Kifo kabla ya uzee, ni mpango wa Mungu?

Kifo kabla ya uzee, ni mpango wa Mungu?

Naomba uniambie ni wapi katika Qur'an ambapo mtu alikufa tu in a good will pasipokuwa na either mistakes alizofanya au mistakes zilizofanywa na kizazi chake
Kwanza mtu hapati hukumu kutokana na yale waliofanya watu fulani au kizazi chake.

Kabla sijakujibu kwanza kiri ya kuwa Qu'an huijui ili nikusaidie.
 
Kama kila kifo ni Mipango ya mungu kwanini mtu akimuuwa mwenzake inakuwa kosa.
Inakuwa kosa sababu hairuhusiwi mtu kuiua nafsi ya mwenzie kwa dhuluma.
Na huyo muuaji wakati huo anakuwa ni sababu ya kupatikana kifo au kumuua mwenzake.

Kosa la mauwaji linakuwa pale pale.
 
Inakuwa kosa sababu hairuhusiwi mtu kuiua nafsi ya mwenzie kwa dhuluma.
Na huyo muuaji wakati huo anakuwa ni sababu ya kupatikana kifo au kumuua mwenzake.

Kosa la mauwaji linakuwa pale pale.
Tunaamini kila mtu amepangiwa kifo cha dizaini yake ,wengine wanapigwa risasi,wengine visu,wengine wanaenda na mafuriko nk....saaa kama tunajua hivyo kwanini mtu akimchoma mwenzake kisu tusiseme ni maandiko yametimia tu.....
 
Tunaamini kila mtu amepangiwa kifo cha dizaini yake ,wengine wanapigwa risasi,wengine visu,wengine wanaenda na mafuriko nk....saaa kama tunajua hivyo kwanini mtu akimchoma mwenzake kisu tusiseme ni maandiko yametimia tu.....
Sisi huwa tunasema Qadar imetimia.Yaani lile alilolikadiria Allah limetimia.
 
Kwanza mtu hapati hukumu kutokana na yale waliofanya watu fulani au kizazi chake.

Kabla sijakujibu kwanza kiri ya kuwa Qu'an huijui ili nikusaidie.
Unamaanisha nini? Wakati unajua kabisa kuwa sisi binadamu na hata kifo ni matokeo ya dhambi ambayo walifanya babu zetu Adamu na Hawa
 
Unamaanisha nini? Wakati unajua kabisa kuwa sisi binadamu na hata kifo ni matokeo ya dhambi ambayo walifanya babu zetu Adamu na Hawa
Thibitisha hilo.Pili mimi imani yangu ndio inanifundisha ya kuwa haukukiwi mtu kutokana na madhambi ya watu waliopitwa.Wao watalipwa na yao na sisi halikadhalika.
 
Naona hili neno limekuwa likitumika sana katika kutoa faraja kwa watu, utasikia mtu anamwambia mwenzake, "Pole sanaa ni mipango ya Mungu" ikiwa ni njia ya kumfanya mtu aone hilo jambo ni la kawaida na ni mipango ya Mungu mtu huyo kufa.

Siamini kwamba kila kifo ni mpango wa Mungu.

Imani yangu ni kwamba Mungu katuumba tuishi na tuzeeke tufe.

Mifano ya watu wote walioishi katika njia za Mwenyezi mungu kwenye vitabu vitakatifu inaniambia walizaliwa wakaishi wakazeeka wakafariki wakiwa wenye umri wa kutoendelea kuishi tena. Vifo vya namna hiyo hata mimi naamini ndio mpango wa Mungu.

Mtoto wa miaka minne, ameugua maralia, wazazi wamechelewa kumpeleka hospital au amepelekwa madakatar wakakosea katika vipimo akafa, watu wanasema ni mpango wa Mungu.

Juzi ajali ile ya mabasi ya city boys, dereva badala ya kuendesha kwenye njia yake, kapita njia ya mwenzake watu 42 wakafa tunasema ni mpango wa Mungu kwamba alipanga watu wale 42 wafe siku hiyo.

