Hongera NSSF na serikali kwa ujumla wake. Habari kama hii hauwezi ukapata wachangiaji wengi kwa vile wachangiaji wengi wameshazoea habari za ufisadi na zinazodhohofisha serikali. Tubadilike watz
Msanifu aliyechora daraja la Kigamboni ni kutoka Misri anaitwa Mohamed Shohayeb wa Arab Consulting Engineers
,Halina. Hawajazingatia watembea miguu kwani muda wao kuthaminiwa haujafika.
,<br>Maandalizi ya Bush kutwaa mradi wa Kigamboni Modern City,ngoja tuone kama kazi itafanyika
na haya magari yetu yasiyo na break nzuri basi ajari lazima magari yatatumbukia baharini tu. daraja hili inaweza kuwa chinja chinja nyingine hasa kwenye hiyo duaraInteresting. . .
Ngoja sasa tuone kama kazi itafanyika au la.
baskeli maguta na waenda kwa miguu watatumia vivuko. swali jingine?,
Hii inaonesha kuwa MJI WA KIGAMBONI UTAKUWA NI WA KIBEPARI ZAIDI na kuwa watakaokaa maeneno hayo ni watu WENYE MAGARI TU ! au siyo ? Naomba Mr NSSf anijibu tafadhali ...haingii akilini kujenga daraja ambalo halina sehemu ya waenda kwa miguu wala baskeli , ni wazi huo ni mji mtarajiwa wa KIBEPARI ! Mr.NSSF tafadhali nijibu nina shauku!
Nataka Mr. Nssf anijibubaskeli maguta na waenda kwa miguu watatumia vivuko. swali jingine?
Ndiyo ulikuwa wasiwasi wangu, halafu kuna mmoja wa waheshimiwa wetu alishawahi kusema kuwa wanasheria wetu hawana uzoefu wa mikataba ya kimataifa ndiyo maana tunaingia mikataba mibovu, kama haikuwa tu sababu isiyo na maana, sasa sijui kama hao waliosaini wameshakuwa na huo uwezo lakini kama haitoshi naogopa kile kipengele cha hata kama wakishindwa kujenga itabidi walipwe fidia ya kukatishiwa mkataba wao na zile charge za vifaa vya kuwapo nchini mwetu, Tunaomba mungu angalau hili daraja liishe iwe mfano mzuri na tupate angalau sehemu ya kupigia picha.Sisi tunataka kuona daraja kwani sas ni zaidi ya miaka mitano mnapiga porojo tu, Kusaini mkataba si kuanza kwa ujenzi.....Kinachotakiwa hapa ni daraja tu...Je huo mkataba na jamaa mmeusoma au mnatia tu sahihi?
ukiumwa na nyoka hata ukiona kiunyasi unaruka..... ha ha ha. Mimi siko huko ila nafikiria tu ile 10% ya 214b, duh.... kufa kufaana.Design iliyochaguliwa siyo hiyo kwenye picha zilizotangulia. Design hii ilikuwa ni kama daraja lingekatisha pale magogoni. Huo mduara ni kwa ajili ya kupandisha magari urefu ambao daraja lingebidi liwe kama lingejengwa hapo kwenye lango la bandari.
Design iliyochaguliwa iko simple zaidi. Ni design isiyohitaji daraja lililo juu sana kwa sababu linajengwa kule mbele ya kurasini oil depot, sehemu ambao meli kubwa hazifiki.
Pamoja na yote hayo, mimi najiuliza bei hiyo ya 214 Billion Shs na muda wa Miaka 3 kulijenga. Ni gharama kubwa mno na ni muda mrefu sana wa kujenga daraja la kilometer 4. Mimi nina wasiwasi kuwa hapa kuna ufisadi uliojificha kama ule wa twin towers. Tena ukizingatia ni pesa za NSSF, pesa za SU, a.k.a sizizo na mwenyewe...🙁
Pamoja na yote hayo, mimi najiuliza bei hiyo ya 214 Billion Shs na muda wa Miaka 3 kulijenga. Ni gharama kubwa mno na ni muda mrefu sana wa kujenga daraja la kilometer 4. Mimi nina wasiwasi kuwa hapa kuna ufisadi uliojificha kama ule wa twin towers. Tena ukizingatia ni pesa za NSSF, pesa za SU, a.k.a sizizo na mwenyewe...🙁
inatakiwa tumnadi mgombea wetu wa 2015, na moja kati ya vivutio (performance yetu) litakuwa ni hili daraja la kisasa kabisa East Africa and Central, Pia tutakuwa ndiyo tumemalizia mradi mkubwa kabisa wa MegaWatt 3000 na umeshaingizwa kwenye grid ya taifa ili kutomomeza kabisa tatizo la umeme liwe ni ndoto.it's politics kama kawaida yenu...huu mradi ulianza kupangwa tangu 1977 na mkandarasi alishapatikana tatizo mkasema ni ukosefu wa fedha, so mnataka kutuambia tangu 77 hadi leo 2012 ndio mmepata fedha?? kwa nini leo?? kwa nini uwe wa miaka 3 wakati fedha zipo na hao wachina wana uwezo wa kujenga kwa mwaka mmoja?? kila mtu anajua 2015 ni mwaka wa uchaguzi msituzuge.. matumizi ya kodi za wananchi ni pamoja na kujenga madaraja, barabara bora na kadhalika, toka mwaka 77 kodi za wananchi hazijatosha kufanya miradi kama hiyo?? acheni siasa.