Kifo kupitia mikono ya POLISI – Kosa la Marehemu?

Mkandara,

I knew when I mention falsafa, you will come out screaming. You know what not having a falsafa is a falsafa in itself, and in some instances in the best falsafa of all. Kwikwikwi.

Police brutality is something that all of us, regarding our polical affliactions, need to discuss. Expecting that if CHADEMA wins, the party will reform the police force is putting all of your eggs in one basket.
 
Last edited by a moderator:




Mkandara. Zakumi na JingalaFalsafa, KUHUSU FALSAFA YA TAIFA!

Guys lets just be serious for some seconds!

1. Awali Mkandara ulituambia kuwa tuna various DIFFERENCES at individual level which form DIVERSITY at a community a Nation level.

2. THEN, Ukapendekeza kuwa tutafute kitu ambacho ni COMMON out of all differences which can form our community with its diversity respected and well taken care!

3. JangalaFalsafa anakubaliana na Mimi kuwa that COMMON UNITY which unity us all Should be UTU whatever that term stand for!

4. JangalaFalsafa ameonyesha jinsi ya kujenga sera, mifumo and policy from UTU which will meet the need of the TOTAL DIVERSITY! WHICH CAN BE TERMED AS FALSAFA YA TAIFA!

5. FALSAFA YA TAIFA, kama Zakumi ataniruhusu kuuita UTU WA TAIFA Haitapingwa na CCM, CHADEMA, WAKRISTO, WAISLAM, POLISI,WAPAGANI,MAKABILA, UKANDA,MASIKINI, TAJIRI ... NAME ALL THE DIVERSITIES !!!Haitapingwa maana jamii nzima itaelimika juu ya dhani hiyo na kuiona ya thamani kubwa kuliko hata tofauti zao.

6. Elimu ifanyike kuwaamsha Watanzania kuhusu umoja wao ambao hauwezi kupuuzwa wala kuchezewa na chochote kile ndani ya kuheshimiana na kuridhiana kwenye kila tofauti zetu na kutukuza umoja wetu kwa kila hali.

Je hii ndio namana ya kejenga falsafa ya Taifa itakayo liokoa taifa hili lisitumbukie kwenye giza kubwa lililoko mbele yake?
 
AshaDii,

Nimesoma sana where I have blued! Inaonekana una insight fulani but honestly simalizii kujua kabisa kabisa kuwa nini hicho kimekusumuka kusema hivo? Najua hujali kufafanua ... !
 
Last edited by a moderator:

Is it a concidence you read the books that I read? Adui yetu wote ni mtu anayetaka kutuona tunasambaratishana kwa ajiri ya manufaa yake binafsi. Huyu tuombe Mungu amrudi na tumkate kwa nguvu zetu zote.
..
Ndahani,

Nimwekea buluu sehemu hiyo! Adui yetu wote ni mtu anayetaka kutuona tunasambaratishana kwa ajili ya manufaa yake binafsi!

Mara ya kwanza nilifikiri nimeelewa vizuri na kuwa huu mtizamo utatufaa kama Taifa! Ghafla nikagundua kuwa CDM Watautumia kwa Mtizamo wao, CCM hivyo hivyo Polisi nao hivyo hivyo ....
 
Last edited by a moderator:
Azimio Jipya,
Adui yetu wote ni mtu anayetaka kutuona tunasambaratishana kwa ajiri ya manufaa yake binafsi
Unaona jinsi msemo huu unavyoweza kutubabaisha..Tunaposema Adui yetu? huyu adui ni nani maana CCM wanaweza kusema hivyo, Chadema wanaweza kusema hivyo, CUF, Waislaam, wakristu, Wahindi, waarabu, weusi au Wazanzibar wanaweza kusema hivyo...Na hii yote inatokana na sisi kutojitambua kama Taifa moja na watu gani. Hadi leo hii we have nothing in common isipokuwa politics zetu zinaelemea ktk KUTAWALA ama KUTAWALIWA ktk mipaka ya nchi huru.

