Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Ukiona msanii anajipima kwa Rais, basi msanii ndiye kashinda.R.I.P uncle JJ.
 
pumzika "moses"....!

always our hero!

pumzika brother.dunia imetambua uwepo wako
 
Hili halina ubishi kuwa Kanumba kawafunika wasanii, macelebrety na wanasiasa wetu wote (Except Nyerere) waliotangulia mbele ya haki kwa kuzikwa na watu wengi zaidi,hii inaonyesha alikuwa anakubalika sana katika fani yake ya uburudishaji katika sanaa ya filamu.Mwenye ugomvi nae amsamehe na mwenye madeni huu ndio wakati wa kulipwa ili mwenzetu akapumzike kwa amani(kama kweli kuna mapumziko). Kilichobaki sasa ni kumuomba Mwenyezi Mungu amrehemu..Ameen

Sudden death of Kanumba, reminds us that we should live our lives everyday as the last day with great fear of the Almighty God. Once your gone, if you had no time to mend/make up right your ways with him, it does not matter how many prayers people will be praying for you, your judgement is already settled. So my dear friend it's about time we should turn and confess all our sins to God. Provide me with scriptures that clear show that with prayers of others you will be rescued from punishment of your deeds.
 
Huwezi kulinganisha msiba wa kanumba na Nyerere. Wewe uliona watu waliovyojipanga kuanzia Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam hadi Msasani? Je, unakumbuka kuwa wakati wa msiba wa Mwalimu hata vibaka na majambazi waliweka chini zana zao za kazi? Pitia taarifa ya polisi inayohusu uhalifu uone maajabu!!! msiropoke kumhusisha Kanumba na Mwalimu ambaye alizikwahadi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marakani na marais wasio na idadi!
 
Lakini na story behind ya kifo chake imedraw attention hence umati mkubwa hivyo. Angeugua hata kwa week moja nadhani isingekuwa hivi.
 
Tumesema mengi juu ya Kanumba,kuna ambayo yatasaidia kutuelimisha.
Lakini sasa imebaki historia tuu.......Kanumba hayupo tena.
Mm nina yangu yamenigusa,kwanza natoa pole kwa wafiwa wote.
Baada ya pole sasa ngoja nifunguke.
Ktk ukiristo kuna kifungu kinasema"ulitoka kwa udongo utarudi kwa udongo"kwa uelewa wangu ni kwamba tuliumbwa kwa udongo na tutarudi udongoni.
Kwa kutumia kifungu hicho basi mwenyezi mungu atawahukumu wote waliomjengea kanumba "hekalu"la kumzikia badala ya kaburi.Sasa kwa mjengo huo yeye atarudi kwa udongo lini?Hamuoni kama atasubili miaka mingi sana kurudi udongoni?
Na huyo sijui padri hakuliona hili?au yeye kifungu hiki hakijui?
Nasisitiza kwamba hayati KANUMBA hakutendewa haki kabisaaaaa!
Naomba kuwakilisha.
RIP KANUMBA.

Watu wa dini hawaishi cha kukujibu. Wanaweza kukuambia "udongo" maana yake ni kutokuwa na uhai, kwa hiyo ametoka udongoni maana yake ametoka kusiko uhai na atarudi kusiko uhai akisubiri ufufuo.

La sivyo kama unaongelea literary, mtu anaweza kuagiza mwili wake uwekwe kwenye spaceship akifa arushwe anga za juu, atarudi vipi kwenye udongo? Au wanaanga wakifikwa na ajali angani miili yao ikatapakaa anga za juu watarudi vipi katika udongo?
 
kwa lugha nyingine wale ambao wakifa miili yao inachomwa moto huwa hawarudi mavumbini? Au umesahau kuwa rohi ndo ya muimu kuliko kaburi?

Hebu mwacheni kanumba alale kwa amani jamani loh!!!!

Mwisho kabisa nakuachia hii
'mwanangu, mlilie mtu aliyekufa;lia kwa uchungu, kuonyesha huzuni yako
Uuzike mwili wake kwa heshima ipasavyo, wala usipuuzie mazishi yake.

Kumbuka, utakufa kama alivyokufa , jana yeye, kesho wewe.
Marehemu anapowekwa kupumzika kaburini,
nako kumkumbuka kuachwe;
nawe usiendelee kumlilia roho yake ikisha ondoka
SIRA 38 :16, 22-23
 
Kwani maandiko ya dini huwa yanabadilishwa kila baada ya muda gani?
Kama huwa hayabadilishwi sasa vp tena mtu akazikwe anga za juu?huoni kwamba pengine hali ya maisha ya sasa imechangiwa na hawa watu wenye mawazo kama yako mkuu???
 
