Kifo kinatisha kwa sababu hatujui kule tuendako

Kifo ni hitimisho ya maisha yako hapa duniani,na hakuna anayekipenda.Na kikimfika mtu,haimaanishi kwamba ameenda mbinguni wala wapi,bali kila kitu kinakuwa kimeishia pale pale.Kutokana na hofu ya kifo,inatufanya kujipa matumaini ya kuwa tunaenda mbinguni n.k ili kujifariji.Ila ukweli hakuna cha mbingu wala nini.Ni sawasa na mende amekufa akaliwa na sisimizi,hata binadamu ni hivyo hivyo.Chamuhimu tu tuishi kwa wema tukijua tunapita
 
Sheikh wewe ni AHMADIYYA? Moto ni wa milele au ni muda (temporary) kwa fiqh za kisunni?



Common sense tu inahitaji kuona Mungu akiwa muadilifu,mwenye huruma, mrehemevu,mkarimu nk, zaidi kuliko binadamu, iweje mtu atende makosa, mfano wizi nk, mahakama za duniani zimuhukumu kifungo cha miaka kadhaa na akishamaliza kifungo anakuwa huru, lakini eti Mungu amuingize mkosefu motoni MILELE kwa makosa aliyotenda kwa muda fulani kipindi alipoishi hapa duniani !!??. Where is the absolute justice??!!

Hiyo "adhabu" ya moto ni kutokana na mapenzi na huruma yake, mfano ni kama vile mzazi kumpatia Quinine au muarubaini mtoto wake anayeugua malaria.

Qur'an na hadithi zinaunga mkono kuwa jehanamu siyo ya milele ila itakuwa "Abadan" yaani ya muda mrefu sana.
 
Kifo ni starehe , subiri kama unavyosubiri x- mas au mwaka mpya . Unaachana na haya maujanjajanja ya duniani . Tulitishwa na wamisionary kuwa kuna motoni na mbinguni hivyo hofu ni moto .
 
Hii mada ni nzito na sintofahamu yakutosha
Kwa uelewa wangu kifo ni kama ganzi ya ufamu isio eleweka na kuishia hapo ki dunia ndivyo navyo fahamu kiroho haina record kamili japo akili tunazo kwanini tusifanye kityu.
 
hv JF hakuna aliyekufa aje atupe updated kuhusu kifo ?



Usingizi ni nusu ya kifo, huna haja ya kumtafuta aliyekufa na kufufuka ili aje akusimulie kifo ninini!

Weka fikra zako unapolala usingizi na usiamke tena ukiwa katika hali hiyo, tofauti ni hii kwamba usingizi ni "kifo chepesi" ambapo mtu huamka baada ya kulala na akaendelea na shughuli zake na kifo ni usingizi mzito (too deep sleep) ambapo mtu hawezi tena kuamka hadi siku ya Akhera.

Kwa hiyo unapotafakari kuhusu usingizi hapo utapata kujua angalau kifo kinafananaje (resemblance).
 
Kinachitisha kwenye swala la kifo siyo kifo chenyewe, ni namna au manner ya namna kifo chenyewe ambavyo huwa kinakuja kwamba lazima upitie taabu na /au maumivu makali. Ingekuwa watu wanafariki pasipo maumivu yoyote let's say wakiwa hata usingizini, wachache sana wangeogopa kifo!
 
Uislamu ni dini ya mapokeo hususan ktk mambo ya ghaibu, yaani tunaamini kuran yote na Hadith sahihi zote tena si kwa uewelewa wetu bali kama walivyoelewa Maswahaba Allah awaridhie wote. Huu ni msingi muhimu sana ktk dini ya uislamu. Kwahivyo basi kwa mujibu wa Quran na Sunnah kama walivyofahamu Maswahaba Allah awaridhie wapo watu watakao kaa motoni MILELE na wapo watu watakaa motoni kwa muda fulani kisha watatolewa humo na kupelekwa motoni.
 
Mkuu umetisha sana
 
Mkuu naomba umalizie wanaokwenda upande wa pili please.
 
Ha ha haa

JF raha sana yaan nimejikuta nimecheka kwa Nguvu afu katikati ya watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…