Unajua kwa nini Nchi za majirani zinatupiga bao leo hii?.. Ni kwa sababu wanajijua wao ni WATU gani na nini ethics na Values zao. Kenya hudai sehemu ya Tanzania kuwa yao kutokana na kuwajali makabila yao yaliyomo tanzania, Uganda, Malawi na hata Kongo hutanguliza kutazama WATU wake wamefika mipaka gani kufikia kudai ardhi hizo wakati sisi tunatazama ramani na kujaribu kuilinda mipaka hiyo.. In fact hatuna ushahidi pale mipaka inapoonyesha kula kwetu kama swala la Malawi..

Ujamaa ulikuja na mazuri yake mengi tu lakini pia Ujamaa ulitujenga kuwa kitu kisichokuwepo leo hii. Enzi za mwalimu hatukuwahi kuulizana kabila au dini lakini leo ni jambo la kawaida kabisa lakini tumefungwa akili zetu kutazama nje ya Ujamaa kwa kuendelea kuaminishwa kwamba sisi bado ni wajamaa wakati sio wajamaa bali wabinafsi. Hivyo CCM wanajitenga kama wao, Chadema wanajitenga kama wao, Polisi wanajitenga kama wao nasi walalahoi tunajitenga kama sisi na kila mmoja wetu akitazama maslahi yake.. UBINAFSI ndio sumu ya yote haya na ndio UTU unapotakiwa - Kushikamana, kupendana na kushirikiana kama Watanzania ni mada nzito zaidi ya utunzi wa falsafa yenyewe. Na ndio maana hata hiyo Katiba mpya tunayoitegemeahaitaweza kuondoa kero na karaha zetu kama haitawezi kutambua kwanza sisi ni WATU gani na tupo ktk mazingira gani. Nachoamini mimi sisi wote ni maskini.. Hivyo falsafa yetu lazima izingatie Umaskini wetu kwa kuwalinda watu maskini ambao ukombozi wao utatokana na umoja wao.

Tulipokwama hatuwezi kutoka ikiwa sisi maskini wote hatutakuwa na agenda moja. Zama za Mwalimu maadui wetu wa nje walikuwa ukoloni mamboleo - Mabeberu Imperialists), Kupe wanyonyaji (wawekezaji) na kdhalika kisha maadui wetu wa ndani walikuwa Umaskini, Ujinga na Maradhi.. Leo hii nambie maadui wetu ni kina nani? kila mmoja wetu atamnyooshea kidole Mtanzania mwenzake kwa sababu ni CCM, Chadema, Muislaam, Mkristu, Mwarabu, Mhindi, Tajiri, Maskini, Mbara au Mzanzibar yaani tumerudi ktk hali mbaya sana kuliko wakati wote wa Utawala wa Nyerere.
 

Mkandara
,

Hakika mtamshi hayo yamenifikirisha sana!

Nikajiuliza hivi KIONGOZI wa Tanzania leo ni nani? Nikimaanisha Rais anatuongoza toka wapi kwenda wapi ? Mawaziir na Wabunge wanatoa jamii ya Watanzania toka wapi kwenda wapi?

Watakuwa na MAJIBU yao tayari tayari ... Nitasubiri Wayatoe hayo majibu. Niwaulize Huko mnakotupeleka ndiko uliko umoja wa Watanzania? Huko mnako tupeleka ambapo ndio umoja wa Watanzania pana upana na ujazo wa kutosha kuzibeba Tofauti zetu kwa heshima na maridhiano.

Kiongozi wa siku zijazo wa nchi hii ...

Anakazi Moja ... KUUTAFUTA UMOJA HUO WA KWELI.

Pili. Awe na uwezo wa Wa Kuubebesha Umoja huo TOFAUTI hizo kwa DHATI!

Vinginevyo Atatuogoza kwenda wapi kutoka wapi? Haijalishi atatoka Chama gani, dini gani, ngozi yake ya rangi gani, katokea pwani au Kanda ya milimani, shabiki wa simba au Yanga ... nk

Lazima awe na uwezo wa Kuwaunganisha Watanzania kwenye umoja wao ambao yeye ana uamini kwa MOYO NA AKILI zake kama ilivyo kwa Watanzania wote!

