Rai yangu kwa CDM na vyama vyote vya upinzani, makosa mawili hayafanyi jema moja. Tumeshaona kuchanganyikiwa kwa CCM kiasi wamefikia pahali tayari wanaua na kuwatesa wale wasiokubaliana nao kwa ajili ya kubaka madarakani; vyama vya upinzani visiwe tayari kufa kwa ajili ya kuingia madarakani. Kama tunavyoona, wanaokufa ni raia wa kawaida na sio viongozi, na hata kama wanaokufa au watakao uliwa ni viongozi, bado taifa linawahitaji. Busara itumike. CCM wameshaonja damu, hawatasita. Tusiwaridhishe kwa yale wanayoyataka. Tutafute njia mbadala ya kupambana nao bila ya kupoteza maisha ya watu wasio na hatia kwani tukifanya hivyo itakuwa hakuna tafauti baina ya mjinga na mwenye akili.
Umezungumza la Msingi... mie mtazamo wangu ni kuwa hata kama Serkali inaonekana ndio inahusika moja kwa moja kuwa kupelekea vifo na kujeruhi raia bado ukweli unabaki kuwa hata CHADEMA Inabidi watambue kwa njia moja ama nyingine wanahusika moja kwa moja; tena positively na negatively...
Hawana haja ya kuendeleza shughuli zao kwa ili mradi wananchi kwa kiasi kikubwa wanawaunga mkono, inabidi wawahakikishie usalama hao wana nchi kwa kuweza kufanya njia zozote ambazo zaweza epusha vurugu na hatimae vifo vya wananchi...
AJ umeongea meengi kwa kina na msingi tena kwa kugusa hasa kitu gani humfafanua mwanadamu... In a way inagusia lile ambalo nimeandika katika moja ya bandiko hapo juu, kuwa wamefanya kazi yao kwa kuikumbatia na kufurahia sababu hata kama 'Amri' waliopewa ni nenda kakomeshe vurugu (Sidhani kama walisisitizwa kuwa lazima mmtese sana mtae mkamata... Hata hivo mim na wewe hatuwezi kujua)
Umegusia swala la unyama na jinsi gani inaweza kuwa vigumu kumrudisha mtu katika mstari kuwa mwanadamu wa kawaida na utu ndani yake. Naomba niseme kuwa sio kila mwanadamu kabahatika kuwa na akili yake timamu ya maamuzi kuegemea na kugubikwa na busara... Kuna watu wanaendeshwa kabisa kama mtoto mdogo hasa katika kazi ambazo watu hufanya kazi kwa makundi.
Pamoja na kusema kuwa askari katika hili wana tatizo - nadiriki kusema kama walivosema wadau wengine kama Nguruvi hapo nyumba kuwa tatizo lipo kwa uongozi wa juu na wao ni kama vidagaa. Kama IGP, RPC na Waziri wa Ulinzi wangesimamia/wangekuwa wanasimamia hili swala kwa manufaa ya wananchi hata waliopoteza maisha yao wangekuwa bado wapo miongoni mwetu. Walau thats what i think.
:caked:Hoja yangu kwenu wakuu AshaDii na MAMMAMIA ni moja tu;
Kwa mawazo yenu mnadhani ni kwa namna gani Chadema wanaweza kuepusha kabisa mauaji haya yanayofanywa kiholela na jeshi la polisi kwa kusukumwa na amri za wanasiasa wa ccm ambao hawako tayari kuona wakiondolewa madarakani.Na wakati wanapojitahidi kuhakikisha kwamba hawawi chanzo cha haya mauaji basi wakati huo huo waweze kufanya kazi zao za kisiasa kadri wanavyoona inafaa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa.
Ningeomba muwe specific kabisa kwamba Chadema wanatakiwa kufanya nini katika mazingira haya kandamizi ambayo kila mmoja anayaona kwa macho yake, kwamba Chadema kufanya shughuli za kisiasa Iringa tarehe 02/09/2012 ni haramu lakini ccm kufanya shughuli za kisiasa Bububu siku hiyo hiyo ni halali.