Unajenga nyumba kizembe zembe mtu anakaa anaangukiwa na ule ukuta unasema ni Mpango wa Mungu.

Nilikuwa naangalia records za vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa upande wa marekani na Tanzania, nikazifanyia comparison, Marekani wana idadi ndogo sanaaaa ya watoto wanaokufa chini ya miaka 5 wakati Tanzania idadi hiyo ni kubwa sana, kwanini? Marekani uangalizi wa watoto wadogo ni mkubwa sana na hata matibabu yake ni ya uhakika wakati Tanzania uangalizi kwa watoto wadogo na matibabu yake ni ya kubahatisha. Je vifo vya hawa watoto ni mpango wa Mungu?

Hivyo hivyo ukiangalia hata hapa kwetu, vifo vya watoto wadogo Masaki na vifo vya watoto wadogo Mbagala utaona kuna ratio ya 1:10 au zaidi ya hapo, Je ni mpango wa Mungu kwamba watoto wengi wafe Mbagala na sio Masaki?

Unaendesha bodaboda kwa speed unaanguka unakufa unasema ni mpango wa Mungu, Mtu katoka huko anaendesha gari lake bila kuwa makini anamgonga raia mwema aliyesimama pembezoni mwa barabara tunasema ni mpango wa Mungu,

Hapana, huo sio mpango wa Mungu, Ni mpango wa binadamu.

Hata katika biblia na Qur'aan ukisoma kama kuna kifo ambacho kilitokea kabla mtu hajazeeka basi fuatilia kuna UZEMBE aliufanya mahali fulani au yeye au wazazi wake wakapelekea akafa.

Kwa kusema hayo, ni imani yangu na ninaomba niwashawishi kwambaa, vifo kabla ya uzee vinaepukika, kutokana na mazingira, kulinda afya yako, namna unavyoishi na watu unaweza kuepuka vifo ambavyo sio mpango wa Mungu.
Kifo chochote kile si mpango wa Mungu
 
Yakupasa kufahamu kuwa Mungu ametuumba kwa makusudi yake anayoyajua yeye mwenyewe

Kila binadamu huwa anashughuli ambayo amekuja kuitimiza duniani ambayo kwa akili zetu wanadamu hatuwezi jua hasa hilo kusudi la mungu ni lipi

Hiyo hata mtoto mchanga akifa huwa kunakusudi flani la Mungu limetimia tayari Na kazi iliyomleta duniani ameahaimaliza ndomaana inabidi afe bila kujali ni ajali au magonjwaa

Katika nnchi zilizoendelea vifo ni vichache kwa watoto chini ya miaka 5 kulinganisha na nnchi maskini lakin hii sababu haitoshi kusema kuwa kifo sio mpango wa Mungu kwani hata huko katka nnchi zilizoendelea kuna kilaaina ya kudhibiti uzembe ili watu wasife lakini bado wanakufa tu. Hii inamaanisha mtu hawezi kukikimbia kifo kwakuwa makusudi ya Mungu yameshatimia hana budi kufa tu.

Kifo ni mpango wa Mungu bila kujali uzembe unaosababishwa na wanadamu wengine.
Fafanua na hili kaka MTU kalituma jini lije likuue halafu akafanikiwa je huo ni mpango wa mungu?
 
Huu ubishi ulishaua mtu mtaani kwetu, jamaa 1 anasema kifo hasababishi Mungu, wa pili anasema anasema anasababisha Mungu.
Jamaa 1 kwa mfano nikichukua kisu nikuue sasa hv utasema Mungu kapanga?
Jamaa 2 ndio
Jamaa 1 nikikuacha he
Jamaa 2 Mungu kapanga usiniue
Jamaa 1 nikikuua
Jamaa 2 Mungu kapanga
Mwishoni jamaa 1 akamuua mwenzake
 
Back
Top Bottom