Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Kwahiyo amevuna alichopanda?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwahiyo amevuna alichopanda?
Umechanganya taarifa boss, huyu sio wa harusi aliyeuza gari, bali ni wa mzigo bandari kavu. Lakini hata huyo wa gari ni nani ananunua gari bila kadi original?Watanzania tuna shida.
Yaani we ukodi gari la watu ukauze. Jamaa unewachukuliaje.
Mambo mengine yakujitakia.
Thanks again for the correction.Umechanganya taarifa boss, huyu sio wa harusi aliyeuza gari, bali ni wa mzigo bandari kavu. Lakini hata huyo wa gari ni nani ananunua gari bila kadi original?
Damu ya mtu ni ya kuiogopa sana,Soma Biblia kama story kuhusu Mungu akimwambia kaini!Damu ya ndugu Yako Abel inanililia.Kulilia kwangu ni muhisika pia kustahili ADHABu.Hii haikubaliki.Naomba nianze na taarifa yenyewe.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kuwa Daisle Simion Ulomi, aliyekuwa ameripotiwa kwamba amepotea, alifariki dunia baada ya kupata ajali mbaya na pikipiki aliyokuwa akiitumia siku ya Desemba 11, 2024.
Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 16, 2024 na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo SACP Jumanne Muliro ambapo ameeleza kuwa tarehe 11 Desemba, 2024 Jeshi hilo lilipata taarifa ya kupotea kwake na ndugu hawakuwa wanampata kwenye mawasiliano ya simu, baada ya yeye kuondoka ofisini kwake Sinza na kudai anaelekea Temeke kufuatilia makontena yake ya biashara.
"Ulomi aliondoka eneo lake huku akitumia pikipiki namba MC 415 DQC aliyokuwa akiendesha mwenyewe, ufuatiliaji umefanyika kwa kushirikiana na ndugu na kubainika kuwa Ulomi alipelekwa kituo cha afya cha Makuburi Ubungo External mchana wa tarehe 11 Desemba, 2024 baada ya kupata ajali mbaya na pikipiki aliyokuwa akiitumia, wasamaria wema walimsadia kumpeleka kwenye kituo hicho akiwa hajitambui na hakuwa na kitambulisho chochote," imeeleza taarifa ya Kamanda Muliro.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa, " Baadae alipelekwa Mwananyamala hospitali na ikabainika tayari alikuwa amefariki na maiti yake kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo kama mtu asiyefahamika akisubiri kutambuliwa na ndugu, ndugu tayari wameutambua mwili huo ukiwa na majeraha maeneo mbalimbali ya mwili. Aidha, Pikipiki aliyopata nayo ajali pia imepatikana ikiwa imeharibika. uchunguzi zaidi wa ajali hiyo unaendelea na taarifa zaidi itatolewa,".
#EastAfricaRadio
Maswali
Kwahio Afisa wa TRA ni kweli alipiga simu? Ni kweli kulikua na mawasiliano kati yake na Afisa wa TRA? Mbona baada ya "Afisa wa TRA" kumkosa (maana hakufika alikoitwa) hakuchukua hatua Yoyote ya kumpata "mteja" wake? Iko wapi simu ya Ulomi? Nani hasa alimpigia Ulomi kwenda bandari kavu? Mawasiliano ya mwisho ilikua chang'ombe, hapo jirani kuna hospital ya Temeke, why apelekwe Makuburi External?
Kwa maswali haya, Polisi wanakua Kwenye nafasi nzuri ya kujibu, wapi Ajali ilitokea, namna Ajali ilivyotokea (kugongwa au kugonga au kuanguka mwenyewe), huyu msamaria mwema ni nani hasa? Alitumia usafiri gani kumfikisha "Makuburi health Centre?"! Kutoka Makuburi (Ubungo) Hadi Mwananyamala kuna hospital kadhaa, mojawapo ikiwa ni Sinza Palestine, ambayo ina uwezo pia WA kupokea maiti, why wafunge safari ndefu Hadi Mwananyamala?
PIA SOMA
- TANZIA - Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala
Kama Polisi ndio walioupeleka mwili Huko, mbona hawakutoa taarifa kwa umma, na mitandao yote iliandika kuhusu kupotea kwa Ulomi? YAANI Polisi walikaa na taarifa Hii Hadi "alipopatikana" kwenye mafriji ya Mwananyamala.
Kama Polisi Wanakiri kuwa Ulomi hakua na Kitambulisho, LAKINI si alikua na Bodaboda "iliyopata Ajali"? Walishindwaje kuangalia usajili WA Bodaboda Kwenye mfumo wa TRA na kumtambua mmiliki? Ina maana angezikwa na Manispaa kwa kua hakua na Kitambulisho?