Swali linakuja tena na tena ...UMOJA WA WATANZNAI NI UPI? WATANZANIA WANUGANISHWA NA NINI? Tofauti zetu hazina shaka ziko nazitaendelea kuwepo na kuogezeaka tena na tena. Tuamini tu kuwa umoja wetu ukishapatikana utazibeba ...

TAFAKARI YA KINA NI HII!!


Watanzania Wa leo TUNAUNGANISHWA NA NINI?
 

Kwahiyo adui yetu sote ni nani mkuu?
 

Mkandara, hata mimi sikujua nimesema nini mpaka mlipoangalia sentesi ile kwa undani zaidi. Ubinafsi ndio chanzo cha matatizo yote.Nguvu nyingi zinazotumika leo kuzima watu wasihoji, ukiangalia sana zinalenga kulinda ubinafsi na maslahi ya watu wachache.
Kweli Tanzania ya kweli ilikwisha ujamaa ulipobwagwa chini.Sasa hivi njaa zetu ndio zinatoa mwelekeo wa nini as individuals tunataka kufanya.
 
Watch this Guy carefully huyu mwenye pensi, picha ya kwanza na ya pili yupo akiwa amenyoosha bastora juu. what was mission of this Guy!!??



 

Mkuu nachelea kusema chochote kwa sababu swali lako linahitaji fikara nzito na sahihi na tena ziwe collective. Falsafa ya Taifa/Jamii lazima iakisi mazingira halisi ya hiyo jamii ili iwe na uhalisia na itoe mwongozo sahihi kwa jamii husika. Nikiangalia Jamii yetu ya leo,kwenye nyanja zote(utamaduni,siasa na uchumi)sioni ni nini haswa kinachotutambulisha kama jamii, zaidi ya kundi la watu waliopuuzia elimu,utu na maadili yao hivyo kuzaa jamii ya watu wenye akili nyepesi nyepesi,wanaoongozwa na tamaa za mwili na wanaokwenda kama kuku aliyekatwa kichwa. Sasa kwa mazingira haya hii falsafa yetu itaakisi kitu gani kitakachotuwakilisha kama jamii? Na kama tukipata mawazo mazuri kama ya Mkuu MKANDARA na JINGALAFALSAFA je ni kwa namna gani tutaya-set in motion ili yasiishie tu kuwa nadharia nzuri.
 
Last edited by a moderator:

Azimio Jipya and Inc.

I think now I understand where you guys stand when it comes to the use of the term falsafa. You don't take it rigorously to imply a proposed utopian society or country that forces people to live like clockwork. Please enlighten me if I am still shooting the blanks.

Now concerning the topic at hand, I think we are hypocrites. For example two weeks ago here in Washington, Mr Sugu told us that he can't take the blame for Mwembechai killings. For he wasn't the member of parliament.

Do you really need to be an MP to condemn what's bad? I believe you don't and before I proceed let me quote the Rev. Martin Luther King Jr.

History will have to record that the greatest tragedy of this period of social transition was not the strident clamor of the bad people, but the appalling silence of the good people.

I believe one of the falsafa that Tanzanians need to nurture, especially during this difficult times, is to speak out against the use of brutal force or injustice. For examples, muslims should speak out against injustice committed against christians and vice versa. Sukumas should speak out against injustice committed against Makondes.
 
WATANZANIA WA LEO TUNAUNGANISHWA NA NINI?

Kwanza niseme wazi kuwa "WATANZANIA WA LEO HAWAFUNGAMANI KWA CHOCHOTE" KILA MTU YUKO MBALI SANA KUTOKA ALIPO MWENZAKE! Yaani "TUNAKINZANA" ni kama pande sawa za sumaku zinavyokimbiana!

Swali ni "KIPI HASA KINAPASWA KUTULETA PAMOJA KAMA WATANZANIA?

