake Tabata Mawenzi? Halafu suala la namna ya kumheshimu marehemu huwa halipangwi linakuja automatically kutokana na mtu mwenyewe alivyogusa watu. Huwezi kupata jibu la kwanini iwe hivo kila mtu ukimuuliza atakupa jibu lake. Kwangu mimi huyu kijana Kanumba amefariki akiwa bado mtoto mdogo na namna alivyokuwa ndo anainukia nyota yake katika maisha ndo inaanza kung'aa halafu akazimika ghafla bin vuu hiyo inauma sana.
 
Duh!

Kwa hiyo Lulu atakuwa amehusika kumsukuma Marehemu na ndipo yaliyompata yakatokea!

Kama ndio hivyo itabidi aachiwe huru bila hata ya kesi mtoto wa watu Lulu!


Rest In Peace Kanumba!
 
Wewe ndio wasema!
HAta waliokufa kwenye Guest house wamezikwa na makanisa.

Jamani guest house ni nyumba ya kilala wageni, mbona mimi mlokole wiki nzima hii nalala kwenye guest house coz I'm a guest.
 
Hapo hakuna mjadala!

Hakuwahi kuoa akawa ameacha!
Kuna vigezo mingi itakayoifanya Kanisa kumzika kwa heshima zote!
Pamoja ya yote hayo ni lazima Kanisa litamzika kwa heshima yote!
 
Back
Top Bottom