Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Ahsante kwa kuniami
Ahlan wa sahlaan!
Kwa uelewa wangu,kuamini hakuhitaji factual knowledge
Ni kweli. Kwa sababu ukishakuwa na ukweli au uhakika wa kitu au jambo inakuwa siyo kuamini tena. Inakuwa ni kujua au kufahamu. Na ukishajua au ukishafahamu huwezi tena kuamini maana sasa unajua na/au unafahamu.
Lakini kuamini kwenyewe wala hakuna shida yoyote ile. Hakuna shida kwa sababu asilimia kubwa ya kuamini ni kufikiri na kujishawishi tu.
Hata mimi wakati mwingine huwa najishawishi kwamba mimi ni Superman, He-man, na Santa. Lakini kiukweli kweli mimi si Superman, He-man, Popeye the Sailor Man, wala Santa.
Mtu anaweza kuamini chochote anachotaka,lakini ili ujue lazima uwe direct perception pamoja na uelewa wa hicho kitu
Direct perception ndo nini?
Labda nikuulize wewe,
We niulize chochote tu....😉.
Unaamini kuwa Mungu hayupo au unajua kuwa Mungu hayupo?
Mimi kwa kweli sijui kama mungu hayupo.
Sina hakika kama hayupo na vilevile sina hakika kama yupo.
[utanisamehe kama wewe ni theist]
Kwa rejea za mijadala ya huko mbeleni, napenda kukufahamisha kuwa mimi ni agnostic.