*Je, ni uislamu? Mbona nao una matawi tena hasimu?
*Je, ni ukristo? Mbona nao una waliookoka dhidi ya wasiookoka? Nuru na giza havichangamani.
*Je, ni Siasa iliyopo? Yaani demokrasia? Mbona haisadifu hata chembe ya watu wetu? Wangapi wenye ufahamu nayo? Zaidi ya 90% ya watanzania, hatuijui Demokrasia! Elimu nayo haipo? Imani nayo haipo? Matumaini nayo hayapo? Ni NANI HASA ANAYOFAIDIKA NAYO KAMA SI KIKUNDI CHA WATU WACHACHE, je hautaibuka UKINZANI hapo?
*Je, ni Uchumi huu uliopo? Uchumi huruhusio kumshindanisha mbio Kinyonga dhidi ya sungura, au masumbi Cheka dhidi ya Wema Wepetu, kwa madai ya Fursa Sawa! Eti UHURU-HAKI. Nani kasema? Je, ni HULKA-HILA ama MANTIKI?​

+Kila kitu kinajenga UKINZANI KWETU, sasa... Kipi hasa KUTUUNGANISHA?
Hapa ndipo linapoibuka hitaji la kuwepo kwa FALSAFA KUU YA TAIFA, kutuleta pamoja! Ili binadamu asikinzane na mwenzake, ni "LAZIMA" sio HIARI, ni LAZIMA aishi KUFIKIRIANA na mwenzake! Sasa kipi kitatufanya TUFIKIRIANE? Unapotaka kuchimba choo karibu na kisima akitumiacho mwenzako, ukatafakari athari yake kwa jirani yako "reasoning", kisha ukaacha ukatafuta sehemu nyingine kwa kugundua utachafua kisima, MANTIKI itakuwa imetumiwa nawe katika maamuzi yako, mimi naiita UTU! UTU ni KUFIKIRIANA-KUTOKINZANA, ni kuwepo kwa Uuwiano Sahihi wa namna yetu ya kuishi pamoja. Basi kumbe UTU ndio upasao Kuunda Falsafa yetu ili kutuunganisha!

WAPI IPO MANTIKI-UTU?
Kwa asili tangu binadamu kuumbwa, amejaliwa mambo makuu mawili NAFSINI MWAKE! Ni HULKA, ambayo siku zote ni HASI na MANTIKI...ambayo siku zote ni CHANYA.

Kwa kutumia UTASHI tuliozaliwa nao pia, binadamu ana uwezo wa kutenganisha na kuyatambua vizuri mambo haya...Nafsini mwake mtu, na kuyafanya hai, katika vitendo! Hapa ndipo tunapotakiwa kuhoji juu ya kile tukiishicho leo, je ni zao la Hulka zetu ama Mantiki?
Na hapa ndipo tunapopata jibu la ADUI YETU HASA NI NANI, aliyetugawa?

Sioni MANTIKI yote katika Siasa, Uchumi wala Utamaduni tuupigania, ni HULKA za watu tu katika kila kitu! Hulka ya kutaka KUJIKWEZA, UMIMI, UBINAFSI, ndio mama wa kila kitu cha leo. Si ukristo wala uislamu, si demokrasia wala haki, si uchumi wala teknolojia, n.k.

Kumbe basi, ipo sehemu ambayo MANTIKI imekiukwa na kugeukia upumbavu -HULKA, na hapo si kwingine ila NAFSINI MWETU! Kumbe ADUI YETU WA KWANZA, ni NAFSI ZETU WENYEWE!

Nafsi zilizonafiki na kusaliti MANTIKI iliyomo ndaniye. Nafsi yangu ndio mimi mwenyewe! Ni lazima tujitakase kwa kupigania MANTIKI.
Tujenge umoja wa taifa letu, sisi WAAFRIKA wa Tanzania.

Kauli hii ni ngumu kidogo kuisema lakini kwangu ndio ukweli wenyewe, na ipo siku itatimia "TUTAANGUSHA DEMOKRASIA, MISIKITI na MAKANISA yatapewa raia kufugia kuku" hili ni katika kuishi MANTIKI KUU, yaani UTU. Thamani ya UTU hailingani hata kwa gharama ya damu ya mtu au watu milioni! Mantiki inapofikia ukamilifu wake, na kusema chinja hawa na hawa, SI DHAMBI KUTEKELEZA, na huo ndio UTU!