Mourinho,Well said Mkandara
Tuna matatizo makubwa kwenye mfumo wa utawala na kubwa zaidi ni nchi kukosa falsafa inayotuongoza. Haya matukio ni dalili tu za ugonjwa tunaoumwa kama jamii na kinachosikitisha zaidi ni jitihada nyingi zimeelekezwa kwenye kujaribu kuzitibu hizi "dalili" za ugonjwa bila kuutibu ugonjwa wenyewe na bahati mbaya dalili zipo nyingi, ukiacha "UCCM na UCDM" tuna "UKRISTO na UISLAM" tuna "UKANDA",wenye vipande chungumbovu ndani yake, na nyingine zitaendelea kujitokeza kila uchao.
Mourinho,
Kuhusu swala la Nchi kukosa falsafa inayotuogoza.
Nadhani hii kuna wakati imejadiliwa hapa kama mada iliyeelta hoja na mitizamo mbalimbali!
Kuna ambao walidhani kuwa hili sio tatizo la msingi kwani kinachotakiwa ni uogozi unaotoa matokeo ya kazi iliyofanywa. Kuna wengi ambao waliunga mkono dhana hii Mimi nikiwa mmoja wao na kumbuka hara Mkandara aliona hii kama hoja.
Mkuu nadhani tusaidiane sasa! Falsafa ya Taifa iwe ni ipi? Tunaitoa wapi?
Mourinho,
Kuhusu swala la Nchi kukosa falsafa inayotuogoza.
Nadhani hii kuna wakati imejadiliwa hapa kama mada iliyeelta hoja na mitizamo mbalimbali!
Kuna ambao walidhani kuwa hili sio tatizo la msingi kwani kinachotakiwa ni uogozi unaotoa matokeo ya kazi iliyofanywa. Kuna wengi ambao waliunga mkono dhana hii Mimi nikiwa mmoja wao na kumbuka hara Mkandara aliona hii kama hoja.
Mkuu nadhani tusaidiane sasa! Falsafa ya Taifa iwe ni ipi? Tunaitoa wapi?
Well. It depends on what it means when they say public security and protecting life. Ukiangalia kiundani unaweza kuona kuwa sasa hivi polisi wetu ni source ya insecurity...unajua polisi wetu wanaua, wanapiga, wanatesa, wanatishia, wanadai rushwa kwa nguvu wakati mwingine kwa kutumia silaha....these do not show that the force is for public security as it claims.
AshaDii,
Today the Journalist has been killed. I am pretty sure some sympatheziers of the ruling party will continue to support police's actions no matter what you tell them.
The truth is the police force still uses the colonial manuals to train its personnel. So the tradition is police are above the law and they can do anything against innocent civilians.
AshaDii
"Never get angry. Never make a Threat. Reason with People" -God Father/Mario Puzo
I no longer support state investigations by forming the so called tume. Kwanza report zake hatuzisikii na hakuna msaada wala mabadiliko yoyote tume hizo zimeshaleta so far.
Ila nakubaliana na Mario Puzo...never show anger to your enemies...treat them with respect ili siku ukiwarudi heshima iendelee kuwepo
Hoja yangu kwenu wakuu AshaDii na MAMMAMIA ni moja tu;
Ningeomba muwe specific kabisa kwamba Chadema wanatakiwa kufanya nini katika mazingira haya kandamizi ambayo kila mmoja anayaona kwa macho yake, kwamba Chadema kufanya shughuli za kisiasa Iringa tarehe 02/09/2012 ni haramu lakini ccm kufanya shughuli za kisiasa Bububu siku hiyo hiyo ni halali.
Azimio Jipya,
Falsafa has got nothing to do with what's going on. In 70s when the country was fully of philosophical cliches, but the police force behaved the same way. Do you remember mauhaji Shinyinga? Do you remember mauhaji Kilombero?
