Steven Kanumba kafakamia kilevi kikali cha "Jack Daniels", na bila shaka walevi wengi waliokubuhu wanaheshimu tofauti kati ya bia na vilevi vikali kama whisky ambavyo havikawii kumfanya mwanaume rijali wa umri wa Kanumba kuwa kama "mdoli" kwa urahisi sana hadi kupoteza sense of balance akitembea kwa hatua zake mwenyewe, achilia mbali kupoteza ufahamu na balance kwenye mazingira ya hamaki aka agression kwa mwanaume aliyelewa kilevi cha aina ya "Jack Daniels". Kwa hili naomba huyo "mkemia wa serikali" atoe toxicology report inayoweka wazi ni kwa kiwango gani haswa Kanumba alikuwa amelewa.
Ama baada ya kusema hayo, jee, kama ingekuwa Kanumba ndiyo kasababisha kifo cha "Lulu", hisia za Watanzania zingekuwa tofauti kwa kiwango gani, maana ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya Wanawake dunia nzima wanapoteza maisha mikononi mwa Wanaume, na ni nadra kwa ukweli huu kuwa kinyume.