Mungu wetu anaita sasa!
 

Jasusi,

My take on when CDM takes over, the major change of all overall change in the system will be a brand new party in ruling for the first time since independence. The change in Tanzania and its citizens will be for the better (minimally) or for the worse (crucially) depending on how the major problematic issues in each sector will be tackled by CDM. While my belief is that it will be briefly for the worse... We should just brace ourselves for whatever is in store for us.

I genuinely don't believe that there will be so much change to the extent that everything will be alright overnight, It will take time with a combination of other lubricating factors. I believe there will be hard work and the times more complicated that they are right now. I also believe that MOST CCM leaders (some even considered as the so called 'Fisadi' will also be in the CDM action pic with the CDM's leaders blessings (whether visibly or under the carpet)

Nashindwa kuelewa kwa wale wenye kasumba ya kufikiria kuwa CDM ikija kila kitu kitakuwa sawa... Na kwamba Police watawasiliza wananchi kuliko viongozi wa serkali. Nakataliana na hilo, mambo mengi yatakuwa vile vile (na I say it confidently kabisa na God willing after years I am hoping to come back to the post and declare 'I said so').

I may be too cynical but that is what I believe. Hapa what matters ni kuwa wao CDM wakija maamuzi watayotoa will they be selfish to themselves or selfless?
 
zomba,

Nimeona picha uliotowa na ujumbe wake ambao naomba ninukuu "ILANI ILANI ILANI ILANI Watu wote mliokusanyika hapo maamriwa na Serkali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuondoka kwa haraka na kwa amani la sivyo tutatumia nguvu" Kwa kutumia picha hii ambayo ni msingi naomba kama hutajali nijuze haya:


  1. Kuwepo kwa kutumika hio Ilani iliyotolewa, je ina justify kipigo ama jinsi alivo uwawa marehemu Mwangosi?
  2. Naomba nijue msimamo wako wa tukio lote lililotokea Iringa na juu ya Kifo cha Marehemu Mwangosi.
  3. BTW katika vurugu zote ambazo hutokea kwenye mikutano ya CDM kwa mtazamo wako nani anatakiwa kulaumiwa kati ya police na CDM na hasa zaidi am more interested in understanding why wakulaumiwa alaumiwe kwa vigezo gani.
 
Last edited by a moderator:
Is it a concidence you read the books that I read? Adui yetu wote ni mtu anayetaka kutuona tunasambaratishana kwa ajiri ya manufaa yake binafsi. Huyu tuombe Mungu amrudi na tumkate kwa nguvu zetu zote.

Usisahau na baadhi ya movies mkuu... hahaha!

AshaDii,

Nimesoma sana where I have blued! Inaonekana una insight fulani but honestly simalizii kujua kabisa kabisa kuwa nini hicho kimekusumuka kusema hivo? Najua hujali kufafanua ... !

Azimio, Never Get Angry, Never make a Threat, Reason with people... Haina maana kuwa huyu mtu hana hasira, kuwa ni mpole daima or kuwa yeye ni mtu wa ku reason kwa kila jambo. Maana yake haipo hivo literally, ila msingi wake ni kuwa unapo deal na vitu vya msingi hasa ukitaka ku achieve kitu flani kwa mtu haitakiwi utumie hasira hata kama huyo mtu anakuboa, kukuchosha ama kukujudge.

Always keep calm, but upande wa vitendo ni otherwise... Una busara, una simile, hulipuki ovyo ila ACTION thats a whole another lever.... Kama kiongozi nikichukula model ya Don Corleone wa "The God Father" naweza sema inatakiwa uwe JK on the surface and Hitler underneath.
 
….kuelekea …. FALSAFA YA TAIFA

WATANZANIA WA LEO TUNAUNGANISHWA NA NINI?