Kwanza kabisa naomba ku-declare interest..mimi siyo mpenzi wa Bongo Movies ila natambua kwamba Bongo movies imeshika katika vichwa vya watanzania wengi ambao kwa asilimia kubwa hawawezi kuangalia even Nigerian (tupa kule american) na wakaelewa..natambua kuwa kuna watu ambao haziwezi kupita walau siku mbili bila kuangalia hizi movie za nyumbani kwetu. Watu hawa wapo wengi kuliko unavyoweza kufikiri na ni kama ilivyo kwangu isivyowezekana kupita siku mbili bila kusoma kitabu chochote au kufuatilia politics!. Lengo la kusema haya awali ni kutaka kuonesha kwamba kama binadamu..kuna wanaopenda vitu fulani fulani il-hali vitu hivyo hivyo wengine hawataki kusikia..ndio maana kuna watu humu JF huwaambii kitu kwa CHADEMA,CCM or even CUF.Ndiyo maana vidole kwenye mikono,miguu ni vitano lakini havilingani..vikilingana.... you can imagine the situation!

Back to the topic, suala hili ambalo limeenea kwa 'the so called' wanaoweza kufikiri na kupambanua i.e great thinkers kwamba watu waliojitokeza kuhudhuria msiba wa Steve Kanumba (R.I.P) ni wajinga,punguani ambao hawana kazi za kufanya limenisikitisha sana.

Nataka kuwarudisha nyuma si chini ya miaka miwili iliyopita ya kifo kilichotokea cha Mtu Mweusi mwenye mbwembwe nyingi..Michael Jackson a.k.a Wacko Jacko. Wamarekani walilala nje ya Mjengo wa Wacko Jacko,ulaya,asia watu walikusanyika open spaces kote huko.. Watu walifunga barabara za mitaa mbali mbali marekani kwa ajili ya kuomboleza..CNN, BBC,Al-Jazeera etc etc walikatisha program zote za Ki-uchumi,kisiasa etc etc ili kucover tukio la kifo cha Wacko Jacko..Tena siyo kwa siku moja..ni kama wiki 2 mfululizo na zaidi na zaidi..! Ndugu zangu akina Masanilo and co., niwaulize hivi hawa hawataki maendeleo ya ki-uchumi?? Wao hawakuwa na kazi za kufanya?.

Je Nyerere alivyokufa watu wakajitokeza barabarani, shughuli za kiuchumi etc etc zikasimama, watu hawakuwa na kazi za kufanya?. Wanasiasa wanapokuwa mahali na kukusanya Lundo la watu (tumeona Zitto kirumba, Mbowe & co Arusha, Barack Obama alipoenda Ujerumani etc etc) wale wahudhuriaji wanakuwa hawana la kufanya?. Tofauti ya matukio haya ni kwamba moja ni msiba jingine ni politics..lakini uhudhuriaji waweza kushabihiana.

Guys, Funguka...usidhani kila unachokifikiri wewe ndio kila mtu afanye..! Kanumba was a celebrity, hata baadhi ya watu hapa wakifa na ikajulikana given the fact kwamba wao ndani ya JF ni Celebrities (I cant mention names,but I know even these guys amongst them ar celebrities within JF)..Quote my words,asilimia kubwa za Post zitawaongelea wa0, mara oh, tutengeneze t-shirt,tujitokeze msibani kwa wingi, alikuwa mtu mzuri etc etc!

Cha msingi ni kutambua kila mmoja ana uhuru wa kufanya yale anayotaka kuyafanya kwa muda wake yeye mwenyewe kadiri anavyoona inafaa. Ndio maana mimi hata sijaangalia wala kufuatilia popote hiyo Live coverage zaidi ya kuingia JF jioni hii na kupata news..it is enough for me! Lakini kuna watu leo ofisini, kwenye biashara zao, kwenye mashamba yao etc etc kulikuwa hakukaliki wakitaka kufuatilia Kanumba anazikwaje kwa kuhudhuria wao wenyewe,kupitia radio,TV au hata internet.

Everything is about Choices, and we must not envy others choices or even mock their choices because definitely they will mock ours, it is simple..they are not theirs. He was great to them, they chose him to be like that, it is not for you, you chose otherwise ..dont mock their choices!

Alamsyk.
 
Hili halina ubishi kuwa Kanumba kawafunika wasanii, macelebrety na wanasiasa wetu wote (Except Nyerere) waliotangulia mbele ya haki kwa kuzikwa na watu wengi zaidi,hii inaonyesha alikuwa anakubalika sana katika fani yake ya uburudishaji katika sanaa ya filamu.Mwenye ugomvi nae amsamehe na mwenye madeni huu ndio wakati wa kulipwa ili mwenzetu akapumzike kwa amani(kama kweli kuna mapumziko). Kilichobaki sasa ni kumuomba Mwenyezi Mungu amrehemu..Ameen

Wengine tulikuwa wadogo wakati wa marehemu Sokoine waliokuwepo watujulishe maana na yeye alikuwa mwanasiasa
 
Huwezi kulinganisha msiba wa kanumba na Nyerere. Wewe uliona watu waliovyojipanga kuanzia Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam hadi Msasani? Je, unakumbuka kuwa wakati wa msiba wa Mwalimu hata vibaka na majambazi waliweka chini zana zao za kazi? Pitia taarifa ya polisi inayohusu uhalifu uone maajabu!!! msiropoke kumhusisha Kanumba na Mwalimu ambaye alizikwahadi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marakani na marais wasio na idadi!
mbona mtoa mada kasema EXCEPT NYERERE...hapo nani karopoka kati yako na mtoa mada.?
 
Back
Top Bottom