wa kupuliza
JF-Expert Member
- Jun 15, 2012
- 15,216
- 37,757
Usafi ukifanywa na mmlaka zinazohusika na ukawekwa utaratibu mzuri na unaoeleweka wa adhabu tutafanikiwa sana. Kiasi kwamba raia hawatasubiri kila J'mosi ya mwisho wa mwezi. Tatizo kuna mikwara ya kisiasa mingi, na sifa kwa watawala kana kwamba wao ndio wanafanya usafi.
Moshi na Iringa ni safi wakati wote, watu wameelewa na hakuna shida. Kila mfanya biashara yupo responsible na eneo lake la biashara. Huwezi kuta mchoma mahindi au mkaanga mihogo anaacha uchafu akimaliza biashara kwa siku, anachukua fagio na kusafisha kiasi kwamba huwezi gundua kwamba hilo eneo lilikuwa bize na biashara.
Sawa kabisa mkuu,shida wataalamu wanaingiliwa na wanasiasa kwenye shughuli zao.
Pita Arusha, Dar, Mwanza sehemu ambako wamachinga wameruhusiwa kufanya kazi zao, ikifika jioni wakishafunga shughuli zao uchafu waliouacha hapo unabaki mtu unashangaa tu.