Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kibagata nimekusoma, pia niliwahi kusikia kuwa alitoa maneno machafu na dharau kwa baba yake mzazi. Japo yawezekana baba yake ni kweli alimtelekeza lakini yeye akiwa kama msanii alitakiwa awe mwalimu wa jamii. maana tabia hiyo ingeigwa na kizazi cha sasa yeye alikuwa role model hakutakiwa afanye hivyo, je ni kweli baba Mzazi wa Kanumba hakufika kwenye mazishi?????
 

Heading na ulichoeleza humu ndani ni vitu tofauti kabisa sijui una maana gani?
 
bado ni vigumu kwangu na watu walionizunguka kuukubali ukweli wa kifo cha nguli huyu!

kwa nini maisha yapo hivi?

na kwa nini tumekawia kuukubali ukweli huu...bora Kanumba ungebaki kule mochwari tujue bado upo nasi,,,ila haupo tena!!

umelala nyumba yako ya milele pale kinondoni

tumelia sana na bado tunaendelea kulia!!

Mungu akusamehe dhambi zako zote;ukaangaziwe mwanga wa milele upumzike kwa amani...

Kanumba haupo tena duniani.umeenda!!huo ndio ukweli tunaokataa kuukubali...naomba tuache kuponda na tuungane na walio wengi kuendelea kuomboleza
 
me ninashangaa kila mtu anamuhukum lulu,kiukweli kila sehem ina utaratibu.Ebu tujaribu kuwa wavumilivu 2one muafaka wa hili suala.Kwa wale wakristo wenzangu ktk ktb kitakatifu kuna wa2 walimpeleka mama mmoja wakamshtak wakiwa na mawe,wakamwambia huyu ameshkwa akizini.Yesu akawaambia acye na dhambi awe wa kwanza kumpiga jiwe,wte wakasepa.Ni mfn tu acye na dhambi amuhukum lulu.
 
Nadhani upo sawa, mimi nilivyomuona jana kwenye Tv anaongea nilihisi kama vile kuna hali ya kutoelewana kati ya Marehemu na baba yake
 


Naunga mkono maoni yako, si kwamba namuonea wivu marehemu kanumba, but frankly speaking, hakustahili heshima kubwa aliyopewa! hakustahili kupewa hadhi ya kuwa kioo cha jamii. mfano mzuri ni mazingira ambayo mauti yalimkuta
 
Mwanao amefariki unasubiri uletewe nauli, Kama haikuletwa hauendi, hii imekaaje?.
 
i saw the interview myself, salama i asked her"una boyfriend kwa sasa"? she replied & i quote"sina boyfriend na wala sijafikiria kwa sasa". I saw it live
 
Mbona mnatuchanganyia habari??Amefika au hajafika lipi tuelewe??maana mwingine anasema hajafika ila mzee shibuda ndio amemuwakilisha mwingine anasema amefika na jana alikuwa anahojiwa so neno gani tukubali hapa!
Kwa ninavyofahamu hajafika, ila mahojiano yalofanyika ni shinyanga akiwa nyumbani kwake na mtangazaji wa tbc
 
Kama ulitizama kaburi kwa ndani (visit jamii photos) kuna sehemu mbili chini ya kaburi (miguuni na kichwani) pameachwa wazi bila kuweka vigae. Na kuna member aliyeuliza ni kwa nini pameachwa katika thread ile. Jibu ni kwamba ni receiving area ya mabaki ya marehemu Kanumba. Japo pia itachukua muda mrefu kusagwa na udongo!!! But ndiyo maziko mengi ya siku hizi ya wenye nazo. Nimehudhuria misiba kadhaa ya namna hiyo.
 
baba yake hakufika, na marehemu hakumtukan he jst said the reality, ambayo inauma lakini ilibidi baba mtu aambiwe maana wazazi huwa wanajitokeza baada ya kuona kuna fedha kwa mtoto. ameifundisha jamii. kwa kumuweka hadharani dingi yake itasaidia wazazi wengine kuwapenda na kuwajali watoto wao no matter what!
 
Uliwahi kuona alipozikwa Papa Yohane Paulo2?
Sure kaburi lake lilisakafiwa hadi chini hakuna hata matundu ya mchanga/udongo kama ilivyaoachwa kwa marehemu Kanumba. Hata marehemu askofu Joseph Sipendi wa Jimbo la Moshi kaburi lake likisakafiwa top down hakuna udongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…