Kifo cha Tabibu Dkt. Buberwa wa Herbal Products utata mtupu

Kifo cha Tabibu Dkt. Buberwa wa Herbal Products utata mtupu

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,390
B2.jpg



Wadau. Nafikiri mnamkumbuka huyu tatibu aliyekuwa maarufu Jijijini Dar Es salaam hasa miaka ya 2010 hadi 2017 .

Huyu mwamba amefariki dunia akiwa katika nyumba ya kulala wageni Jijijini Dodoma na tayari amezikwa Jijini Dar huku kukuiwa na utata wa familia ya mkewe aitwaye Riziki mwenyeji wa Kilimanjaro na ndugu wa marehemu. Mengine yatasemwa baadaye lakini tambua kuwa huyu mwamba amakwisha zikwa wiki mbili zimepita.

RIP DR Buberwa

Tazama video zake hapa.


Mrejesho no 1

Tukio lenyewe liko hivi.

Huyo Dr Buberwa aliingia msukosuko na mkewe huyo Riziki baada ya familia kuingilia kati juu ya mambo ya mali maana alikuwa na watoto 3 wa kike kwa huyo dada Riziki na mtoto mkubwa wa kiume mkubwa aliyekutwa wakati anaolewa.

Ilikuja kubainika kuwa huyo Dr buberwa mali zote ikiwemo maduka ya dawa, nyumba zote za Dar na huko kwao ukweni walikokuwa wamejenga zilkuwa kwa jina la mke huyo.

Tangu day one huyo mama anaolewa alikuwa na one mission ya mali na kumfilisi huyo dr.

Huyo mwanamke alikimbilia mahakamani kuonesha vielelezo baada ya ndugu kuchachamaa. Mahakama ilitoa hukumu na kuonesha Dr buberwa hakuwa na kitu chochote bali usajili wa kampuni ambaye naye huyo mama ana hisa ndani.

Hivyo Dr buberwa alifukuzwa hata kwa nyumba akaanza maisha mapya kupanga. Aliishi kwa msaada wa ndugu na akaanza kuzunguka mikoani kutoa huduma mbalimbali

Alianza kubadili huduma ikiwemo kuuza bidhaa za ulinzi kama cctv camera nk pamoja na mambo ya unabii.

Baadaye alianza kuugua magonjwa mbalimbali hadi kukatwa mguu mmoja. sijui chanzo cha ugonjwa uliosababisha ukatwe ila inasemekana ni kansa.

Kutokana na kuangaika mikoa mbalimbali mauti yalimkuta akiwa guest dodoma ambapo haijulikani kama aliuawa,alijiua au alikufa kifo cha kawaida. wahudumu walikuja kushtukia mteja wao hafungui mwishowe ikabanika amekufa.

Sasa ndugu walipopata taarifa walimtafuta mkewe naye akasema anazo taarifa. Wakakubaliana kuwa kwa kuwa maiti iko dodoma basi wapitie maiti waipeleke Bukoba direct kuzika.

Dadake na marehemu aitwaye Jen na ndg wengine walianza safari kuelekea dodoma lakini walipofika wakaambiwa maiti imechukuliwa na mkewe kwenda Dar.

Mzozo ulianza lakini hawa ndg walipitiliza hadi Bukoba huku mke akisema ameipeleka kwake ili aagwe then watarudisha mwili bukoba.

Huyu dada alianza visa na visa na mwishowe akashirikiana na mdogo wake na marehemu wa kiume wakazika huko dar.

Kule Bukoba wakasubiri wapeleke udongo ( kulingana na taratibu za mila zao) pamoja na watoto lakini udongo ulitumwa lakini huyo mama na watoto hawakwenda.

Ilikuja kubainika kuwa hadi mauti yanamkuta marehemu alishakuwa maskini wa kutupwa na hata yule kijana mkubwa alikuwa anaishi kwa huyo riziki hana chochote kile kutoka kwa baba.

Hitimisho.
Tutumie tukio hili kuishi vema na wake zetu siyo kwa kuwa huyu alikuwa mchaga bali dunia ya tamaa za mali imeongezeka sana.