In old days we didn't have instant communication or for that matter freedom to speak.
Nakubaliana na Mario Puzo Pia, ila at the end of the day hata kama haoneshi anger ni mtu wa kuchukua 'action' mradi apata kile ambacho kapanga. Katika hili naweza tumika msemo ambao naukubali sana katika kupanbana na adui hasa katika vita (toka katika kitabu cha The Art of War), ni ya centuries ago but still applicable to any war which could ever occur.
"If your enemy is secure at all points, be prepared for him. If he is in superior strength, evade him. If your opponent is temperamental, seek to irritate him. Pretend to be weak, that he may grow arrogant. If he is taking his ease, give him no rest. If his forces are united, separate them. If sovereign and subject are in accord, put division between them. Attack him where he is unprepared, appear where you are not expected." - sun wu (Chinese Military Strategist).
Azimio Jipya,
Falsafa has got nothing to do with what's going on. In 70s when the country was fully of philosophical cliches, but the police force behaved the same way. Do you remember mauhaji Shinyinga? Do you remember mauhaji Kilombero?
In old days we didn't have instant communication or for that matter freedom to speak.
Let me ask you guys this question. Do you think if CHADEMA takes power, the police force or for that matter our security forces will behave differently?
Zakumi,
Let me give you an answer. Do you remember the mutiny of 1964? Nyerere used that as an opportunity to retrain our army and it became the peoples army. When we take over we will retrain the police force to become the people's police and not the fisadi police.
Falsafa ndiyo ingeamua nini kiwepo au kitokee nini kwa wakati gani!
Ni zaidi ya Dira ama msingi! Ni JINSI GANI TUNAPASWA KUISHI kwanini, kwa namna gani, ili iwe nini na kwa nani! Hapo ndipo Falsafa kuu inapohitaji kufanywa maisha yetu halisi, yaani kuanzia ngazi ya imani, mila, desturi, itikadi, mitazamo, mienendo, vitendo, n.k. vitakayosadifu na kufungwa na falsafa kuu. Kisha hayo yatazaa sera bora kusadifu na kufungwa na falsafa kuu, sera hizo zitazaa sheria zitakazosadifu na kufungwa na falsafa kuu, sheria hizo za kiuchumi, siasa na utamaduni zitazaa mfumo utakaosadifu na kufungwa na falsafa kuu! Hapo kila kitakachotokea, au tutakachotaka kufanya, kitapimwa kwa mizani ya falsafa yetu kuu!
TUJIULIZE LEO:
Ni falsafa ipi ituongozayo, itufungayo na kututambulisha?
Sheria zinatungwa kwa jinsi watu wajisikiavyo tu, ameshawishiwa na mkewe ama rafiki yake mweupe, anasimama jukwaani "tunataka rais asishtakiwe 'katiba iseme' " wengine nao "tunataka utawala wa majimbo" hawa nao "tunataka serikali tatu/mbili/1"
laiti kama tungekuwa na Falsafa yetu, kusingekuwa na malumbano yasiyokuwa na msingi kama yale yanayotokea Dodoma! Kila mtu angepima mawazo yake katika kupata mashiko kwenye falsafa yetu! Kama ameyaona anayawasilisha kwetu.
Ninaamini kabisa haya yatokeayo leo, yasingekuwepo kama tungekuwa na falsafa yetu, labda tu kama ingezaliwa kutokana na HULKA za binadamu na si MANTIKI ya mambo, naita UTU!
Taifa pasi na Falsafa bora, raia wake huongozwa na HULKA na MATAMANIO yao, na hapo UKINZANI ndipo uibukapo, ni chuki na visasi, hofu na umungu kila mtu atapigania kuwa juu ya mwenzake, mauaji kama pombe...matabaka, unyonge, n.k Haipo Falsafa ya kutufunga!
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani, anaita sasa!