Badluck. Baba yangu alihisi vitu vyote hivo. Ila hiyo ni gas, acid.
Na ni dalili moja kwa moja za shida ya moyo. Alipima ma ecg.
Hakuna kitu. Akapotezea. Mwaka baadae 2024 ghafla akiwa njiani anaendesha gari akazidiwa, akapelekwa hospitali. Zoezi. Likahamia shida ikawa moyo. With no direct answer. Akapewa madawa sijui kidonge kile cha kuweka chini ya ulimi.
Paap ghfla akasimama akarudi hospital akawa pressure ndiokinachomsumbua, akaambiwa anaendelea vizuri aendelee nadawa. Jumapili akatoka akaenda kanisani. Anaendesha gari.
Akarudi home akasema kitu kina mpanda kifuani.
Akasema reflux sijui. Akaenda hospital hakufanikiwa kukutana na doctor same sunday.
Paap jumatatu karudi ofisini. Strong kabisa. Akaandika barua za kustaafu, lakini akasema afanye safari ya mwisho ya kikazi.
Paap mpaka mji husika akafika salama salmini.
Saa 9 usiku akashtuka usingizini moyo unamuuma. Moyo unambana. Akanipigia simu almost 20minuts toka Hali ile ianze. Wakati naongea nae kwenye simu. Nampa moyo ajikaze, same time tunasubiri usafiri umfikie pale. Akakata kauli hakuweza kuongea, simu akashikamtu wa karibu.
Paap saa kumi na dakika zake naambiwa hayupo tena duniani. R.I.P BABA YANGU MPENDWA.
Hiyo hali boss wangu usiichukulie poa. Nenda JKCI