Kifo hakipangwi na Mungu

Ahsante kwa kuniami

Ahlan wa sahlaan!

Kwa uelewa wangu,kuamini hakuhitaji factual knowledge

Ni kweli. Kwa sababu ukishakuwa na ukweli au uhakika wa kitu au jambo inakuwa siyo kuamini tena. Inakuwa ni kujua au kufahamu. Na ukishajua au ukishafahamu huwezi tena kuamini maana sasa unajua na/au unafahamu.

Lakini kuamini kwenyewe wala hakuna shida yoyote ile. Hakuna shida kwa sababu asilimia kubwa ya kuamini ni kufikiri na kujishawishi tu.

Hata mimi wakati mwingine huwa najishawishi kwamba mimi ni Superman, He-man, na Santa. Lakini kiukweli kweli mimi si Superman, He-man, Popeye the Sailor Man, wala Santa.

Mtu anaweza kuamini chochote anachotaka,lakini ili ujue lazima uwe direct perception pamoja na uelewa wa hicho kitu

Direct perception ndo nini?

Labda nikuulize wewe,

We niulize chochote tu....😉.

Unaamini kuwa Mungu hayupo au unajua kuwa Mungu hayupo?

Mimi kwa kweli sijui kama mungu hayupo.

Sina hakika kama hayupo na vilevile sina hakika kama yupo.

[utanisamehe kama wewe ni theist]

Kwa rejea za mijadala ya huko mbeleni, napenda kukufahamisha kuwa mimi ni agnostic.
 
That's logically impossible

Kama tukikubaliana kuwa sisi wanadamu tuna uwezo wa kuchagua
Basi kufanya maovu pia ni moja ya chaguo

Sasa dunia isiyo na maovu na mwanadamu mwenye uwezo wa kuchagua havichangamani[coexist]

Kwasababu kufanya maovu ni chaguo pia
Kuumba ulimwengu usio na maovu ni sawa na kumuondolea mwanadamu freewill
 
Nyani Ngabu said:
Direct perception ndo nini?
Nilisahau kuweka kiunganishi
Ili ujue lazima uwe na direct perception au cognition

Lazima uwe na uelewa mpana wa hicho kitu
That was my stance

Mimi kwa kweli sijui kama mungu hayupo.

Sina hakika kama hayupo na vilevile sina hakika kama yupo
Huwa napenda philosophical basis ya agonostics
Kwa sababu wapo tayari kwa matokeo yoyote
Aidha Mungu yupo au hayupo!

Kwa rejea za mijadala ya huko mbeleni, napenda kukufahamisha kuwa mimi ni agnostic.
Hahaa

Nashukuru kama wewe ni agnostic maana atheists ni wabishi kana kwamba wamesearch ulimwengu mzima na kupata uhakika kuwa Mungu

Japokuwa wao si omnipresents
 
Vipi kuhusu wale watu wenye genetic predisposition to violent behavior?

Nao wana uwezo wa kuchagua kutofanya maovu?

Kwamba nikujibu kama naamini au najua kama Mungu yupo?

Niseme hivi...naamini kuwa Mungu yupo kupitia uzoefu wangu binafsi na kupitia kwa watu wengine.

Natamani niseme najua kuwa Mungu yupo lakini sitaki niseme hivyo kwa leo.
 
Case closed!
 
Mungu katuumba na utashi (free will) tofauti na mimea na wanyama. Ile kuamua jema na baya. Unaweza kuamua kuishi au kufa.

Huwezi kumpangia Mungu. Hivyo ndivyo alivyoamua mfumo wa ulimwengu uwe. Kwamba kaumba dunia lakini katuachia jukumu sisi wanadamu tuamue jinsi gani dunia iwe....ama nzuri ama mbaya.

Kuna shida gani hapo?
 
Huwa napenda philosophical basis ya agonostics
Kwa sababu wapo tayari kwa matokeo yoyote
Aidha Mungu yupo au hayupo!

Yup....we are open-minded, rational, and reasonable!

Nashukuru kama wewe ni agnostic maana atheists ni wabishi kana kwamba wamesearch ulimwengu mzima na kupata uhakika kuwa Mungu

Mimi naona atheists ni bora mara mia kuliko theists.

Walau atheists wanatumia akili/ mantiki katika kupinga uwepo wa mungu.

Theists wao ni mwendo wa hisia na mambo ya kufikirika tu. Matumizi yao ya akili ni kidogo sana. Wengine hata tofauti ya kujua na kuamini hawaijui.
 
Sijataka kumpangia mungu wako, nataka kujua kama unamuelewa na mimi kumuelewa pia. Kwa sababu kwa sasa hivi ha make sense.

Habari ya kwamba mungu katuumba na free will si kweli.

Mimi nataka kurudi 1982, siwezi kurudi. Free will iko wapi hapo?

Utaona kwamba ulimwengu hauna complete free will. Kuna mambo hatuwezi kufanya.

Sasa kama ulimwengu umeumbwa kuna mambo hatuwezi kufanya, kwa nini mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya, maovu, majanga, magonjwa etc hayawezekani?

Hujajibu hili swali.

Ukisema "huwezi kumpangia mungu, hivyo ndivyo alivyoamua", unachoniambia hapa ni kwamba huwezi kujibu swali langu.

Kama huwezi kujibu swali langu, huelewi unachokiamini.

Kama huelewi unachokiamini, inawezekana kabisa unachokiamini kama mungu hakipo.
 
Mkuu hakuna andiko Mungu linalotaka watu wamwelewe ila maandiko yanataka watu wamwamini na siyo kuelewa ukijua kutofautisha hayo maneno mawili basi hutakuwa na tatizo,, tena anataka uchague kumwamini au kutomwamini wala hakulazimishi
 
Kwa nini wamuamini na si kumuelewa?
 
Mkuu hakuna andiko Mungu linalotaka watu wamwelewe ila maandiko yanataka watu wamwamini na siyo kuelewa ukijua kutofautisha hayo maneno mawili basi hutakuwa na tatizo,, tena anataka uchague kumwamini au kutomwamini wala hakulazimishi
Nani kasema nafuata andiko la mungu?

Mimi hata sikubali uwepo wa mungu, nitafuata vipi andiko la mungu?

Ukiamini bila kuelewa una tofauti gani na msukule?
 
Sasa kama hutaki kusoma maandiko yanayomhusu Mungu utaelew vp mkuu,, nimekwmbia hakuna lazma ni uamzi wwe kama hukubali basi fanya shuguli zingine tuachie Mungu wetu
 
Honestly....sina majibu. Hata mimi wakati mwingine huwa najiuliza hivyo hivyo.
But in the end, I choose to (cautiously) believe.
 
Sasa kama hutaki kusoma maandiko yanayomhusu Mungu utaelew vp mkuu,, nimekwmbia hakuna lazma ni uamzi wwe kama hukubali basi fanya shuguli zingine tuachie Mungu wetu
Nani kasema hataki kusoma maandiko yanayomhusu mungu?

Wewe umesoma vitabu gani vinavyomhusu mungu?
 
Kwa imani yangu nasoma biblia ndiyo guide yangu ya kuimarisha imani yangu, nakuombea kiranga upate pia muda wa kumwamini Mungu kabla hujaondoka duniani,, narudia kusema 'swali kuhusu Mungu halina jibu' unapaswa kumwamini basi
 
Siku zote nilikuwa nadhani naongea na Mtu mzima kumbe toto la mwaka 1982?

Ndio maaana nilikuwa nashindwa kuelewa Kosa lako ni nini.
Kumbe toto dogo bado.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…