Steven Kanumba kama alivyofahamika, kwa sasa ni marehemu.
Kifo chake naweza kusema kuwa kimewagusa watu weengi ukizingatia alikuwa ktk fani ya maigizo, na ni mmoja kati ya waigizaji ktk runinga anayetajwa kuwa maarufu sana hapa nchini na nchi za jirani.
Hakuwa msanii mkongwe, lakini amekuwa na nyota ya kupendwa na kuvuta hisia za wengi kwa kipindi hiki kifupi alichojiunga ktk fani hiyo.
Kifo chake pia kimekuwa faraja kwa vyombo vya habari hasa Televisheni na Redio ambazo hazina vipindi vya kueleweka.
Pia hata Magazeti ambayo hayana ya maana ya kuandika, nayo pia yamejaza picha za marehemu na udaku wa hapa na pale.
Kifo cha kijana huyu pia kimeita hata viongozi wa ngazi mbalimbali za kisiasa hapa nchini.
kimemuita mpaka Rais wa nchi na kumlazimu aahirishe safari yake ambayo ilikuwa na manufaa kwa taifa na kuja kujumuika ktk msiba.
Kila kona ya wasio na kazi au wasio na ya maana ya kufanya basi habari imekuwa ni ya kifo cha Kanumba, kwenye basi kanumba, mahospitalini kanumba, stendi kanumba, bar Kanumba, wakristo nao hawaelezi tena kufa na kufufuka kwa Yesu kristo bali nao wameshikwa na kifo cha Kanumba, kila kona ni Kanumba, Kanumba, Kanumba.
wengine wamejaribu kukurupuka na kusema msiba huu ni wa kitaifa.
Wengine wamekuja na wazo eti mwili wa Kanumba ukaagwe ktk uwanja wa Taifa.
Wengine tumewasikia wakikaririwa wakisema kwa nini hakufa Ray badala ya Kanumba?
...Stupid
Binafsi najaribu kuuangalia uwezo wa Kanumba kikazi.
Ni wazi kuwa Kanumba alikuwa ni msanii wa kawaida tu ila nyota yake pamoja na yale aliyowahi kukaririwa Baba yake akiyasema ndiyo yamefanya kijana huyu aonekane ni mkali zaidi hapa nchini.
Kanumba movie zake nyingi ni za kawaida na tumeshashuhudia movie zake nyingi zikikosolewa sokoni na wapenzi wa sanaa hiyo.
Haya ni lazima yasemwe hata kama katangulia mbele ya haki.
kwa miezi ya karibuni uwezo wa uigizaji wa hawa mahasimu wawili yaani Ray na Kanumba umepata ushindani mkubwa toka kwa mtu ambaye anaaminika kuwa yuko ktk chati ya juu kwa sasa, akifahamika kama JB ama Jacob Steven.
Je nini kimefanya Ray na Kanumba waporomoke ktk chati ile na kumpisha bila hiana JB?
binafsi kuna mambo matatu yaliyonifanya nimshushe Kanumba na kumdharau.
1. kwa siku za karibuni Kanumba alikaririwa akisema yeye hana mchumba na wala hanywi Pombe, lakini kifo chake kimedhihirisha kuwa Kanumba alikuwa ni Mzinzi na mlevi pia.
Hivyo ni wazi kuwa Kanumba alikuwa ni msanii muongo mwennye kutaka kuonekana msafi machoni mwa watu
2. Pia Kanumba kwa siku za karibuni amesikika akidai kuwa Baba yake pamoja na mama yake wa kambo walimtesa sana pindi alipokuwa anaishi nao.
Wenye akili wakahoji je walikutesa vipi?
Lakini likaja jibu kuwa Kanumba alipokuwa kwao alikuwa anachunga Mbuzi na kuosha vyombo.
Hayo ndio mateso ambayo Kanumba aliamua kumuanika Baba yake na kupelekea kutoelewana kati yao.
Hapa dogo alikosea...
3.Pia jamii iliamini kuwa Lulu ana uwezo mkubwa wa kuigiza.
Hivyo ilimkabidhi Kanumba mtoto huyo ili akisimamie kipaji cha mtoto huyo lakini Kanumba hakufanya hivyo bali alimtumbukiza mtoto huyo kwenye dimbwi la ngono.
Sasa je kwa machache hayo Kanumba kaifunza nini jamii inayovutiwa na kazi zake za sanaa?