Kwanza niseme wazi kuwa"WATANZANIA WA LEO HAWAFUNGAMANI KWA CHOCHOTE" KILA MTU YUKO MBALISANA KUTOKA ALIPO MWENZAKE! Yaani "TUNAKINZANA" ni kama pande sawa zasumaku zinavyokimbiana! Swali ni "KIPI HASA KINAPASWA KUTULETA PAMOJA KAMA WATANZANIA?"

· Je, ni uislamu? Mbona nao una matawi tenahasimu?

·
Je, ni ukristo? Mbona nao una waliookoka dhidiya wasiookoka? Nuru na giza havichangamani.

· Je, ni Siasa iliyopo? Yaani demokrasia? Mbonahaisadifu hata chembe ya watu wetu? Wangapi wenye ufahamu nayo? Zaidi ya 90% yawatanzania, hatuijui Demokrasia! Elimu nayo haipo? Imani nayo haipo? Matumaininayo hayapo? Ni NANI HASA ANAYOFAIDIKA NAYO KAMA SI KIKUNDI CHA WATU WACHACHE,je hautaibuka UKINZANI hapo?

· Je, ni Uchumi huu uliopo? Uchumi huruhusiokumshindanisha mbio Kinyonga dhidi ya sungura, au masumbi Cheka dhidi ya WemaWepetu, kwa madai ya Fursa Sawa! Eti UHURU-HAKI. Nani kasema? Je, ni HULKA-HILAama MANTIKI?

+Kilakitu kinajenga UKINZANI KWETU, sasa...?

Kipi hasa KUTUUNGANISHA?

Hapa ndipo linapoibuka hitaji lakuwepo kwa FALSAFA KUU YA TAIFA, kutuleta pamoja! Ili binadamu asikinzane namwenzake, ni "LAZIMA" sio HIARI, ni LAZIMA aishi KUFIKIRIANA namwenzake!

Sasa kipi kitatufanya TUFIKIRIANE?Unapotaka kuchimba choo karibu na kisima akitumiacho mwenzako, ukatafakariathari yake kwa jirani yako "reasoning", kisha ukaacha ukatafutasehemu nyingine kwa kugundua utachafua kisima, MANTIKI itakuwa imetumiwa nawekatika maamuzi yako, mimi naiita UTU! UTU ni KUFIKIRIANA-KUTOKINZANA, ni kuwepokwa Uuwiano Sahihi wa namna yetu ya kuishi pamoja. Basi kumbe UTU ndio upasaoKuunda Falsafa yetu ili kutuunganisha!

WAPIIPO MANTIKI-UTU?

Kwa asili tangu binadamu kuumbwa, amejaliwamambo makuu mawili NAFSINI MWAKE! Ni HULKA,ambayo siku zote ni HASI na MANTIKI...ambayosiku zote ni CHANYA. Kwa kutumia UTASHI tuliozaliwa nao pia,binadamu ana uwezo wa kutenganisha na kuyatambua vizuri mambo haya...Nafsinimwake mtu, na kuyafanya hai, katika vitendo! Hapa ndipo tunapotakiwa kuhoji juuya kile tukiishicho leo, je ni zao la Hulka zetu ama Mantiki?

ADUI YETU HASA NI NANI?

Na hapa ndipo tunapopata jibu laADUI YETU HASA NI NANI, aliyetugawa? Sioni MANTIKI yote katika Siasa, Uchumi walaUtamaduni tuupigania, ni HULKA za watu tu katika kila kitu! Hulka ya kutakaKUJIKWEZA, UMIMI, UBINAFSI, ndio mama wa kila kitu cha leo. Si ukristo walauislamu, si demokrasia wala haki, si uchumi wala teknolojia, n.k.

Kumbe basi, ipo sehemu ambayo MANTIKIimekiukwa na kugeukia upumbavu -HULKA, na hapo si kwingine ila NAFSINI MWETU! Kumbe ADUI YETU WAKWANZA, ni NAFSI ZETU WENYEWE!

