[h=3]AliKiba kufia jela[/h]
a
ENDAPO itathibitika kuwa, ni kweli msanii wa Bongo Flava, Ali Saleh Kiba ‘Ali Kiba' anavunja amri ya sita na nyota mdogo anayetamba katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu', basi mwanamuziki huyo anaweza kuingia matatani ikiwemo kwenda jela maisha au kifungo cha miaka 30, Risasi Jumamosi limenyetishiwa.
Hilo linathibitishwa na baadhi ya Wanasheria wa Tanzania ambao waliongea na gazeti hili Alhamisi (juzi) na kutoa baadhi ya vifungu vya sheria ambavyo vinaweza kumweka pabaya Ali kiba a.k.a Kiba endapo tu itathibitika anacheza mchezo wa ‘baba na mama' na kinda huyo mwenye umri chini ya miaka 18.
Kufuatia kuwepo kwa hali hiyo huku Lulu akiwa hajafikisha umri wa kuamua kuwa na mpenzi, Risasi Jumamosi liliongea na Wanasheria, Dk. Ngali Maita, Sylvester Shayo na Issa Maige, ambao waliweka bayana kuwa, kufanya mapenzi na binti mwenye umri wa chini ya miaka 18 ni ubakaji hata kama msichana atakuwa ameridhia.
Mawakili hao waliweka bayana kuwa, kwa mujibu wa sheria za mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura ya 16 (The penal code, caption 16) pamoja na sheria ya kujamiiana ya mwaka 1998 (Sexual Offences Special Provission Act of 1998 (SOSPA) adhabu yake ni kifungo cha maisha (life sentence imprisonment).
Kuwepo kwa adhabu hiyo kunasisitizwa na Wakili Issa John Maige wa MJ Diamond Advocates ambaye aliweka kweupe kwamba, kwa mujibu wa sheria mpya ya ubakaji, mwanaume au mwanamke anayefanya mapenzi na mtu wa chini ya miaka 18 anahesabiwa kubaka hata kama wawili hao watakuwa katika ridhaa.
Alisema kuwa, kinachotakiwa kuwepo na mtu atakeyelalamika ili sheria ichukue mkondo wake ambapo ni pamoja na vyombo vya Dola kumtia nguvuni mhusika.
Katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Clouds hivi karibuni, Lulu alikaririwa akisema kuwa, mwananume anayeamini atamuoa ni Ali Kiba hivyo kuifanya jamii kuamini minong'ono ya mara kwa mara kuwa, wawili hao wanatoka kimapenzi.
Hata hivyo, kwa upande wake, Ali Kiba alipopewa fursa ya kulielezea hilo, alisema Lulu alikuwa anajifurahisha tu lakini yeye hana uhusiano na ‘sidanganyiki' huyo licha ya kukiri kwamba, wanafahamiana na wana ukaribu.
Sintofahamu kwa usiri wa wawili hao unazidi kujikunja na kisha kukunjuka kufuatia miezi ya karibuni, Lulu kufikishana Polisi Magomeni na mrembo aliyewahi kushiriki Miss Dar City Centre wakidaiana kuibiana simu lakini mlimbwende huyo alikwenda mbele zaidi pale alipoweka wazi kuwa, Lulu amekuwa akimwonea wivu akiamini yeye (mrembo) ana uhusiano wa kimapenzi na Kiba.