Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Chanzo namba moja cha kifo cha Marehemu ni uzinzi, walikuwa wanafanya Uzinzi na Lulu na popote palipo na Uzinzi ni shetani tu ndiyo anatawala hilo eneo hakuna malaika mwema, sasa nitashangaa sana leo kama kwenye Ibada hao viongozi wa dini hawatakemea vitendo vya zinaa, kifo cha Kanumba ni kazi ya shetani.Truth is bitter pill many people don't like it.
Kwa makosa gani mkuu?Wakufungwa hapa ni alikiba,dr cheni na ray!!
katika hali isiyo ya kawaida kwa wale ambao wamesikia wimbo wa kanumba.katika wimbo ule kasema akifa watu mtasema nani pengo ataliziba.maadui wake watabeba jeneza lake. yeye ni mmoja hawezi pigana na watu 1000. je hii alijua atakufa?
bahati mbaya maiti haisemi, hv ukweli kabisa unasema the deceased alimfundisha ngono kale katoto?????? kale katoto kamejifunza kenyewe mbn kalisahshindikana mapema...ukweli ni kuwa kifo chake amejitakia mwenyewe, tulimkabidhi katoto kale akafunze sanaa yeye akakafunza na ngono pia, cha kusikitisha ni kuwa pamoja na kuelimisha jamii lakn yeye hakuwa ameelimika aliwanyanyasa wanawake kwa kuwapiga kama alivyoigiza ktk yellow banana!!!!, ngono zembe zikamuu, katoto alikokalea kamepelekea kifo chako hii yote kwa kuwa alikosa maadili kama baba mlezi, ni laana....mficha donda mauti humuumba
John Shibuda ni Mbunge wa Shinyanga kupitia chama cha Chadema na baba wa marehemu anaishi Shinyanga! Shibuda anaendelea kushusha mistari yenye vina kama tulivyomzoea.
TBC 1 wamekatiza matangazo baada ya John Shibuda kuonekana Live! Hahahaha siasa mchezo mchafu sana!
Wakufungwa hapa ni alikiba,dr cheni na ray!!
kumbuka, lulu alishikiliwa jumamosi, asingeweza kupelekwa mahakamani kwasababu ilikua ni public holiday, jpili na jtatu, leo ndio anaweza kupelekwa huko mahakamaniKitendo cha kumuweka mtuhumiwa ndani kwa muda mrefu bila kumfikisha mahakamani ni uvunjaji wa haki za binadamu. Kama ni kweli ianvyoelezwa kuwa Lulu anahusika moja kwa moja na kifo cha Kanumba basi inatakiwa afikishwe mahakamani haraka kwa kosa la kuua bila kukusudia ili aombewe dhamana. Watanzania bado tunakumbuka kuwa Ukiwaona DITOPILE Mzuzuri Mwinshehe Ramadhan alimfuata dereva wa daladala kutoka pale alipogongwa gari yake hadi kituo kilichofuata na kumfyatulia risasi hadi kufa, lakini alipatiwa dhamana kwa kuwa kosa la kuua bila kukusudia (Manslaughter) linastahili dhamana. Vivyo hivyo kwa huyu Lulu ambaye inasemekana alidundwa na marehemu Kanumba na kuna alama za kipigo mwilini mwake (kwa mujibu wa waliomuona eg Bulaya, Mdee) anastahili kupewa dhamana na kuendelea kuhudhuria kesi akiwa uraiani hadi hukumu itakapo tolewa. Pia tukumbuke huyu mtoto bado ni minority kwa kuwa hana miaka 18 hivyo sehemu ya lawama kwa kosa alilolifanya inamuendea aliyemsababishia kosa kwani akili ya mtoto wa miaka 17 haijapevuka. Kamanda Kova, dunia nzima inakuangalia na huyu mtoto amekaa ndani kwa zaidi ya masaa 96 bila kufikishwa mahakamani, kuendelea kumshikiria ni uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu.
Nimesikia huo wimbo...sauti ni kama ya SK hivi kweli wimbo huo uliimbwa naye au ni wasanii wa muziki wametunga kumuenzi SK?
Amesema akazikwe fasta!Amesemaje shibuda tbc1 imekata nimeshindwa kuona live na huku kwetu clouds haishiki kabisa!
Chanzo namba moja cha kifo cha Marehemu ni uzinzi, walikuwa wanafanya Uzinzi na Lulu na popote palipo na Uzinzi ni shetani tu ndiyo anatawala hilo eneo hakuna malaika mwema, sasa nitashangaa sana leo kama kwenye Ibada hao viongozi wa dini hawatakemea vitendo vya zinaa, kifo cha Kanumba ni kazi ya shetani.