Nafsi zilizonafiki na kusaliti MANTIKI iliyomondaniye. Nafsi yangu ndio mimi mwenyewe! Ni lazima tujitakase kwa kupiganiaMANTIKI.

Tujenge umoja wa Taifa letu, sisiWAAFRIKA wa Tanzania.

Kauli hii ni ngumu kidogo kuisemalakini kwangu ndio ukweli wenyewe, na ipo siku itatimia "TUTAANGUSHADEMOKRASIA, MISIKITI na MAKANISA yatapewa raia kufugia kuku" hili nikatika kuishi MANTIKI KUU, yaani UTU. Thamani ya UTU hailingani hata kwagharama ya damu ya mtu au watu milioni! Mantiki inapofikia ukamilifu wake, nakusema chinja hawa na hawa, SI DHAMBI KUTEKELEZA, na huo ndio UTU!


JingalaFalsafa, nimepata HOJA yako, ... Natafakari!
 
Last edited by a moderator:

1. Kumbuka haikuwepo ilani hiyo tu pekee, kwanza kabisa vyama vyote mkoani Iringa walishatangaziwa na Polisi wasifanye mikutano ya kisiasa wakati wa kampeni, wajizuie kwa wiki moja.

Ilani zilizotolewa zaidi ya hiyo ya kitambaa:


Halafu walitangaziwa siku ya tukio, licha ya hicho kitambaa cha ilani, walipewa ilani kwa njia ya vipaza sauti kuwa wasambaratike.

Kwa hiyo hili la Ilani utaona kuwa ni ukaidi ulifanywa makusudi kabisa na wanachadema wa Iringa, kwa nini? isitoshe:

Sasa wewe jiulize na ujibu, ikiwa mmepewa Ilani zote hizo na Polisi na mkakaidi na mkaingia kwenye vita na wao kwa dakika 30, halafu atokee mmoja hukohuko kwenye kundi linalipogana na Polisi aje amvae Mkuu wa kikosi, kwa nia yoyote ile, unafikiri kutakuwa na usalama kwake hapo?



2) Tukio lote lililotokea Iringa nalichukulia ni uvunjifu wa amani wa makusudi kabisa kwa "wapiganaji". Siasa sio kukaidi amri za Polisi kwa nguvu, hivi unategemea nini baada ya kuvunja amri za Polisi? Licha ya kuwawametangaziwa, hata ikitokea tu kuwa wamejikusanya kikundi cha watu ambapo polisi wanaona hapa kuna uwezekano wa amani kuvunjika basi wana haki ya kuwaambia watawanyike bila ilani yoyote ya kabla.

Sasa jiulize tena, hivi walikusudia nini hawa waliokaidi amri zote hizo na kupambana na mapolisi?

3. Ikiwa umeambiwa usifanye maandamano, ukayafanya kwa nguvu, ukatokea uvunjifu wa amani kwa polisi kuzuwia hayo maandamano, hapo unategemea nani alaumiwe?

Ikiwa unaambiwa usifanye mikutano siku fulani, wewe unaumuwa kufanya kwa nguvu wakaja polisi kuzuwia mkusanyiko huo ukakaidi na kupigana na Polisi ni nani wa kulaumiwa?

Conclusion:

Licha ya hoja zote hizo juu zinazoashiria uvunjifu wa amani wa makusudi kabisa, hata kwa bahati mbaya ukijikuta wewe ni mpita njia kwenye vurugu (riots) za namna hiyo na Polisi wameshatowa amri ya watu kutawanyika na wameshajipanga kuwafata na kuwatawanya wakitumia zana zao za kuzuwia fujo, usijaribu hata siku moja kuwafata wanapotokea na kuingia kwenye himaya yao kutokea walipo wanaotawanywa, kufanya hivyo ni:

1) amma kujitafutia kifo (suicide) kwa makusudi kabisa,

2) au kujitafutia kifo cha kujitowa mhanga (terrorism),

3) amma kujitafutia kifo kwa ujinga wa kwenda kuanzisha fujo na kutokujuwa namna ya kujihami yanapokushinda.

