Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

kuna la leo gazeti liliandika kuwa..baba mzazi wa kanumba awasili dar!
tuseme hakuna baba wadogo, baba wakubwa mpaka shibuda?
hata hivyo nilimsikia yule mzee(baba kanumba) akisema lazima kijana akazikwe shinyanga na kwa mujibu wa mila zao ingetakiwa apelekwe nyumbani kwa babu yake kwanza ndipo apelekwe makaburini maana jina la KANUMBA alirithi kutoka kwa babu yake!

hii mizimu ya wasukuma inaweza ikawarudia wote waliolazimisha SK azikwe DAR
 
Huo msiba uliishatekwa nyara na wahaya siku nyingi so usitegemee kitu chochote cha kisukuma zaidi ya ibada ya AIC kwa kuwa kanisa hilo huzika bila kuweka masharti magumu. Mama Kanumba alitumiwa ticket ya ndege huku baba akiachwa solemba. Wahaya bana...

Kwani mama Kanumba ni MHAYA?
 
Chanzo namba moja cha kifo cha Marehemu ni uzinzi, walikuwa wanafanya Uzinzi na Lulu na popote palipo na Uzinzi ni shetani tu ndiyo anatawala hilo eneo hakuna malaika mwema, sasa nitashangaa sana leo kama kwenye Ibada hao viongozi wa dini hawatakemea vitendo vya zinaa, kifo cha Kanumba ni kazi ya shetani.

mkuu kama we ungekuwa pastor ungeweza kusema hadharani?
 
kichefuchefu kinakusmbua na uongo wako mbona tangu jana yupo hapo msibani na alihojiwa na waandishi wa habari.

Mkuu jana alipohojiwa na TBC1 alikuwa nyumbani kwake Shinyanga.Kwa maelezo yake alitazamia kamati ya maziko ya mwanae wamfanyie utaratibu wa usafiri aweze kuwahi mazishi Dar.
 
Nimekuja kugundua kuwa,jamvini humu ni watu waachache sana wenye weledi na mambo ya kichunguzi..
Hakika lakini ndio vyema kuanza kupeana ufahamu,manake ndio hivyi dunia inabadilika na magonjwa nayo pia hivyo hivyo,ukweli ndio huo hata familia inalijua kuwa ni tatizo lake!!
 
Steven Kanumba kama alivyofahamika, kwa sasa ni marehemu.

Kifo chake naweza kusema kuwa kimewagusa watu weengi ukizingatia alikuwa ktk fani ya maigizo, na ni mmoja kati ya waigizaji ktk runinga anayetajwa kuwa maarufu sana hapa nchini na nchi za jirani.

Hakuwa msanii mkongwe, lakini amekuwa na nyota ya kupendwa na kuvuta hisia za wengi kwa kipindi hiki kifupi alichojiunga ktk fani hiyo.

Kifo chake pia kimekuwa faraja kwa vyombo vya habari hasa Televisheni na Redio ambazo hazina vipindi vya kueleweka.
Pia hata Magazeti ambayo hayana ya maana ya kuandika, nayo pia yamejaza picha za marehemu na udaku wa hapa na pale.

Kifo cha kijana huyu pia kimeita hata viongozi wa ngazi mbalimbali za kisiasa hapa nchini.
kimemuita mpaka Rais wa nchi na kumlazimu aahirishe safari yake ambayo ilikuwa na manufaa kwa taifa na kuja kujumuika ktk msiba.

Kila kona ya wasio na kazi au wasio na ya maana ya kufanya basi habari imekuwa ni ya kifo cha Kanumba, kwenye basi kanumba, mahospitalini kanumba, stendi kanumba, bar Kanumba, wakristo nao hawaelezi tena kufa na kufufuka kwa Yesu kristo bali nao wameshikwa na kifo cha Kanumba, kila kona ni Kanumba, Kanumba, Kanumba.

wengine wamejaribu kukurupuka na kusema msiba huu ni wa kitaifa.
Wengine wamekuja na wazo eti mwili wa Kanumba ukaagwe ktk uwanja wa Taifa.
Wengine tumewasikia wakikaririwa wakisema kwa nini hakufa Ray badala ya Kanumba?
...Stupid

Binafsi najaribu kuuangalia uwezo wa Kanumba kikazi.
Ni wazi kuwa Kanumba alikuwa ni msanii wa kawaida tu ila nyota yake pamoja na yale aliyowahi kukaririwa Baba yake akiyasema ndiyo yamefanya kijana huyu aonekane ni mkali zaidi hapa nchini.

Kanumba movie zake nyingi ni za kawaida na tumeshashuhudia movie zake nyingi zikikosolewa sokoni na wapenzi wa sanaa hiyo.
Haya ni lazima yasemwe hata kama katangulia mbele ya haki.


kwa miezi ya karibuni uwezo wa uigizaji wa hawa mahasimu wawili yaani Ray na Kanumba umepata ushindani mkubwa toka kwa mtu ambaye anaaminika kuwa yuko ktk chati ya juu kwa sasa, akifahamika kama JB ama Jacob Steven.
Je nini kimefanya Ray na Kanumba waporomoke ktk chati ile na kumpisha bila hiana JB?

binafsi kuna mambo matatu yaliyonifanya nimshushe Kanumba na kumdharau.
1. kwa siku za karibuni Kanumba alikaririwa akisema yeye hana mchumba na wala hanywi Pombe, lakini kifo chake kimedhihirisha kuwa Kanumba alikuwa ni Mzinzi na mlevi pia.
Hivyo ni wazi kuwa Kanumba alikuwa ni msanii muongo mwennye kutaka kuonekana msafi machoni mwa watu


2. Pia Kanumba kwa siku za karibuni amesikika akidai kuwa Baba yake pamoja na mama yake wa kambo walimtesa sana pindi alipokuwa anaishi nao.
Wenye akili wakahoji je walikutesa vipi?
Lakini likaja jibu kuwa Kanumba alipokuwa kwao alikuwa anachunga Mbuzi na kuosha vyombo.
Hayo ndio mateso ambayo Kanumba aliamua kumuanika Baba yake na kupelekea kutoelewana kati yao.
Hapa dogo alikosea...


3.Pia jamii iliamini kuwa Lulu ana uwezo mkubwa wa kuigiza.
Hivyo ilimkabidhi Kanumba mtoto huyo ili akisimamie kipaji cha mtoto huyo lakini Kanumba hakufanya hivyo bali alimtumbukiza mtoto huyo kwenye dimbwi la ngono.


Sasa je kwa machache hayo Kanumba kaifunza nini jamii inayovutiwa na kazi zake za sanaa?

Mkuu nimependa mawazo yako tofauti yanayoangalia upande wa pili wa marehemu Kanumba.
Mara nyingi mtu ukifa watu wanaangalia upande wa mazuri na kukusifia pasipo kuangalia upande wa pili. Leo hii hata kipofu akiendesha gari akapa ajali akafa watu tutaanza kumsifia pasipo kuhoji kwa nini kipofu aendeshe gari?

Tuwe wakweli tuangalie pande zote, hawa jamaa hawapaswi kumfanya lulu mpenzi wao, walihitajika kumuongoza katika sanaa kutokana na umri wake mdogo ili awe na mda mrefu zaidi kwenye sanaa.
 
kuhusu msanii wa magogoni watahudhuria wanao kula nae pesa za shoo.
 
Acha ujinga wa kutabir ww, inaweza ikawa wewe au ndugu yko. Kwan kififo anapanga mwanadam?
Sasa mimi ujinga wangu nini??Au umekurupuka kwenye pombe ya maharage nakuleta ushuzi wako hapa??soma contenti siyo unakurupuka ukikuta "MTI UMESIMAMA??"si utajitunga??
 
siasa mapaka misibani hii inatisha.
siku ya j1 kupitia clouds TV alihojiwa Asha Baraka kuhusu msiba na wageni waliofika bila shaka kwa aliyemskiliza kwa makini atakubaliana nami kuwa hajui Sinza Vatican ipo jimbo lipi na mbunge wake ni nani.Kwani alisema hata mbunge wa Kinondoni Idd Azan ameshawasili na tunae msibani utafikiri ndo mwenye msiba au guest of honor.Mnyika iliyekuwepo hakutajwa na wala alionekana hausiki kabisa.
Siasa mpaka msibani!
Alikuwa hajamwona Mnyika atasemaje kuwa naye yupo. Asha alikuwa hapokei wafiwa na wafiliwa kama wewe
 
mh hajafika! hata mimi nilimsikia akisema Kanumba akazikwe alipozikwa babu yake. Panapotokea msiba nani anakuwa na kauli ya mwisho marehemu akazikwe wapi? Jamaa hakuacha wosia akazikwe wapi, hivyo kuna jamaa wamejibebesha majukumu jamaa akazikwe wapi kwa maslahi yao wenyewe.
Mbona hilo lipo waz mkuu,ww angalia kamati yote ya mazishi ndugu wapo mwachache wengi walikuwa wasanii wenzake na marehem.
kuna siku nimesoma uzi hapa kuwa ile kamati ilikuwa inamsubir mama wa marehem ili wamshawish mazish yawe j4 Dar!
so nafikiri nafas ya familia kutoa maamuzi ilikuwa ndogo sana ni kama jeshi vile.
 
Si kweli kwamba wasanii wa filamu ndio hawakuzingatia malezi,bali wazazi ndio tatizo unapomwacha
mwanao kuingia mapema kwenye mambo yatakayomfanya ajione staa mapema,unategemea
atasoma kweli? na je akifika kwenye foolish age ataweza kuhimili changamoto za umaarufu?
jibu ni kuwa ukimruhusu mwanao kujiingiza kwenye kuigiza na kuwa maarufu tegemea kuwa na
mtoto aina ya Lulu hata kama angekuwa na akili kiasi gani.
 
Huo msiba uliishatekwa nyara na wahaya siku nyingi so usitegemee kitu chochote cha kisukuma zaidi ya ibada ya AIC kwa kuwa kanisa hilo huzika bila kuweka masharti magumu. Mama Kanumba alitumiwa ticket ya ndege huku baba akiachwa solemba. Wahaya bana...
Acha mawazo ya ukabila wewe! Msiba umetekwa na CCM na wasanii wenzake,usisingizie wahaya!
 
sijawai kukutana na swali la kushangaza kama hili hasa kwenye kipindi cha uzuni! wewe unazani utaishi milele! au unazani utaishi miaka mingi kama kobe? tafadhali badilisha swali.Amani kwako!
 
Back
Top Bottom