Kifuatacho baada ya Job Ndugai kujiuzulu, tukae mkao wa kula

Kifuatacho baada ya Job Ndugai kujiuzulu, tukae mkao wa kula

Gibeath-Elohimu

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2014
Posts
487
Reaction score
700
Natumai sote tuko poa na salama, hakika Mungu ashukuriwe Kwa rehema na neema zake.

Japo nchi na raia wengi wamepokea taarifa za kujiuzulu Kwa speaker wa Bunge Kwa taharuki na mshangao. Lakini swali la kujuiliza hapa, je, nini kutafuta/nini maana ya hii move Kwa maana ya mihimili ya nchi (Serikali, Bunge na Mahakama).

Hakika wengi wanaweza muona Ndugai kama amefeli hivi, Ila ukifanya analysis ya kiuongozi na kisiasa ni kama jamaa ama make a political trap Kwa serikali iliyopo.

Ni kama amatega mtego wa kufungua hoja za kuanzishwa Kwa vuguvugu na Katiba mpya.Kwa nini nasema hivi.Ukitizama Kwa umakini na Kwa kina ni dhahiri na wazi kuwa Ndugai hakufanya kosa kama muwakilishi wa mhimili huru wa BUNGE....japo wengi wanaweza sema namna aliyotumia kuwasilisha hoja yake haikuwa sahihi,lakini swali linakuja,je kuwasilisha huko kulimuondolea ukweli kuwa yeye ni spika wa Bunge....yaani mhimili huru wa nchi.

Move hii ni dhahiri ina inaibua hoja ya je NI kweli nchi yetu ina mihimili mitatu huru yenye Uhuru wa kuhoji na kushauri mhimili mwingine bila uwoga wala kificho.

Jibu ni hapana Kwa kurejelea kujiuzulu Kwa ndugu Ndugai.Hii ni wazi kuwa mhimili mmoja Una nguvu kubwa kuliko mihimili mingine.

Hivyo basi,kifuatacho hapa ni nchi kuingia kwenye mtego wa kuhoji utendaji wa mihimili hii mitatu inayounda taifa la Tanzania.

Swali ni je,nchi itanasa kwenye huu mtego au itajinasua.

Nawasilisha.
 
Lini kajiuzuru?
IMG_20220106_172334.jpg
 
Inahuzunisha kama sio kushangaza kwamba watu hawaoni kosa la Ndugai lililopelekea Rais kumnanga wazi hadi akachukia uamuzi wa kujiuzuru.

Ni kweli speaker ana nafasi ya kutumia Uhuru wake wa kutoa maoni as a normal Tanzanian. Alichokifanya alitumia Uhuru wake wa kikatiba kutoa maoni yake binafsi.

Lakini tunasahau Jambo moja kwamba kila Uhuru una mipaka yake hata Katiba inatamka wazi kuhusu haki za binadamu. Unapotoa maoni yako unapaswa kuangalia na viapo vingine ulivyoapa katika utekelezaji wa majukumu yako.

Ndugai akiwa bungeni akiwa anatekeleza majukumu yake hazuiwi kutoa maoni yake na amekuwa akifanya hivyo mathalani kwenye mambo mbalimbali hata Bandari ya Bagamoyo, kuhusu mjadala wa watoto waliopata ujauzito kurudishwa shule nk.

Tatizo linakuja pale anapotoa maoni yake nje ya bunge ingali yeye ni kiongozi wa mhimili ambao umepitisha hiyo hoja akiwa amesimamia mijadala yote halafu anaibuka nje ya bunge na kuongea namna Ile.

Sasa Rais ndio head of state, pamoja Kuna separation of powers lakini Katiba hiyohiyo inatamka Rais ni head of state maana yake Ndugai anawajibika kwa president despite ya kuwa head of one of pillars of the government.

Hapa unaweza kuelewa kwamba huwezi kuita wanahabari kumpinga boss wako maana Ndugai kama spika anakuwa mtumishi wa umma by virtue ya cheo chake.

Spika akiwa bungeni anakuwa "functus officio" hivyo haina shida Ila hawezi kuongea kumcrash boss wake nje ya bunge.

Pia kwenye chama Rais ni boss wake hivyohivyo anajikuta hawezi kumcrash Mwenyekiti wake nje ya vikao vya chama.

Kawaida ukitaka kumchallenge Mwenyekiti angepaswa kuongea kwenye vikao vya chama Tena yeye ni Mjumbe wa CC wangejadili kama hiyo anachofanya Rais anakiuka ilani ya chama.

Ndio maana wanaotaka kumchallenge Mwenyekiti huwa wanajitoa kwenye chama ndio wanaongea wanayoona wapo sawa.

Mzee Lyatonga Mrema baada ya kutokubaliana na Rais mzee Mwinyi alipoamua kumpatia mfalme wa uarabuni kitalu Cha kuwinda kule Loliondo kwa miaka 99 Mrema aliona hakubaliani na yale maamuzi ndipo alijiuzulu na akajitoa CCM ndipo akaita press conference kueleza sababu za kujiuzulu.

So in my personal view, Ndugai yawezekana ana hoja ya msingi Ila amekosea protocol ya kuwasiliana maoni yake.
 
Natumai sote tuko poa na salama,hakika Mungu ashukuriwe Kwa rehema na neema zake.

Japo nchi na rai wengi wamepokea taarifa za kujiuzulu Kwa speaker wa Bunge Kwa taharuki na mshangao.Lakini swali la kujuiliza hapa....je,nini kutafuta/nini maana ya hii move Kwa maana ya mihimili ya nchi (Serikali,Bunge na Mahakama).

Hakika wengi wanaweza muona Ndugai kama amefeli hivi,Ila ukifanya analysis ya kiuongozi na kisiasa ni kama jamaa ama make a political trap Kwa serikali iliyopo.

Ni kama amatega mtego wa kufungua hoja za kuanzishwa Kwa vuguvugu na Katiba mpya.Kwa nini nasema hivi.Ukitizama Kwa umakini na Kwa kina ni dhahiri na wazi kuwa Ndugai hakufanya kosa kama muwakilishi wa mhimili huru wa BUNGE....japo wengi wanaweza sema namna aliyotumia kuwasilisha hoja yake haikuwa sahihi,lakini swali linakuja,je kuwasilisha huko kulimuondolea ukweli kuwa yeye ni spika wa Bunge....yaani mhimili huru wa nchi.

Move hii ni dhahiri ina inaibua hoja ya je NI kweli nchi yetu ina mihimili mitatu huru yenye Uhuru wa kuhoji na kushauri mhimili mwingine bila uwoga wala kificho.

Jibu ni hapana Kwa kurejelea kujiuzulu Kwa ndugu Ndugai.Hii ni wazi kuwa mhimili mmoja Una nguvu kubwa kuliko mihimili mingine.

Hivyo basi,kifuatacho hapa ni nchi kuingia kwenye mtego wa kuhoji utendaji wa mihimili hii mitatu inayounda taifa la Tanzania.

Swali ni je,nchi itanasa kwenye huu mtego au itajinasua.

Nawasilisha.
Kuondoka kwa ndugai kumenifanya nione mapungufu mengi sana kimfumo

1 . Hii nchi ina mhimili moja tu hizi zingine geresha
2. Hoja za mashiko hazipewi nafasi
3. Tunako elekea wimbo wa katiba mpya tutaimba wote ...muda ni mwalimu mzuri
 
Back
Top Bottom