Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

tatizo kubwa sana katika huu msiba.....mzee ana point sio bure
 
lulu hana hatia ya kuua, hakukusudia na alikimbia kwa uoga wa kawaida wa kibinadamu cause ataingekua mimi ningekimbia. hatumhukumu kwa kuua maana hata nikimfikiria sidhani hata kama anaakili za kuwaza kumuua mtu, ila atakua amepata fundisho kubwa sana.
 
Mkuu hilo andiko vipi sasa?inamaana halina nafasi kwa mwenye pesa?
 
huo ndo ukwel na jamii imehuzunishwa na tukio na siyo kifo,alikua karibu na jamii kuliko rais ila alikua kimaslah na si kuelimisha

nchi yetu njaa ni kali sana sasa angebobea kuelimisha zaidi ya kuburudisha asingepata mashabiki na kazi zake zisingenunuliwa sana...alisoma alama za nyakati na kuwapa wapenzi wake kitu wanataka!
 
na hapa Sugu akitoa Salaam za Mwisho kwa niaba ya WAPIGANAJI WOTE , WAHANGA WOTE WA WIZI WA SANAA, NA KWANIABA YA VIJANA WAPENDA HAKI NA SANAA


Dah!Kamanda anaonekana kuwa na machungu ya ukweli...Yaani badala ya kuonyesha ishara ya msalaba au kupiga magoti kama ilivyo ada ya madhehebu mengi ya ki kristo...Yeye kaamua kupiga salute kama mjeshi vile.
 
sikuona hata mdogo wa marehemu wala mama yake kukaa eneo maalumu..ila nimeona wasanii kibao na miwani yao myeusi
 
Believe kanumba ameishi zaidi maisha ya kifilimason,ndio maana nduguze wamemsusa
 
hata km nitakosana na mwanangu au mzazi wangu akifa au nikifa tuzikane jamani
 
nchi yetu njaa ni kali sana sasa angebobea kuelimisha zaidi ya kuburudisha asingepata mashabiki na kazi zake zisingenunuliwa sana...alisoma alama za nyakati na kuwapa wapenzi wake kitu wanataka![/QU@ kwel njaa ipo tena kali mno.
 
Apa kuna kitu kimekiukwa
Nyerere alikuwa kipenzi cha watu zaidi ya Kanumba na alizikwa kwao sasa why Kanumba azikwe DSM wakati baba mzazi alitaka azikwe Shy.
Time will tell utashangaa mwili unahamishwa kwenda shy bse Dingi hajalidhika
 
Pole yako.......

Na unadhani unanijua?
Pole sana. . . .

Binadamu ni wepesi sana wa iuhukumu mtadhani nyie ni malaika kumbe uozo mtupu.........

sasa kama binadamu wote ni wakosefu, kwanini wote wasifungwe gerezani? maana yake ni kuwa hata kama ni wakosefu lakini tunatofautiana ukubwa wa makosa, hivyo usimtetee sk.Atajitetea mwenyewe kwa sir god manake kesi za huko nasikia hazina wakili wala rufaa!
 
jamani kama baba kakutenga, kakupa manyanyaso ya haja utafikiri wewe ulisingiziwa kwake, mungu si Achumani, ukatoka kutoka huko ulikokuwa, kwa kawaida utaegemea zaidi upande uliokupa upendo, baada ya kifo chake Clouds TV, nafikiri yule dada ni zamaradi katika kipindi kile jamaa alikiri kabisa kwamba alikuwa apigwa na mzazi wake huyo, bila kumung'unya maneno akasema si unajua maisha ya mama wakambo. tunajua wazee wengi miaka ya nyuma kidogo kupiga ilikuwa ni kitu cha kawaida hasa kwa watoto wanapokosa, lakini kwa SK kuliongea hilo inawezekana ilizidi kipimo.

hivyo basi Baba inawezekana alikuwa bado hapata nafasi kwenye moyo wa SK. na inawezekana mama ndio mtu wa karibu hata kwa marafiki zake.
 
Vicent kigosi maarufu kama ray amesema atacheza filamu na jennifer pamoja na yule dogo mwingine wa kiume walioigina na kanumba katika filamu ya anko JJ ili kumuenzi kanumba. Pia ameahidi kuanza kuigiza na watoto wadogo kama alivyokuwa anafanya kanumba ili kumuenzi.


source: DW idhaa ya kiswahili.
 
Dah!Kamanda anaonekana kuwa na machungu ya ukweli...Yaani badala ya kuonyesha ishara ya msalaba au kupiga magoti kama ilivyo ada ya madhehebu mengi ya ki kristo...Yeye kaamua kupiga salute kama mjeshi vile.

Alianza kupiga ishara ya msalaba ndo akapga hiyo salute ila huo mkono wa kushoto mitaa ya kati vp? au ndo anawakilisha kuwa SK ni hapo kati ndo pamechangia kifo chake?
 
Hili halina ubishi kuwa Kanumba kawafunika wasanii, macelebrety na wanasiasa wetu wote (Except Nyerere) waliotangulia mbele ya haki kwa kuzikwa na watu wengi zaidi,hii inaonyesha alikuwa anakubalika sana katika fani yake ya uburudishaji katika sanaa ya filamu.Mwenye ugomvi nae amsamehe na mwenye madeni huu ndio wakati wa kulipwa ili mwenzetu akapumzike kwa amani(kama kweli kuna mapumziko). Kilichobaki sasa ni kumuomba Mwenyezi Mungu amrehemu..Ameen
 
Sidhani kama ni wakati mzuri wa kunyoosheana vidole ,binafsi naona ni wakati mzuri wa mtu mwenyewe kujitazama uishivyo na pili kujiuliza utakapofikwa na hali kama hiyo{umauti} utakuakatika hali gani?
Msisitizo: Ni vema kujichunguza mtu binafsi na kujirekebisha kwa dhati yani kwa kumaanisha ili kua mfano mzuri kwa jamii inayokuzunguka ukiwa hai na ata utakapokufa.
 
Im a new comer; plz naomba mnipokee. @@kwel sasa hatma ni mambo ya low2 hapo kuanzia kwa dpp,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…