Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Haya ni matatizo ya mahakama zetu. Ingekuwa kwa wenzetu mtu anapelekwa chambers hata usiku ule ule wa Jumamosi!.

Uko sahihi mkuu Pasco,mtu anatakiwa kushikiliwa si kwa zaidi ya 24 hours,kabla ya kumfikisha mahakamani au kumrelease,cha ajabu jeshi letu la polisi kuna baadhi ya watu wana vikesi vya bangi na vya ajabu ajabu,lakini utakuta wanashikiliwa week kadhaha bila kufikishwa mahakamani alafu wanakuja kuwaachia
 
kanisa,shule na misikiti ya kazi gani?ushamba+nyege+pombe+sifa+anasa=kifo.kwani king majuto,mtanga,bambo n.k wako simple
 

Du!! Aisee..! Kazi ipo kumbe dogo alichezea kipigo...NN,nipe frequency za Times Fm.
 
Hilo la serikali kusaidia kwenye mazishi ya mtu mwenye uwezo na umaarufu mkubwaa kama msanii kanumba limeniuma sana hiyo ni moja ya kutafuta kura za vijana na wasanii. Hebu njoo kwenye kambi ya kuwalea wazee hapa misungwi machozi yatakutoka hiyo pesa ingetumika kuboresha nyumba na vyoo vya wazee hawa ambao hawawezi kuchuchumaa kujisaidia. Tunakwenda wapi na tabia hii na si kwa serikali tuu hata kwa jamii tunachangia maharusi lakini wazee hatuwakumbuki
 

Inavyosemekana kwa sasa maisha hayawezi kuendelea bila hii story ya marehemu Kanumba na Lulu, hamna Lema na ubunge wala CCM wamefanya nini? Wabunge wanatuwakilishaje, CHADEMA wanafanyaje! Yaani sasa hivi ni Marehemu na Lulu tu, kaaaaaaaaaaaaaaaaaaazi, kweli kweli.
 
````LULU amewahi kujinasibu kuwa ametimiza umri wa miaka 18. na kudai kuwa ana furahi kwasababu atakuwa anasaini mikataba mwenyewa badala ya kupitia kwa trustee............... leo vyombo vya habari vinaripoti tena kuwa ana miaka 17...,,,,,,,,,,,,!!! KULIKONI
 
Katika masiko ya wengi jina hili katika siku za karibuni ,limetumika sana wengine kwa mtazamo Hasi, na wengine chanya.

Mimi ningependa kumshukuru sana kijana Huyu, only 28, kwa kuweza kuinuana magogo na vigogo
wa kisiasa na hata wananchi wa kawaida, na hati aye wengi kumi na kile alichokuwa akili khamis kwa nguvu zake zote na hati aye mafnikio kuanza kuonekana, kwa mbali.

Kanumba hakuwa msomi, kwa maana ya madigirii mengi tu tena mengine ya uzamili na uzamivu!

Kanumba hakuwa mwanasiasa, ksema kuwa chama Fulani ndio kimempa nafasi katika kazi zote

Kanumba alikuwa kijana tu saw a na kijana yeyote

Kanumba hakutoka kwenye koo zenye pesa na zenye uwezo

Lakini,

Kanumba alipata vision Yake mwenyewe na alijitengeneze mission.

Kanumba alikuwa a relentless performer, striving to improve his own self katika yote aloyokuwa anafanya.

Kifo chake Kama mtanzania yeyote kime nitia simanzi kubwa kwani juhudi, mategemeo na ndoto zimezimika ghafla.

Hata hivyo kwamba mafanikio yake yamekuwa noticed na Marais, Mawaziri,viongozi serikalini,wabunge,wananchi wa kawaida, hili ni fundisho kubwa sana kw kila mwananchi na kwa nafasi yake.Je wewe unayesoma mada hii nawe wafanyakazi nini kufanikisha juhudi za vijana Kama Kanumba?

Na kwa kutuachia mafundisho hayo namshukuru sana na Mungu amuweke mahali .
 
Na nyie wa taarifa za ndani na nje si mseme?Ama ndo nyie na majina bandia mnazuga humu?
Mara nje mara ndani, duh!

Usijali mkuu,mimi nitatoa taarifa za pembeni soon. Stay tuned.
 
Upendo huwa wakati wa raha tu...palikobakia kila mtu anachunga mzigo wake

Ile ya marehemu ilikuwa ni raha? na kwa kuwa movie bado inaendelea basi wahamie upande wa lulu sasa, maana kipande cha marehemu mchezo wake uliisha mara baada ya mazishi yake, hila lulu movie yake bado inaendelea.
 
Juzi niliandika KIFO CHA KANUMBA FUNDISHO KWA VIJANA WA KILEO. Mimi sijawahi kuwa shabaki wa bongo movie. Huwa naangalia labda nikiwa kwenye vyombo vya usafiri. Ukiwa msomaji wa novel mbalimbali (sio za shigongo) na ukibahatika kuangali filamu za nje...mfano za Matt Damon, born identity, born supremacy. Au angalia The God Father. Kamwe huwezi shawishika kuangalia huu uozo wa bongo movie. Msanii unakuta anamiliki PRADO na kupanga nyumba ya mil 7 kwa mwezi hana hata kiwanja. Kazi yake starehe tu. Wasanii wa bongo usiku kwao ndio kumekucha, hawalali. Asubuhi unawakuta kwenye bar wanakunywa supu ya kongoro, yaani ni kinyaa tupu. Wasanii karibu wote wametengwa na wazazi wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…