Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Kinaitwa kifungua kinywa, kizungu wanaita break a fast. Maana kwa masaa 10 au zaidi uliyokuwa usingizini mwili ni kama ulifunga.
Mashariki ya Kati utamaduni wao wa kifungua kinywa ni mikate, matunda ya mzaituni na dengu.
Warumi wa kale walifungua kinywa na mkate usio na chachu, tende, asali na zabibu.
Wasomi wa Kirumi ndiyo waligundua umuhimu wa virutubisha vya yai kwa kifungua kinywa. Walianza kula maya ya njiwa kabla hawajaanza kufuga kuku.
Kifungua kinywa chenye mayai manne kiliandaliwa kwenye officers mess. Ni wanajeshi kuanzia cheo cha Major ndiyo walipata hadhi ya kula kifungua kinywa hiki.