Kwangu Mimi hii taarifa imenipa mashaka Sana kuliko majibu.
View attachment 3178202
Sasa hapo Amani Kwa maskini itatoka wapi nae ana Njaa?Taabu kwa wote .Nchi hii
1. Ukiwa na mfanyabiashara tabu.
2. Ukiwa mwanaharakati tabu.
3. Ukiwa mwanasiasa wa upinzani tabu.
4. Ukiwa mkosoaji tabu.
Mtu pekee anayeishi kwa amani hapa Tanzania ni maskini aliye mpumbavu
Hata huyo "mpumbavu" hana nafuu anapo ingia kwenye maandamano ya CHADEMA kwa "upumbavu" wake.Nchi hii
1. Ukiwa na mfanyabiashara tabu.
2. Ukiwa mwanaharakati tabu.
3. Ukiwa mwanasiasa wa upinzani tabu.
4. Ukiwa mkosoaji tabu.
Mtu pekee anayeishi kwa amani hapa Tanzania ni maskini aliye mpumbavu
Duh 🙄 umesoma kinyume au una majibu yako tuuu. Hii taarifa umeitoa wapi??Watanzania tuna shida.
Yaani we ukodi gari la watu ukauze. jamaa umewachukuliaje.
Mambo mengine yakujitakia.
what if hio mamlaka ya uteuzi ndio imemtuma?>Kamanda wa political Kanda Maalumu ajiusulu au aondolewe na mamlaka ya uteuzi kwa kutoa taatifa za uongo na isio na welding kwa Emma.
Afikishwe mahakamani kwa kuficha taarifa na kutoa taarifa za uongo kinyume na kiapo chake cha uteuzi
Huyu nae anaongea tuu!whai if hio mamlaka ya uteuzi ndio imemtuma?>
Usichokijua ni kwamba hata hao wasamaria wema wakishamgikisha mgonjwa hospital wanatakiwa kitoa taarifa polisi na Kuna hospital nyingine mgonjwa wa ajali hawamdhughulikii kabisa mpaka ipatikane PF3.Ajali ikitokea siyo rahisi majeruhi kumkuta na kitu chochote mfukoni Kwa sababu ya uporajinna hilo ni jambo la kawaida
Ofisa wa tra baada ya kumkosa ulomi aliwasiliana na mkewe na kukubaliana zoezi husika lifanyike siku inayofuata
Kuhusu wasamaria wema Huwa wapo tu na siyo lazima wajitambulishe wanapomfikisha majeruhi hospital
Nimekuelewa kakaMkuu muda mwingine kodi inapokua kubwa mwenye mzigo anatafuta nafuu ya kulipia huo mzigo kwa kupitia hizo njia nadhani wa Ilemi umeelewa Agent anatumika kujaza kila kitu mpaka kwenye hatua ya malipo ila kabla hapo Wasizwa wanakaa kuweka mazingira mazuri ya kodi nafuu..
Hongera Viongozi wetu. Msife moyo Mungu atawababriki kwa jinsi mnavyojitoa kwenye Mazingira magumu.
Ametoa taarifa bila kutumia weledi wa kazi yake na kuacha matundu mengi yenye kutia shaka na kudhalilisha mamlaka husika.what if hio mamlaka ya uteuzi ndio imemtuma?>
Hata yale majibu ya ofisa wa TRA kuhusu wao kufanya kazi na Agent wake utapata jibu pale maana mzigo haujatoka kisa cha yeye kufatilia ilikua ni nini? Pana vitu vingi sana hapo mkuuNimekuelewa kaka
Ili wajue tu kuwa watanzania wa Leo sio MAZOMBI kama wao walivyo.Mtauliza na hamna cha kufanya na mtu ndio keshapotea
Mtiririko wa simu zake zote za mwisho ziwekwe hadharani tutapata majibuKazi ya kutoa mgonjwa hospitali ni ya polisi? Kwani wamekua ambulance? Maana mgonjwa akishakadhiwa hospitali ni jukumu la madaktari. Je wao walimsafirishaje? Manifest ya kumtoa ubungo external ipo wapi?
Chawa kama mwijaku baba levo doto magari juma lokole: na chawa wengine wengi kama kina Lukas Mwashambwa, hoa ndio wanaoishi bila wasiwasi tz ya sasaNchi hii
1. Ukiwa na mfanyabiashara tabu.
2. Ukiwa mwanaharakati tabu.
3. Ukiwa mwanasiasa wa upinzani tabu.
4. Ukiwa mkosoaji tabu.
Mtu pekee anayeishi kwa amani hapa Tanzania ni maskini aliye mpumbavu