Kwa uelewa wangu, msanii kuwa kioo cha jamii maana yake nikwamba sanaa ya jamii fulani ni moja ya vitu ambavyo vinonyesha sura ya ilejamii.
Nikiangalia wasanii wa movie za Tanzania nachoona reflection ya maisha ya kila siku ya vijana wengi wanaoishiktk miji mikubwa...uvaaji wao, starehe zao wakitoka usiku, mahusiano yao, hatamovie wanazo tunga na kuact, nyingi zina reflect mawazo, tabia zilizoko kwenye jamiizetu, au maisha ya vijana wengi wakawaida wa mijini kwa ujumla...na hata uchezaji movie eg low quality,kuchanganya kiingereza kibovu na Kiswahili, uigizaji wa viwango vya chinikulinganisha na nchi ambazo zimeendelea katika hii fani etc vyote hivivinawakilisha maisha ya vijana wa jamii zetu za mijini... elimu duni, teknologiahafifu, kuiga zaidi ya ubunifu, dhana kwamba kiingereza kitatutoa, kuigafasheni na life styles za magharibi, huku tukipigana na umaskini, ubinafsi namfumo mbovu uliogubikwa rushwa za aina mbalimbali.
Sidhani kwamba wasanii ndio chanzo kikuu cha maovu yoteyanayoendelea katika jamii kwamba waondio wafundisha watoto / vijana kuwa na tabia zisizofaa kwenye jamii etc kwakiasi kikubwa , nadhani wasanii ni reflection tu ya kile ambacho kinaendeleakwenye jamii. Utakuta mama au dada mkubwa anacheka na wanawe/wadogo zaketeenegers uvaaji "nusu uchi" wa msanii wa kike kwenye bongo movie, "duh kavaakama Rihanna, kapendeza kiasi chake, ila hajamfikia, angekuwa mwembamba hivi... halafu ile mini ingebana zaidi, angalau...."etc
Nafikiri watu nambari wani wanaopaswa kuwajibika kwenyemalezi kwa kutoa mfano mzuri kwa vijana/watoto wetu ni sisi wazazi. Kuto spend qualitytime na watoto, kuwapa mlolongo wa wasichotakiwa kufanya bila kuchambua nakuelewa kinachoendelea out there na kujadiliana nao wanacho takiwa kufanya nambinu za kuishi kimaadili bila kufuata makundi au kuiga tabia zisofaa, kujenga uadui zaidi na watoto wetu kuliko urafiki.Wazazi tutunze ndoa zetu, tuwe best friends wa wake/waume zetu na marafiki/mentorswa karibu watoto wetu.