Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kwa wale ambao wanaweza kuona Clouds Tv na Tbc mnaweza kushuhudia hali ilivyo!
 
NATA kwanini unaongea hadithiaka michapo wakati Tecno zipo na unaweza kupiga picha hata za kiuzushi ukakazia kauli yako?
 
Dha! Kila nafsi itaonja mauti, Dha! kifo cha ghafla ivi dha! Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Steven mahala pema. Amina
 
mkuu Hossam si kazi ya madaktari kutaja nani alimtikisa Kanumba, hiyo ni kazi ya Polisi
 
katika hali isiyo ya kawaida kwa wale ambao wamesikia wimbo wa kanumba.katika wimbo ule kasema akifa watu mtasema nani pengo ataliziba.maadui wake watabeba jeneza lake. yeye ni mmoja hawezi pigana na watu 1000. je hii alijua atakufa?
Katika ulimwengu huu sidhani kama kuna kitu cha uhakika zaidi ya kifo. Wewe mwenzetu huna uhakika kuwa kuna siku utakufa?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Anaweza kuwa alianguka kwa kuteleza kwenye tiles, maana twaambiwa alikuwa katoka kuoga.
Concussion inaweza tokea kwa kujigonga, kupigwa au kutikiswa.
Nashindwa kuelewa why ung'ang'anie kuwa Lulu anahusika, bila ku rule out hizo option nyingne.
Lulu ana nguvu gn za kumsukuma Kanumba hd aanguke?
Utasema kanumba alikuwa amelewa, labda ndo maana alisukumwa kirahisi.
Lkn si imesemwa kuwa Kanumba aliweza kumkimbiza Lulu, kumkamata na kumvutia ndani(whch means alikuwa na nguvu za kutosha tu kumshinda Lulu).
 
kuna uharo mwingine nimemsikia anasema eti tuyaenzi yoote alioyafanya kanumba...
Mi nimejiuliza ya ulevi na umalaya pia yaenziwe?
Au kuwasimanga wazazi wetu kwa maneno ya uongo redioni nayo tuyaenzi?
 
Forum ipunguze HATERS, IONGEZE GREAT THINKERS,
 
Kwa taarifa za kuaminika ni kwamba mzee Kanumba hakufika kumzika mwanae ila katuma muwakilishi tuu.
Kunani hapa?????????
 
kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Kinondoni amenukuliwa na gazeti la Daily News la leo hii akisema kuwa Kanumba (RIP) inasadikika alimpiga na mapanga Lulu kwenye sehemu zake za siri.

Kadiri ambavyo habari zinazidi kutoka vyanzo mbalimbali, naona lawama zinazidi kuelekea upande wa Kanumba, pengine yeye mwenyewe ndo alisababisha kifo chake.
 
Kitendo cha kumuweka mtuhumiwa ndani kwa muda mrefu bila kumfikisha mahakamani ni uvunjaji wa haki za binadamu. Kama ni kweli ianvyoelezwa kuwa Lulu anahusika moja kwa moja na kifo cha Kanumba basi inatakiwa afikishwe mahakamani haraka kwa kosa la kuua bila kukusudia ili aombewe dhamana. Watanzania bado tunakumbuka kuwa Ukiwaona DITOPILE Mzuzuri Mwinshehe Ramadhan alimfuata dereva wa daladala kutoka pale alipogongwa gari yake hadi kituo kilichofuata na kumfyatulia risasi hadi kufa, lakini alipatiwa dhamana kwa kuwa kosa la kuua bila kukusudia (Manslaughter) linastahili dhamana. Vivyo hivyo kwa huyu Lulu ambaye inasemekana alidundwa na marehemu Kanumba na kuna alama za kipigo mwilini mwake (kwa mujibu wa waliomuona eg Bulaya, Mdee) anastahili kupewa dhamana na kuendelea kuhudhuria kesi akiwa uraiani hadi hukumu itakapo tolewa. Pia tukumbuke huyu mtoto bado ni minority kwa kuwa hana miaka 18 hivyo sehemu ya lawama kwa kosa alilolifanya inamuendea aliyemsababishia kosa kwani akili ya mtoto wa miaka 17 haijapevuka. Kamanda Kova, dunia nzima inakuangalia na huyu mtoto amekaa ndani kwa zaidi ya masaa 96 bila kufikishwa mahakamani, kuendelea kumshikiria ni uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu.
 
kwa taarifa tulizo nazo alianza kumtafuna mtoto akiwa na 16,jamaa alikuwa mtu wa ovyo sana

Duh! Utadhani ulikuwepo wakati wanaanza, Lulu nimtu mzima, angekuwa anaishi Arumeru angepiga kura kumchagua mbuge
 
Duu mzee ana hasira sana kama kweli hakuja,labda anaogopa usalama wake si unajua kulikua na beef hapo juzi kati?
 
Ya nini afe kwa presha kwa kupandishwa ndege kwa mara ya kwanza uzeeni!...acha amlilie mwanae akiwa nyumbani tu!
 
Jaman tukumbuken kuwa kipimo unachotumia kumhukumu mwenzio ndicho kitakachotumika kukuhukumu wewe,
2sipende kumuhukumu Lulu kama mleta thread anavyosema mi mwenyewe siwezi kumuhukumu Lulu kama muuaji anayeujua ukweli ni mungu, marehemu na Lulu mwenyewe.
 
katika hali isiyo ya kawaida kwa wale ambao wamesikia wimbo wa kanumba.katika wimbo ule kasema akifa watu mtasema nani pengo ataliziba.maadui wake watabeba jeneza lake. yeye ni mmoja hawezi pigana na watu 1000. je hii alijua atakufa?

....haya sasa, nani anayedhani hatakufa?
Mwenye imani haba hujisahau, ....mwenye kumbukumbu kifo ni
popote, kwa yeyote, mahala popote, kwa sababu au bila sababu yoyote.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom