Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kaka/dada tatizo kwa Tanzania umaarufu hautokani na vipaji bali vituko vinavyo pelekea uandikwe andikwe kwenye magazeti ya udaki. Hebu niambie kama hawa wafuatao kweli tuta sema wana vipaji:
Wema, Lulu, Uwoya, Wolper, Jini Kabula, nk...hawa kweli kwa kuona uigizaji wao tunaweza sema wana kipaji cha kipekee? Je tuna weza hata taja movie walizo igiza? Au tuna wajua kutokana na vituko vyao?
Je ni wasanii wangapi ambao hawa andikwi kwa ubaya kwenye magazeti ya udaku ambao tuna wajua?
Huyu huyu Lulu mwenyewe kaanza kuigiza tokea akiwa mtoto wangapi mlimjua kabla hajaanza vituko?

Kwa hiyo kaka/dada kwa sasa Tanzania "masupastaa" hatuna au kama tunao ni wachache sana ambao umaarufu wao unatokana na vipaji vyao pekee. Sasa ukiwaambia waache vituko umaarufu watautoa wapi? Industry kwa sasa ina hitaji ufanye vituko ubaki machoni pa watu mpaka sasa tunaanza kusikia baadhi ya wasanii huuza habari zao wenyewe kwenye magazeti.

Ila hii inaweza ikawa ndiyo nature tu ya biashara ya burudani duniani. ANgalia hata Marekani. Kila leo wasanii/wanamuziki wana kufa vifo vya ajabu ajabu. Na hata huko wale wanao andikwa andikwa kwenye magazeti ndiyo wanaumaarufu zaidi. Mtu kama Kim Kadarshian ana kipaji gani?

Kwa hiyo ndugu zangu fame comes with a price. Wengi kabla ya kuupata wanaulilia lakini jamani madhara yake ni makubwa. Maisha ya kuwa mburudishaji na maarufu ni kazi sana na ni watu wachache sana wenye akili na maarifa ya kuweza kuhandle hiyo lifestyle. Maana mtu ukiona kipaji hakitoshi kukupa umaarufu kama unautaka sana utakua tayari kufanya chochote na lolote.
 
Yaani kwa mwendo huu TACAIDS wana kazi kweli!

Ninadhani huyu mheshimiwa ana "wapenzi wengine", na pia Kanumba alikuwa na "wapenzi wengine", na zaidi ni kwamba hao "wapenzi wengine" wana "wapenzi wengine" ambao wana "wapenzi wengine" ambao nao pia wana "wapenzi wengine" ambao wana....na hatimaye, huenda wewe pia ni mmoja wao wa hao "wapenzi wengine" na una "wapenzi wengine".

Duh! Kwa kweli, huu ni uteja wa mapenzi
 
......duh....
Yaani hizi sridi za LULU.....ngumu kama hesabu za log....unaweza chizika
 
Kwani ujui simu ya mwisho alipigiwa na kigogo? Huyo ndo anamlinda full stop.
 
hv mna uhakika na mnayo andika au mna tunga theory na kuzi publish humu. grow up pls! how valid are ur texts?
 
na kweli yatasemwa mengi, ingawa ningefurah sana kama ingekuwa kweli
 
mbona umeng'ang'ana sana na "ningefurahi"...uliwashikia miguu ama?
 
hana gari huyo binti ila alikuwa anatumia gari aliyohongwa na kigogo mmoja wa Chama Cha Matusi ambaye ni mbunge toka mkoa wa jimbo mojawapo mkoani Tanga.

hehee, hii kali sasa
 
Back
Top Bottom