Chaguwa wewe ni yepi katika hayo yaliyomkuta Daudi?

Ukweli ubaki kuwa ukweli.
 

AshaDii,

In management theories, stepping aside and observing processes from afar is a good thing. For, it give individuals or group entities opportunity to learn and rectify their own problems.

With that in mind, I think CCM need to step aside. Not because they are bad, but because they have become complacent which isn't good for the country and the party itself.

Continuity that CCM want to maintain is an elephant or 800 pound Gorilla in the room which hinders reform and accountability. And the only way to get rid of that animal is therefore to reduce CCM's outreach or force the party to go into the opposition entirely.

Therefore, I support the efforts of CHADEMA and other opposition parties. But I am very realistic and don't expect overnight solution. For, the magnitude of our problems is huge.

Majority of leaders in opposition camps are activists not executives or technocrats. They have never run and excute a budget. They have never run a payroll to pay salaries. They have never controlled security and defend forces. So there's a learning curve that isn't going to be achieve in a year or two.

The inexperience of opposition is there. So even though we want the opposition to win, we should control and manage our expectations. For example, changing the working habits of civil servants include the police officers will take time.

Now back to my friend Jasusi, he is being disingneous when he tells me that they will reform the police force when CHADEMA take power. I don't buy that. For, the only time Nyerere reformed the defend forces was when they undermined his authority. Likewise, if the security forces serve well those in power, we shouldn't expect miracles.
 
zomba kuna wakati mwingine mkuu wangu sio lazima uchangie kitu hasa ktk maswala mazito kama haya kwa ushabiki wa chama. Uchadema na UCCM ni vitu vingine kabisa inapofikia kifo cha raia, mwananchi tena mwandishi wa habari ambaye hakuwa na silaha isipokuwa akiwa kazini. Zaidi ya hapo Polisi waliambiwa wazi kuwa huyo wanayempiga ni mwandishi wa habari na walimwona aki record pande zote mbili na mfarakano na hata huyo mkuu wa Polisi alimwona vile vile.

Unachojaribu kujenga hoja hapa ni sawa na sheria ya Makaburu (Apartheid) ambapo wananchi wafanyakazi waligoma kwenda migodini kwa madai ya nyengeza ya mshahara wakauawa bila huruma halafu kisheria ndio wenye kubeba lawama na makosa kusababisha vifo hata kama walikuwa wakidai haki zao pasipo kumshambulia mwenye mgodi ama kufanya fujo mgodini..Kuna vitu vya kutetea na hasa vinapokuwa vya kisiasa lakini sio hili.

na ifahamike tu kwamba hatuna madaraka mikoani, swala la sensa ni swala la Kitaifa, swala la Jamhuri nzima hivyo huwezi kutoa amri kuzuia watu kutofanya shughuli zao mkoani wakati nchi nzima watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida isipokuwa wneye dhamana ya kuhesabu ndio wanawafuata watu majumbani mwao na kuwahesabu. Ingekuwa hivyo basi hata wale waliokutwa hawapo majumbani wangekamatwa, wote walioenda kazini wakait wa kuhesabu wangewajibishwa vile vile. Ilani pekee iliyotolewa Kitaifa ni kwa wale watakao kataa kuhesabiwa.

Na Polisi hawahusiki kabisa na utoaji tahadhali ikiwa kamati ya sensa haikuomba kuahirishwa kwa shughuli zote nchini ama Iringa sizimamishwe ili kuwawezesha wafanye kazi kwa ufasaha na haraka.. Polisi wameingilia kazi isikuwa yao kwa sababu walijua ni Chadema tu mkoani Iringa waliokuwa na shughuli kati ya siku hizo. Labda nikuulize hilo bango liliandikwa lini na kwa ajili gani haswa? wapi sehemu nyingine liliwekwa?..Hii ina maana Polisi walijiandaa mapema kwa kuelewa watafanya nini...Hivyo wanaposema ilani ile ni kwa vyama vyote sidhani kama wanasema ukweli maana hapakuwepo na shughuli nyingine yoyote zaidi ya ile ya Chadema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…