Asante

Update ipo katika post no 228 uk wa 12
utasoma mrejesho no 2.
riziki2.jpg


riziki3.jpg

Mrejesho no 2
Maelezo ya Bi Riziki Buberwa yako wazi wakati akiongea na wawakilishi wa ndugu wa marehemu kwamba walianza kutafuta mali wote na walifunga ndoa na kupata watoto watatu .

Anasema kuwa hawakujua awali kama mumewe ana mtoto mkubwa.

Kwamba baada ya kutokea kutoelewana baina yao aliamua kwenda mahakamani kutafuta haki yake kisheria na mahakama iligawa mali sawa kwa sawa. Hata ofisi ya huduma za kitabibu iligawanywa kila mmoja akabaki na ya kwake.

Hivyo kila mmoja alianzisha maisha yake huku wote wakiwa na jukumu la kulea watoto

Anasema miaka kadhaa baadaye alikuja kugundua kuwa mumewe huyo amefilisika na hajui zile mali zake alipeleka wapi au kufanyia nini maana hata mtoto wake mkubwa alikosa mwelekeo. Aliamua kumchukua na kukaa naye.

Anasema maisha ya mumewe waliyetengana bila kuvunja ndoa yalikuwa hayaeleweki na kila mmoja aliishi kivyake hadi hapo mauti ilipomkuta akiwa dodoma.

Anasema taratibu za kumzika alizifanya yeye akishirikiana na badhi ya ndugu wa marehemu hasa mdogo wake wa kiume,watoto wake wote wanne na yeye.

'Dr Buberwa hakuwa na mama wala baba ,amezikwa na mkewe,baadhi ya ndugu zake na watoto wake wote hata mwanamke aliyezaa naye huyo mtoto alikuwepo' sasa mtasemaje familia yake haikuhusika?. alijibu wakati akihojiwa .

Kuhusu kutopeleka msiba bukoba Riziki anasema kuwa kulitokea sintofahamu iliyotokana na maziko ya mumewe lakini kwa sasa anajinga kupeleka msiba na watoto huko Bukoba.

Alipoulizwa alipo yule mtoto wa kiume kwa sasa amesema kuwa amepelekwa Morogoro kwa mamake.

Kuwajua vema wapendao hawa waliotikiza na kuvunja historia ya harusi za kifahari Jijijini Dar. unaweza kutazama hapa chini

grmproductiontz.blogspot.com

The Wedding of Dr Joseph Buberwa and Riziki N. Onja kidogo Jinsi mambo yalivyojiri!

Hakika Dr Joseph B na Riziki walipendeza sana. Nice Swagga la chungulia chini! Swagga la Pingu za mais...
grmproductiontz.blogspot.com
grmproductiontz.blogspot.com



Husikose mrejesho no 3
 
Mbona sura yake inaonyesha ni mtu aliyekuwa na maradhi sugu kama sio ukimwi ni kisukari
Kweli mkuu aliwahi kusema wazi kuwa ana kisukari na kudai kuwa moja ya dawa zake inatibu kisukari lakini yeye anataka ajifunze madhara ya kisukari hatajitibu.

Pia alijiita nabii kwa kutabiri mwisho wa dunia kimahesabu, hesabu zilizoangukia mwisho kuwa 2037 hivi..!
 
View attachment 1837507View attachment 1837508

Wadau. Nafikiri mnamkumbuka huyu tatibu aliyekuwa maarufu Jijijini Dar Es salaam hasa miaka ya 2010 hadi 2017 .

Huyu mwamba amefariki dunia akiwa katika nyumba ya kulala wageni Jijijini Dodoma na tayari amezikwa Jijini Dar huku kukuiwa na utata wa familia ya mkewe aitwaye Riziki mwenyeji wa Kilimanjaro na ndugu wa marehemu. Mengine yatasemwa baadaye lakini tambua kuwa huyu mwamba amakwisha zikwa wiki mbili zimepita.

RIP DR Buberwa

Tazama video zake hapa


Dodoma, tiba asili, nyungu .. niishie hapo nitaendelea baadaye.
 
Back
Top Bottom