Kitendo cha kumuweka mtuhumiwa ndani kwa muda mrefu bila kumfikisha mahakamani ni uvunjaji wa haki za binadamu. Kama ni kweli ianvyoelezwa kuwa Lulu anahusika moja kwa moja na kifo cha Kanumba basi inatakiwa afikishwe mahakamani haraka kwa kosa la kuua bila kukusudia ili aombewe dhamana. Watanzania bado tunakumbuka kuwa Ukiwaona DITOPILE Mzuzuri Mwinshehe Ramadhan alimfuata dereva wa daladala kutoka pale alipogongwa gari yake hadi kituo kilichofuata na kumfyatulia risasi hadi kufa, lakini alipatiwa dhamana kwa kuwa kosa la kuua bila kukusudia (Manslaughter) linastahili dhamana. Vivyo hivyo kwa huyu Lulu ambaye inasemekana alidundwa na marehemu Kanumba na kuna alama za kipigo mwilini mwake (kwa mujibu wa waliomuona eg Bulaya, Mdee) anastahili kupewa dhamana na kuendelea kuhudhuria kesi akiwa uraiani hadi hukumu itakapo tolewa. Pia tukumbuke huyu mtoto bado ni minority kwa kuwa hana miaka 18 hivyo sehemu ya lawama kwa kosa alilolifanya inamuendea aliyemsababishia kosa kwani akili ya mtoto wa miaka 17 haijapevuka. Kamanda Kova, dunia nzima inakuangalia na huyu mtoto amekaa ndani kwa zaidi ya masaa 96 bila kufikishwa mahakamani, kuendelea kumshikiria ni uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu.